Elections 2015 Magufuli atueleze ile M Bank iliyo ndani ya Jengo la Mapato Dar ni ya nani?

Sasa mkuu shaka yangu ni kule kuwemo kwenye jengo la TRA wamepanga?kama wame panga inakuweje ofisi ya serikali tena nyeti kama hiyo ipangishwe?

Kuna tatizo gani kwa hiyo Bank kuwa pale?Mnajua hayo ndo Lowasa anataka kupambana nayo, kuchukia watu kiwivu wivu bila hoja.Wakija UKAWA, ni mabepari pure, hata bandari watauza alımradi kuwepo na ufanisı.
 
Acha Majungu. Kila Bank ilikuwa inaruhusiwa kufanya ili mradi tu iweze ku-automate process ya ulipaji ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato. Hao wengine hawakuweza sasa unataka serikali ifanyeje? Iwafanyie au?
 
Makomeo kaenda pale kulinda mkate wa wakubwa husiguswe,ndio maana unawaona wakubwa wanaporomosha matusi kwa jazba,wanafikiri mtanzania wa sasa anaogopa mkwara wa kiongozi,dawa yao ipo oktoba
 
Sasa mkuu shaka yangu ni kule kuwemo kwenye jengo la TRA wamepanga?kama wame panga inakuweje ofisi ya serikali tena nyeti kama hiyo ipangishwe?
kaka mbona crdb ipo ndan ya jengo la tra pale posta??mbona nmb ipo kwny jengo la tra pale mwenge sasa shaka yako ww ni nn sijakuelewa ni issue ya kibiashara tu!na hyo bank m muhusika mkuu ni nimrod mkono!
 
Hawa ndio Mkapa aliyokuwa amewasema, wanakurupuka tu na kuandika wanachohisi, hawafanyi uhakiki wa wanachokisikia, wana presha, wanataka-kuwa wa kwanza kuchangia mada....kweli mzee mkapa hakukosea.

Mbona mapovu yanakutoka kama mtoto wa ngiri
 
Hii benki mwenyekiti wake ni Nimrod Mkono na pia ni shareholder; lakini la msingi ni kuwa benki hii ilianzishwa kwa pesa yetu iliyoibiwa na wale wezi wa EPA wakina JEETU Patel!!! Mpaka leo hii serikali ya magamba inaogopa kumgusa Jeetu kwani atawaumbua mahakamani na ndio maana kesi zinazomhusu za EPA zimezimwa mapaka DHAIFU atoke madarakani!!

Na ndio maana anakazania waingie madarakani watu ambao atakuwa rahisi kuwa kontrol
 
Kati ya Benki M, NMB na CRDB, ipi tunaweza kusema ni benki ya Watanzania? Ukijua hilo, utapata majibu ya hoja iliyoko jukwaani
 
Kama ana fikiria kwa kuwa karibu na Magufuri na kung'ang'ania kuendelea kuwa mwenyekiti ndio atamcontrol Magufuri ni lazima atakuwa mpumbavu;

Kila mtu anajua kuwa Magufuri hakuwa chaguo lake kama vile yeye hakuwa chaguyo la Mkapa na ndio maana alimdhalilisha sana alipoingia madarakani na yeye vivyo hivyo atarajie kuwa uozo wake na familia yake lazima utaanikwa hadaharani baada ya uchaguzi!
 
Kuna tatizo gani kwa hiyo Bank kuwa pale?Mnajua hayo ndo Lowasa anataka kupambana nayo, kuchukia watu kiwivu wivu bila hoja.Wakija UKAWA, ni mabepari pure, hata bandari watauza alımradi kuwepo na ufanisı.

Imekula kwako,jibu hoja wacha ngonjera
 
Wakuu bado sijapata jibu ninani hasa mmiliki wa bank hii na kwa nini imeruhusiwa kuwa yenye dhamana ya kukusanya mapato ya serikali huku ikiwa ni ya binafsi.Naona kabla hata ya kupata jibu uzi umesha unganishwa tayari huenda hata wenye majibu hawaja pata nafasi ya kutupatia.Naliona ni jambo lenye public interest,kwasababu wananchi wangependa kujua kwanini mapato yao ya ingie mifukoni mwa watu ndipo ya ingie hazina.Bank hii hukusanya chapchap na nyaraka zake hupokelewa chapchap.Ndiyo maana nilidhani Magufuli anaweza kuwa analijua hili kuliko Lowasa aliye ondoka serikalini 2008.Ikoshaka kuwa walio mweka magufuli ni wale wanao jikusanyia mapato ya serikali na kuweka mfukono na kisha kuacha nyaraka zitembezwe kuwa serikali imepata mapato.Tuna elezwe kwa taarifa zisizo rasmi kuwa hiyo M maana yake ni Mkapa bank,na mkapa ndiyo tume mwona anavyo kuwa mkali kwenye kampeni akitukana vile.Kwa nini tusiamini kamweka magufuli kulinda bank ya kukusanya hela za kifisadi?
M Bank unamaanisha Bank M? Kama ndiyo, basi ni ya fisadi Nimrod Mkono! Bank kuwapo ndani ya jengo la TRA hakuna tatizo lolote coz' hiyo ndio maana halisi ya Long Room! Ikiwa Bank M ni mmoja wa mawakala wa TRA katika kukusanya mapato, sasa badala ya kumfanya mteja atoke bandarini hadi somewhere else liliko tawi la Bank M kwa ajili ya kulipa ushuru, basi wanamaliza issue mzima hapo hapo mjengoni! Na kwa ninavyofahamu Bank M ni corporate kwahiyo bila shaka wana wateja wa kutosha wanaofanya biashara na TRA/Bandari! Sasa hapo lengo ni kuondoa usumbufu wa kwenda na kurudi!

