Nikiri kwamba kaanza vizuri sana lakini bado hajanishawishi, watanzania tunahitaji maisha bora na yenye uhakika, tunataka uchumi wa nchi ukae vizuri, tunataka vifaa vya ujenzi vishuke bei, tunataka pembejeo za kilimo zishuke bei, tunataka vyakula vishuke bei, tunataka mafuta yashuke bei ili kushusha gharama za usafiri, tunataka umeme wa uhakika na wa kiwango cha chini, tunataka maji ya uhakika, tunataka elimu ya uhakika ikiwemo kuboresha maslahi ya walimu, tunataka madawati na majengo kwa uhakika, tunataka huduma bora za afya nchi nzima, hapo nitaanza kukuunga mkono.