Magufuli bila madaraka yukoje?

Mzee njoo ulisome tena hili bandiko.
 
Sasa waulize nini wakati ukweli wake bado unasimama?
Kwamba:

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile

Bado unayasimamia hayo maneno kuwa Magufuli bila madaraka si mtetezi wa rasilimali za nchi?
 
Asante sana JF kwa kutunza kumbukumbu. Katika jamii wako sadists na wako masochists na hata humu JF pia wapo. Ili uweze kufanikiwa katika kuumiza lazima wawepo wanaopata raha kuumizwa na kushangilia wenzao kuumizwa.
 
Hiyo b hapo mwishoni. Zamani ulikuwa na akili sana mkuu.
 
Swadakta
 
Nguruvi3 njoo utupe mrejesho wa haya maelezo yako kwa sasa.
Mkuu tindo
Kwanza, ahsante kwa kutenda haki ya kunisikiliza kabla ya 'hukumu'.

Pili, nasimama na bandiko langu ulilonukuu kwa mantiki yake,kwamba tunahitaji kiongozi mwenye 'discipline, vision, goals and action' kama nilivyomalizia.

Tunahitaji kiongozi anayesimamia kanuni na sheria na si anayetaka cheap popularity.
Swali, je, haya yanawahusu waliotajwa?

Tatu, kuna misemo ya watu maarufu inayoeleza kwanini bandiko langu linaweza kuwa na msimamo tofauti
Rais Lincoln wa US alisema '' If you want to test a man's character give him power ''
Kwa kiswahili kisicho rasmi, ukitaka kujua tabia ya mtu mpe madaraka

Lord Acton, British Historian alisema '' Absolute power corrupts absolutely'
Kwa kiswahi kisicho rasmi, mtu akiwa na madaraka juu ya watu au vitu, madaraka hayo humlevya''

Ni upi mrejesho wa maelezo yangu kwa sasa?
Ukisoma bandiko la asili, nimetumia neno '' Viongozi'' kwa maana ya Leaders na si Watawala (rulers)

Tunahitaji mfano wa kiongozi ni Nyerere. Pamoja na mapungufu aliyokuwa nayo kama mwanadamu, Nyerere alikuwa na sifa hizi, kuthamini Utu, kuthamini Maisha ya watu, kuheshimu haki zao na kuheshimu sheria.

Katika kipindi cha miaka kadhaa tangu bandiko la asili nimeshuhudia yale yaliyosemwa na Rais Lincoln na Lord Acton pamoja na yale aliyosimamia mwalimu Nyerere .

Hakuna usimamizi wa sheria kwa viongozi bali usimamiaji wa kisheria kwa watawala.
Mtawala haihitaji kufuata sheria anahitaji sheria zimfuate.
Kiongozi anasimamia sheria hata kama zinakwenda kinyume na matakwa yake

Kuna kubomoka kwa kwa taasisi za nchi. Mapungufu ya mihimili yetu yalikuwepo, lakini kwa kwa sasa ni kama vile mihimili imeungana. Natamani awepo mtu wa kunielimisha tofauti ya uvccm/uwt na Bunge au Mahakama!

Maendeleo ya kweli ni ya watu kuwa sehemu ya kujitawala(si kutawaliwa) ,sehemu ya kuongoza na ni huru katika kusema, kupanga na kushiriki bila vitisho au kuandamwa.
Wananchi wakiwa huru hata katika lindi la umasikini bado ni matajiri.

Mwisho, kupo kubomoka kwa misingi inayotufanya sisi tuwe Taifa.
Hatuwezi kuwa Taifa kukiwa na mbegu au hisia za kibaguzi , hofu na wasi wasi.

Kwamba, kutofautiana kimawazo ni kosa la jinai kama si uhaini.
Kwamba, uzalendo ni kuimba mapambio na si kuamini katika Utaifa unaotujenga sisi kama watu wamoja.
Kwamba, tunazidi kugawanyika katika misingi ya kikanda , kikabila, na itikadi zote za kidini na kisiasa.

Endapo hatuheshimu haki za watu kuishi kama inavyosema katiba, haki za kujieleza, kupokea na kutoa habari, kushiriki na kupanga. Kama hatuthamini maisha ya watu! maendeleo yoyote hayatakuwa na maana.

Tutahitaji kumuomba radhi mkoloni aliyetuheshimu hata pale tulipotofautiana naye kimawazo.

Hakumpiga Nyerere risasi kwa kusema arudi Ulaya. Mkoloni hakufunga watu kwa kushiriki siasa .

Kama ni hivyo, kwanini leo tunababaika kuiona tofauti ya kujitawala na ile ya kutawaliwa na mkoloni?

Nadhani maoni yangu yatakuwa yamejibu hoja yako

Ahsante
 
Maisha yanakwenda kasi sana aisee...
Uzi huu ulisadifu uhalisia.. najiuliza tu kwanini mambo yalibadilika baada ya mamvi kumpiga ngwala balozi yule!!???
 
Daaaah! Ukweli mtupu na roho mbaya pia (ile heri tukose wote!!!)

Mzee njoo ulisome tena hili bandiko.
Daaah watu wanafukunyua... 😀
 
Nadhani hapa ulikuwa hujajua kwa undani zaidi historia yake ya ubunge aliupataje, anapitaje bila kupingwa, miradi yake ya barabara nk jinsi inavyosimamiwa na kupigwa juu kwa juu.
Sasa bado na haya ya 2015 kwenda mbele
 
Mkuu huyo hajitambui hata chembe. Baada ya kuamua kuunga mapambio akawaruhusu pia wapakue ubongo wake wote sasa amebaki kuwa ZOMBIE tu wa kufukuzia teuzi.
 
Kwenye b ulipiga kunako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…