Uchaguzi 2020 Magufuli ataweza himili joto hili hapo Oktoba?

Siku hizi sichangii kabisa siasa, lakini naomba nikuulize: Hivi umekutwa na nini ???
Kile kiburi, kashfa na kejeli ulizokuwa unawatolea watu hapa kisa mahaba na Raisi viko wapi ?
 
Siku hizi sichangii kabisa siasa, lakini naomba nikuulize: Hivi umekutwa na nini ???
Kile kiburi, kashfa na kejeli ulizokuwa unawatolea watu hapa kisa mahaba na Raisi viko wapi ?
Safari huanza na wengi, lakini mwisho hufika na wachache!
 
Safari huanza na wengi, lakini mwisho hufika na wachache!
Hawa ndugu zangu akiwemo huyu jamaa macho_mdiliko walishawahi kunitukana sana na kunishambulia hapa jukwaani nilivyokuwa naongea kuhusu Raisi Magufuli. Walinitolea kashfa sana hadi kuniita mimi Tarumbeta ya Fisadi Membe. Ndugu yangu Chige ni shahidi jinsi huyu jamaa alivyokuwa anatoa kashfa kwa watu ili kumtetea Raisi Magufuli: Lakini nafurahi kuona akili na utu vimeanza kumrudia. Natumai wengi tu wataiga mfano wake,.........

Siku hizi huwa sizingumzi kabisa siasa hadharani na watu, lakini huyu jamaa amenifanya nifikirie mengi na kuwaonea huruma wengine walio kama yeye. Nchi yetu sote hii unapoona binadamu mwenzako anadhalilishwa na kuonewa usifurahie hata siku moja.
 
Si peke yake... Magufuli amekatisha tamaa watu wengi sana!
 
Zama za Lowassa si hizi!! Kama Lowassa aliyekua hawezi ongea zaidi ya dakika 5 alipata Kura million 6 vipi Membe?
Bro acha kujifariji 2015 Lowasa umarufu wake ndo ulipata hizo kura milioni 6. Membe hawezi mfikia Lowasa. Na kwataarifa yako 2015 Membe ndo angelikuwa anagombea CCM then Chadema Lowassa. Mapema sana Lowasa angelichukua Nchi.
 
Sioni uchaguzi kuwa mgumu mwaka huu watanzania wachache humu jf nadhan wengi wenu hampo kwa masilahi ya taifa.mnasinizia kuminywa dsmocrasia hiyo democrasia ni adui wa maendeleo ya africa.angalia mataifa yanayoenda kasi kimaendeleo singapole ,indonesia,vietnam na china it is too wrong kwa nchi changa kimaendeleo kama tz kulilia democrasia wakati rais anakimbia kwa speed ya jet.kama kuna ufisad kwenye ndege acha uwepo maana miaka yote ishirin tumekodi ndege kwa gharama kubwa

Sent from my SM-T355Y using JamiiForums mobile app
 
Uzi wa washabiki wa lisu na chadema kujifariji!
Kipigo hakikwepeki!

Hivi Membe atakuja na hoja ipi mpya?
Nyarandu nae atakuja na hoja ipi mpya?

Hahhha.. Mambo mengine ni kichekeshana tu jamani.
 
Ni moja ya chaguzi nyepesi kbs za nchi...matunda ya kazi yake yameonekana kwenye jamii..labda uchaguzi wa jamii forum
 
Uzi wa washabiki wa lisu na chadema kujifariji!
Kipigo hakikwepeki!

Hivi Membe atakuja na hoja ipi mpya?
Nyarandu nae atakuja na hoja ipi mpya?

Hahhha.. Mambo mengine ni kichekeshana tu jamani.
Wewe mla dagaa kauzu huna jipya!!

Zaidi ya Stigla na SGR bwana wenu ana jipya gani?
 
We ndo utajitoa hiyo blood sacrifice au unaongea tu, unaifahamu blood shed lakini!?, au kazi kupotosha umma tu.
Kipindi Zanzibar imezalisha wakimbizi ulikuwa hujazaliwa bila shaka, kama huna taarifa basi elewa kwamba wakati Mkapa anagombea kwa awamu ya pili kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu yaliyopelekea mauaji ya watu kadhaa bara na visiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…