Magufuli atashindwa kama Nyerere

Magufuli atashindwa kama Nyerere

nyerere alikua sahihi kabisa, ila kwa bahati mbaya sana watanzania hatukumuelewa, kama tungemuelewa si ajabu na sisi tungekua na maendeleo kama china au japan,

Hatujaendela sana kwa sababu Watanzania wengi ni SIMPLE minded. .

Hawawezi kufikiri mambo makubwa hiyo ndiyo shida. ..wengi wanapenda udaku na porojo.

Ukitaka kuthibitisha hilo .Hata mkikaa bar 90% ya mazungumzo mpira wa ulaya... unafikiri baada ya hapo tunapata nini. Mara chache siasa

Nyerer was ahead of time. ...sasa JPM naye ana maono kama ya mzee nyerer ...tunatumain anaweza kutusogeza
 
Hapo hauko sawa.

Misingi mibovu ya zamani imeshabomolewa na Kikwete kisha jenga mipya, sasa Magufuli anajenga nyumba tu. Misingi imara na thabiti imeshawekwa ndiyo maana unaona watu kama Mramba na Yona wananyea debe. Unaona watu kama Lowassa wakitemwa na CCM na unaona watu kama Kingunge na Sumaye wakiingia mitini wenyewe.
Dada Faiza, ikiwa Kikwete alibomoa misingi mibovu ya zamani, haya majipu anayotumbua Mugufuli ya TRA, Bandari na kwengineko yalitunza usaha wakati wa rais gani - Nyerere, Mwinyi, Mkapa? Ninabaki na dhana kwamba nchi imefisidiwa kwa miaka mingi, kuijenga upya kunataka moyo wa ujasiri na mashirikiano ya kila mmoja wetu. Ninachosisitiza ni kuwa tumsaidie Magufuli, tusitafute wachawi, wapo wengi.
 
Kuna kitu nyuma ya pazia kuhusu uwekezaji Oysterbay. Tukumbuke wakati wa Mwinyi kuna kibali kilitolewa kujenga Hotel upande wa bahari wa barabara ukapigiwa kelele na ikapigwa marufuku uendelezwaji (Binafsi?) wa upande wa pili wa barabara. Je marufuku hiyo ilifutwa? Pili katika tembea yangu kwenye fukwe za nchi nyingine upande unaogusa bahari ukiendelezwa huwa ni kwa faida ya umma, na sio private beach, ikiwa kwamba hazuiliwi mtu kutembea sehemu hiyo e.g Sceveninem den Hague, OOstende, Hamburg, Seine Paris na kwingingineko. Wawekezaji hupata faida kwa migahawa inayokuwepo sehemu hiyo. Kama mkataba huo utazingatia hayo kwa uwazi hauna ubaya vinginevyo nini kelele?
 
Ninachoamini mimi, uwekezaji wa ovyo , yani uliopatikana kwa kupindisha mambo flaniflani ya kisheria ni kwa faida ya wachache tu na hayatakua na tija kwa mtanzania wa kawaida hata kidogo, Tusidanganyane hapa. Hawa jamaa wanaotaka kupata kinyemela hawana mpango na Watanzania wengi ambao maisha yao ni yakawaida sana. Akipata tu ndo utaona tofauti ya kujichanganya na kutengwa kati ya cc wenyewe.
 
Yaani ndio naona uwezo wa mungu ulivyo tuumba tofauti kweli kifikra yaani kuna watu hawaoni hata chembe Juhudi za kulikomboa hili taifa nakutafuta vitu vidogo vidogo nakuponda, nakumuombea kufeli Khaa tunakaazi kweli. Kwa kweli mimi binafsi kwa uthubutu aliouenyesha namuombea kwa mungu ampe afya njema tuzidi kuona mengi.
 
Waliozowea vya kunyonga watamchukia Magufuli kama wanavyomchukia Nyerere sababu ya majipu waliyo nayo.
 
Dada Faiza, ikiwa Kikwete alibomoa misingi mibovu ya zamani, haya majipu anayotumbua Mugufuli ya TRA, Bandari na kwengineko yalitunza usaha wakati wa rais gani - Nyerere, Mwinyi, Mkapa? Ninabaki na dhana kwamba nchi imefisidiwa kwa miaka mingi, kuijenga upya kunataka moyo wa ujasiri na mashirikiano ya kila mmoja wetu. Ninachosisitiza ni kuwa tumsaidie Magufuli, tusitafute wachawi, wapo wengi.

Hapo ndipo unaposhindwa kuelewa kuwa Magufuli alikabidhiwa ofisi na vitu pending vya kufanyiwa kazi haraka.

Majipu ya TRA yalikuwa yanangoja uchaguzi tu uishe na hayakutaka yatumbuliwe mwaka wa uchaguzi. Kumbuka hilo.
 
NYERERE ALIFELI VIBAYA SANA ECONOMICALLY INGAWA ALIFANIKIWA SOCIALLY.
MAREKANI NA WESTERN HUAMINI UKITAKA KUMTAWALA MTU MKONTROL ECONOMICALLY.

Sasa Nyerere alidai hataki wawekezaji kwa rasilimali zetu mpaka tupate uwezo wetu wenyewe. Tungekaa kusikiliza mawazo hayo tungekaa miaka 1000 labda ndio technology tungekuwa tumeipata pamoja na fedha.

