Magufuli aufufua mradi utakaoweza kusambaza umeme Afrika Mashariki nzima!

Karne hii bado anawaza umeme wa maji..dah kweli ujinga kitu kibaya sana ..anaenda ku invest hela nyingi hapo hakuna la maana..si walisema gesi inakwenda kumaliza tatizo la umeme au
Mkuu fanya utafiti kidogo tu utapata majibu ya hoja yako.

Hii ni link ya mradi mkubwa wa karibuni tu ambao mataifa yaliyoendelea yamewekeza pesa zao.

Three Gorges Dam - Wikipedia
 
Kama sera ya viwanda itatekelezwa ipasavyo, bado umeme wa Stiegler hauwezi kutosheleza mahitaji miaka 10 baada ya kukamilika. Mfano, vikijengwa viwanda vipya vya saruji hata 5, huo umeme unaweza usitoshe. South Africa ina idadi sawa ya watu na sisi, lakini wao wanazalisha umeme ambao ni mara 25 ya ule tunaozalisha na bado wanakuwa na mgao wa umeme.

Kwahiyo programu za REA na Viwanda, zitaumeza huo umeme hata kabla haujakamilishwa.
Umesahau na smelter ya mchanga wa dhahabu nasikia inakula MW 1000 yenyewe tu. Hapo bado treni la umeme Dar-Moro!
 
Umesahau na smelter ya mchanga wa dhahabu nasikia inakula MW 1000 yenyewe tu. Hapo bado treni la umeme Dar-Moro!
Nani huyo alikudanganya smelter ya dhahabu inakula mw1000? Smeltel ya kiwanda cha cement inakula umeme mwingi kuliko ya dhahabu. Labda kidogo ungesema smelter ya copper. Hiyo ya copper haija fikia ata robo ya mw 1000. Ulikuwa mwenye vijiwe vya kahawa.
 
JK alituambia mradi wa gesi ya Mtwara-Dar ukiisha Tanzania itaanza kusambaza umeme Africa mashariki.

Sijui huu mradi haujaisha au tayari?
 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa mkoa wa pwani kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kwamba miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla inatekelezwa kama alivyoahidi.

Mhe. Rais ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati, ujenzi wa barabara njia sita Dar-Chalinze na ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge) ambao mipango ya ushirikiano katika utekelezaji na Ethiopia imeshaanza.

NOTE: Kwa msiofahamu mradi wa Stiegler's Gorge ni moja ya key priority projects zilizotajwa kwenye East African Power Master Plan. Huu mradi, pamoja na mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, utaiwezesha Tanzania kuwa power house ya Afrika Mashariki, ukizingatia kwamba grid za umeme za mataifa ya Afrika Mashariki sasa zimeunganishwa tayari.
Mradi utazalisha hadi MW 2100 za umeme, ambazo ni zaidi ya umeme wote unaozalishwa hapa Tanzania kwa sasa.

Viva JPM Viva Tanzania na Viva EAC!
Teh teh teh.!
Sasa hivi unampenda Magufuli eeh?
 
JK alituambia mradi wa gesi ya Mtwara-Dar ukiisha Tanzania itaanza kusambaza umeme Africa mashariki.

Sijui huu mradi haujaisha au tayari?
Mbona maswali ya namna hii yanajirudiarudia?
Mnataka mjibiwe Mara ngapi?
 
Karne hii bado anawaza umeme wa maji..dah kweli ujinga kitu kibaya sana ..anaenda ku invest hela nyingi hapo hakuna la maana..si walisema gesi inakwenda kumaliza tatizo la umeme au
Ni kweli ujinga kitu kibaya, na hapa umeonesha ujinga wako
 
Jombaa wato wanaongelea MEGAWATT sio WATT.....


Kaka afadhali usaidie wenye akili ndogo maana MTU kasomea ualimu wa historian nae anataka kuleta challenge ya utalaamu wa sayansi....sasa ona anakurupuka na WATT bila kujua ukubwa wa WATT 2100 ni balbu 20 tuu za aina ya yai za sh mia tano....ukimuuliza ukubwa was megawatt no ngapi jicho linamtoka kama kala pilipili mbuzi,,,nae ana challenge et bado tunazalisha WATT,,,Akili ndogo
 
Back
Top Bottom