The idea is commercial/customer services oriented labda kama tatizo liwe kwenye uendeshaji wake!
 
Huwa tunahitaji uzalendo ila matokeo yake mtanzania akifanya kitu cha kimaendeleo mnasema ni ufisadi ila yule alieenda kuunda mkampuni wake huko na kuweka uongozi wa kizungu na kujifanya wawekezaji na kuchukua tenda na leo ana puyanga barabarani kulaghai alio waibia na kuwasanifu na bado mna mkumbatia alafu una kurupuka kuanzisha uzi wa ki'' lugha ya mkapa '' nyie ndio mkapa alio wasema
 
bank M ni ya advocate Mkono, labda kama ameiuza

Akishirikiana na jamaa aliyetukana juzi pale jangwani na makao makuu yake yapo kule sea view ambapo jamaa cha matusi ameitoa hio nyumba iwe ndio makao makuu ya m bank
 
M Bank unamaanisha Bank M? Kama ndiyo, basi ni ya fisadi Nimrod Mkono! Bank kuwapo ndani ya jengo la TRA hakuna tatizo lolote coz' hiyo ndio maana halisi ya Long Room! Ikiwa Bank M ni mmoja wa mawakala wa TRA katika kukusanya mapato, sasa badala ya kumfanya mteja atoke bandarini hadi somewhere else liliko tawi la Bank M kwa ajili ya kulipa ushuru, basi wanamaliza issue mzima hapo hapo mjengoni! Na kwa ninavyofahamu Bank M ni corporate kwahiyo bila shaka wana wateja wa kutosha wanaofanya biashara na TRA/Bandari! Sasa hapo lengo ni kuondoa usumbufu wa kwenda na kurudi!

The idea is commercial/customer services oriented labda kama tatizo liwe kwenye uendeshaji wake!

Well done! Ila siamini kama mkono ni fisadi kulinga na shughuli zake
 
Dr.Pombe Magufuli ni Waziri wa Ujenzi na bandari haiko chini ya Wizara ya Ujenzi hivyo Dr.Pombe Magufuli hahusiki na chochote kinachoendela bandarini na hana mamlaka (bado mpaka baada ya 25/10) ya kuingilia Wizara nyingine hivyo ningekushauri utafute majibu ktk kwa Wizara husika, si ajabu fisadi Lowasa na Genge lake pia wanaweza kujua sina uhakika lkn jaribu kuwauliza!

Na vipi kuhusu barabara zinazojengwa kuwa upana wa 5.7m-6m badala ya 6.5m tumuulize nani?? Maana lami kwa 0.5M kwa makilometa yoote haya, ni pesa mingiiii!!! Hebu tujuze tumuulize nani??

Cc. Lizaboni
 
Last edited by a moderator:
Well done! Ila siamini kama mkono ni fisadi kulinga na shughuli zake
Katika hali ya kawaida unaweza kumwita sio fisadi kwavile pesa ya Mkono inatokana sana na taaluma yake ya kisheria! Tatizo la wanasheria, ujanja ujanja mwingi mno na hili si kwa Mkono tu bali almost wanasheria wote hususani kama wanafanya kazi na taasisi za serikali (taasisi as a client)! Sasa ukichulia kesi za TANESCO kwa mfano ambazo Mkono alikuwa wakili wao... kesi zingine ukiziangalia vizuri ni kama zilikuwa zinatengenezwa ili watu waendelee kupiga pesa na hili linakuja pale unakuta TANESCO wanafungua kesi, wanashindwa wanakata rufaa wanakula za uso na sehemu zote zote hizo watu wanakula per hour!

Anyway, kama na wewe ni mwanasheria basi am very sorry but I don't trust you guys... ujanja ujanja mwingi mno!
 
Back
Top Bottom