Elections 2015 Magufuli atueleze ile M Bank iliyo ndani ya Jengo la Mapato Dar ni ya nani?

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Kama umewahi kutoa mzigo pale bandarini utakuwa ume ona bank moja iitwayo M bank ambayo hukusanya mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Hiyo bank haina kazi nyingine bali kukusanya kodi.Kwa nini ipo kwenye jengo la mapato ya serikali?.Kwa hakika ni ya mtu binafsi sasa niya nani?

Haiingii akilini kama utaratibu huo hauna harufu ya ufisadi wa kutisha kwa mapato ya serikali.Kama kulikuwa na ulazima wa kurahisisha ulipaji wa kodi si ingekuwa vema wange weka hata bank kama NMB ambayo serikali ina hisa kuliko mazingira hayo ambayo bank hiyo inaweza kukusanya na kufanyia mambo yao kabla ya kuwasilisha hazina?

Na nimetoa mimi mzigo pale,yaani ukilipia kwenye bank hiyo nyaraka zake zimefanywa kuwa na nguvu kuliko bank nyingine ambazo hupelekwa kwanza hazina.Lakini wao ukilipia hakuna nyaraka kusubiri ziende hazina,una chukua mzigo moja kwa moja.Na taarifa nilizo nazo nasikia hiyo 'M' maana yake Mkapa bank.

Sasa kama ni kweli kwanini tusihusishe Mkapa kumtaka Magufuli awe Raisi ili kulinda ufisadi kama huo?.Halafu Mkapa mwenyewe ana kampeni kwa matusi kama kwa kupanic?

Hali hii inatia shaka kubwa juu ya uteuzi wa Magufuli kwamba anakwenda pale kulinda maslahi ya mafisadi.
 
M Bank. Wajuzi tupeni raha kuuhusu hii ili tumchane live bila chenga mwenye matusi yake.
 
Dr.Pombe Magufuli ni Waziri wa Ujenzi na bandari haiko chini ya Wizara ya Ujenzi hivyo Dr.Pombe Magufuli hahusiki na chochote kinachoendela bandarini na hana mamlaka (bado mpaka baada ya 25/10) ya kuingilia Wizara nyingine hivyo ningekushauri utafute majibu ktk kwa Wizara husika, si ajabu fisadi Lowasa na Genge lake pia wanaweza kujua sina uhakika lkn jaribu kuwauliza!
 
Mkapa Bank ... ndo maana anatuita Malofa ... Wapumbavu kwa hela zetu wenyewe ... Ilianzia kwenye Nyumba aliyojigawia pale sea View ...
 
Dr.Pombe Magufuli ni Waziri wa Ujenzi na bandari haiko chini ya Wizara ya Ujenzi hivyo Dr.Pombe Magufuli hahusiki na chochote kinachoendela bandarini na hana mamlaka (bado mpaka baada ya 25/10) ya kuingilia Wizara nyingine hivyo ningekushauri utafute majibu ktk kwa Wizara husika, si ajabu fisadi Lowasa na Genge lake pia wanaweza kujua sina uhakika lkn jaribu kuwauliza!
Ni vigumu kumwuliza Lowasa kwa sababu aliondolewa serikalini 2008,na Magufuli mpaka juzi alikuwa serikalini.Kumbuka kuna ile collective responsibility,kwa hiyo Magufuli yumo katika baraza la mawaziri haiwezekani akawa hajui
 
Wakuu bado sijapata jibu ninani hasa mmiliki wa bank hii na kwa nini imeruhusiwa kuwa yenye dhamana ya kukusanya mapato ya serikali huku ikiwa ni ya binafsi.

Naona kabla hata ya kupata jibu uzi umesha unganishwa tayari huenda hata wenye majibu hawaja pata nafasi ya kutupatia.

Naliona ni jambo lenye public interest,kwasababu wananchi wangependa kujua kwanini mapato yao ya ingie mifukoni mwa watu ndipo ya ingie hazina.Bank hii hukusanya chapchap na nyaraka zake hupokelewa chapchap.

Ndiyo maana nilidhani Magufuli anaweza kuwa analijua hili kuliko Lowasa aliye ondoka serikalini 2008.Ikoshaka kuwa walio mweka magufuli ni wale wanao jikusanyia mapato ya serikali na kuweka mfukono na kisha kuacha nyaraka zitembezwe kuwa serikali imepata mapato.

Tuna elezwe kwa taarifa zisizo rasmi kuwa hiyo M maana yake ni Mkapa bank,na mkapa ndiyo tume mwona anavyo kuwa mkali kwenye kampeni akitukana vile. Kwa nini tusiamini kamweka magufuli kulinda bank ya kukusanya hela za kifisadi?
 
bank M ni ya advocate Mkono, labda kama ameiuza

Hii benki mwenyekiti wake ni Nimrod Mkono na pia ni shareholder; lakini la msingi ni kuwa benki hii ilianzishwa kwa pesa yetu iliyoibiwa na wale wezi wa EPA wakina JEETU Patel!!! Mpaka leo hii serikali ya magamba inaogopa kumgusa Jeetu kwani atawaumbua mahakamani na ndio maana kesi zinazomhusu za EPA zimezimwa mapaka DHAIFU atoke madarakani!!
 
Bank nyingi tuu tofauti na Bank M zinakusanya kodi for TRA, kama exim, Fbme,Fnb, Boa, Uba.etc so mkuu usiwe na wasiwasi.
Sasa mkuu shaka yangu ni kule kuwemo kwenye jengo la TRA wamepanga?kama wame panga inakuweje ofisi ya serikali tena nyeti kama hiyo ipangishwe?
 
Hawa ndio Mkapa aliyokuwa amewasema, wanakurupuka tu na kuandika wanachohisi, hawafanyi uhakiki wa wanachokisikia, wana presha, wanataka-kuwa wa kwanza kuchangia mada....kweli mzee mkapa hakukosea.
 
Back
Top Bottom