Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,073
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa mkoa wa pwani kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kwamba miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla inatekelezwa kama alivyoahidi.
Mhe. Rais ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati, ujenzi wa barabara njia sita Dar-Chalinze na ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge) ambao mipango ya ushirikiano katika utekelezaji na Ethiopia imeshaanza.
NOTE: Kwa msiofahamu mradi wa Stiegler's Gorge ni moja ya key priority projects zilizotajwa kwenye East African Power Master Plan. Huu mradi, pamoja na mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, utaiwezesha Tanzania kuwa power house ya Afrika Mashariki, ukizingatia kwamba grid za umeme za mataifa ya Afrika Mashariki sasa zimeunganishwa tayari.
Mradi utazalisha hadi MW 2100 za umeme, ambazo ni zaidi ya umeme wote unaozalishwa hapa Tanzania kwa sasa.
Viva JPM Viva Tanzania na Viva EAC!