Magufuli aufufua mradi utakaoweza kusambaza umeme Afrika Mashariki nzima!

Fufueni general tyres mwanzo acheni longo longo, kila mwaka mnatenga fedha tu...dah!
 
Kuna wananchi mnashangaza kutopenda maendeleo ya nchi yetu, kwa kuwa negative kwa kila kinachofanywa bila ya kuwa na subira!

Mkikaa kimya mtakuwaje na kuyafikiria humo humo kwenye vichwa vyenu!?

wengi wa hawa manyan'gau ni wale wa vijijini huko...Hawana lolote . Nafurahi kuona kuna wachache wanasimamia nchi na kulinda nchi.
 
Megawat 2100?..!!

Kwani sasa tunazalisha WATT ngapi?
vyovyote tutakavyozalisha kumbuka kwamba umeme wa maji kama maji yatakuwepo ya kutosha, ndio umeme wa bei rahisi zaidi kuzalisha kuliko huo wa gas. na mto rufiji unamwaga tu maji baharini hata hatuyatumii. kama akifanikisha huo mradi nitampongeza sana, maana kwa sasa sijaona alichofanya yeye binafsi (isipokuwa vile alivyovianzisha jk na yeye anavimalizia tu hivyo credit to jk), zaidi ya zile campus za udsm pekee.
 
Karne hii bado anawaza umeme wa maji..dah kweli ujinga kitu kibaya sana ..anaenda ku invest hela nyingi hapo hakuna la maana..si walisema gesi inakwenda kumaliza tatizo la umeme au
 
Huo mradi, Tanesco waliuombea 1.2trillion mwanzoni mwa miaka ya 90, serikali ikagoma....ikampa ufadhili IPTL na kutuzalishia umeme wa dharula kwa miaka 20. Hapo ndipo tulipojitabiria kuwa na dharura ya miaka 20 iliyofuata.

Wasiguswe.
 
Karne hii bado anawaza umeme wa maji..dah kweli ujinga kitu kibaya sana ..anaenda ku invest hela nyingi hapo hakuna la maana..si walisema gesi inakwenda kumaliza tatizo la umeme au

Kwan ndo mwsho .nchi c inakua ..unataka kinyerezi ndo iwe mradi wa mwsho
 
Kama sera ya viwanda itatekelezwa ipasavyo, bado umeme wa Stiegler hauwezi kutosheleza mahitaji miaka 10 baada ya kukamilika. Mfano, vikijengwa viwanda vipya vya saruji hata 5, huo umeme unaweza usitoshe. South Africa ina idadi sawa ya watu na sisi, lakini wao wanazalisha umeme ambao ni mara 25 ya ule tunaozalisha na bado wanakuwa na mgao wa umeme.

Kwahiyo programu za REA na Viwanda, zitaumeza huo umeme hata kabla haujakamilishwa.
safari inaanza na hatua mama...Stiegler Gorge halafu inafuata miradi mingine kuna miradi ya umeme wa joto ardhi ipo kwenye michakato pia
 
Karne hii bado anawaza umeme wa maji..dah kweli ujinga kitu kibaya sana ..anaenda ku invest hela nyingi hapo hakuna la maana..si walisema gesi inakwenda kumaliza tatizo la umeme au
Sina hakika kama unafahamu kuwa huo ndo umeme wa bei rahisi zaidi???

Pia unafahamu mataifa kama Japan, Germany n.k wamejipanga kuondokana na nishati ya umeme kwa kutumia nyuklia???

Unafahamu kwanini Zambia na Zimbabwe walikuwa na mgogoro kuhusu Victoria falls, Uingereza alihusika.

Kidatu, Kihansi na Nyumba ya Mungu, kwa pamoja ndio ulikuwa uti wa mgongo hapa TZ unapozungumzia nishati ya Umeme.
 
safari inaanza na hatua mama...Stiegler Gorge halafu inafuata miradi mingine kuna miradi ya umeme wa joto ardhi ipo kwenye michakato pia
Kwa Tanzania yetu, ni kawaida kwa mtu kutoamini michakato. Hata Stiegler ilikuwa kwenye michakato kwa miongo mingi tu. Hata kubinafsishwa kwa sekta ya umeme kupo kwenye mchakato.
 
Nimeanza kumwamini nipo Mwanza kwa siku hizi mbili naona Vic fish anavunja kuta za kiwanda chake kupisha upanuzi wa reli.

Wenyeji wangu wanasema upanuzi huo unaanzia hapo voil hadi maeneo ya Mwanza huduma(makaburi ya wahindi)

Tumpe muda ila atujali na sisi watu wa kada za chini.
 
Back
Top Bottom