Hivyo 1992 iliamliwa kuruhusu uwekezaji katika madini, gesi,elimu,afya,umeme,usafirishaji,viwanda,mawasiliano nk sasa hivi kila MTU ana simu,TV vitu vidogo unavovisense mahali ulipo. Je, kusingekuwa na uwekezaji what do u think?

Magufuli nae anataka kumzuia Manji asiwekeze Coco Beach eti watu wa Mazenze wataogelea wapi? Uwekezaji huo ulikuwa haubadilishi matumizi ya public Bali kuboresha mazingira na yawe ya kuvutia.

Issue sio kuzuia uwekezaji bali mkataba na sheria nzuri za uwekezaji. Leo Meck Sadick nae kaogopa anamuomba Manji aache uwekezaji pale Coco Beach.

Hizi Sera za Nyerere si zilijifia kitambo kuzifufua na kujisumbua tu.

Argue,don't shout!

Ukiona ugomvi wa watoto mpaka baba ameingilia kati ujue kuna mmoja wao amecheza faulo (faul)..

Uwekezaji wa fukwe za bahari umefanywa sehemu nyingi..Kuna Berinda beach resort, Girrafe,Silver Sands na nyingine nyingi..Sasa kwanini hujiulizi Raisi kutolea macho Coco Beach tu na sio hizo nyingine? Unahisi amekurupuka? unahisi hakushauriwa vizuri na timu yake? Unahic wewe unajua vizuri Nature na kilichomo ndani ya mkataba wa uwekezaji wa Manji kuliko Raisi na Usalama wa Taifa..I do smell Something fishy, Don't U ?!
 
NYERERE ALIFELI VIBAYA SANA ECONOMICALLY INGAWA ALIFANIKIWA SOCIALLY.
MAREKANI NA WESTERN HUAMINI UKITAKA KUMTAWALA MTU MKONTROL ECONOMICALLY.

Sasa Nyerere alidai hataki wawekezaji kwa rasilimali zetu mpaka tupate uwezo wetu wenyewe. Tungekaa kusikiliza mawazo hayo tungekaa miaka 1000 labda ndio technology tungekuwa tumeipata pamoja na fedha.

Hivyo 1992 iliamliwa kuruhusu uwekezaji katika madini, gesi,elimu,afya,umeme,usafirishaji,viwanda,mawasiliano nk sasa hivi kila MTU ana simu,TV vitu vidogo unavovisense mahali ulipo. Je, kusingekuwa na uwekezaji what do u think?

Magufuli nae anataka kumzuia Manji asiwekeze Coco Beach eti watu wa Mazenze wataogelea wapi? Uwekezaji huo ulikuwa haubadilishi matumizi ya public Bali kuboresha mazingira na yawe ya kuvutia.

Issue sio kuzuia uwekezaji bali mkataba na sheria nzuri za uwekezaji. Leo Meck Sadick nae kaogopa anamuomba Manji aache uwekezaji pale Coco Beach.

Hizi Sera za Nyerere si zilijifia kitambo kuzifufua na kujisumbua tu.

Argue,don't shout!

Wewe umefanikiwa kiasi gani kuendesha familia yako (kama unayo)? Jee, kama unayo familia, kila mwanafamilia unampatia mahitaji yote ya ndoto zake? Kama umeshindwa na kama huna mfano wa mwenye familia aliyeweza kukamilisha ndoto zote za wanafamilia wake, kwanini unategemea Dk. Magufuli akidhi shida za watanzania zaidi ya milioni 40 ambao miongoni mwao ni wakwepa kodi kama wewe?
 
jamani hivi pale coco kuna nini kigumu cha kuwekeza.
kama ni vyoo hivi manispaa haiwezi kujenga vyoo vya kutosha pale.
kama ni ukuta manispaa haiwezi kufanya hilo.
kama ni sehem za kubadilishia nguo waogeleaji manispaa haiwezi kufanya hayo.
mpk mtu mmoja aingie mkataba wa kumiliki coco yote nakujenga mambo hayo manispaa iko wapi.
mi nadhani magu anaweza akaanzia na hao wa manispaa kama wanashindwa kujenga hivyo vitu vidogo tu basi hawafanyi kazi waondolewe tu maana hamna namna nyingine.
 
Hapo ndipo unaposhindwa kuelewa kuwa Magufuli alikabidhiwa ofisi na vitu pending vya kufanyiwa kazi haraka.
Majipu ya TRA yalikuwa yanangoja uchaguzi tu uishe na hayakutaka yatumbuliwe mwaka wa uchaguzi. Kumbuka hilo.
Dada FaizaFoxy, nimekufahamu lakini haiingii akilini - Sherehe za Kitaifa na safari za nje, bila kutaja hayo ya TRA na TPAambazo zilikuwa zinatafuna mabilioni ya fedha ya walipa kodi huku walipa kodi wenyewe hawana shule, hawana vikalio, hawana walimu kwa ajili ya watoto wao; mahospitalini mashine zimesimama, wagonjwa wanarundikana chini, hakuna madawa wala vifaa tiba. Hii ni kusema tangu alipotuondokea Mwalimu Nyerere, tunawacha mambo pending mpaka aje anayefanana na Nyerere.
Msisitizo, Magufuli tushirikianae naye, asihujumiwe kusijekuwa na pendings nyengine.
 
Last edited by a moderator:

Hilo la hawana shule, si kweli.

Sasa hivi shule za msingi na sekondari kila kata, ahsante Kikwete.

Kuhusu yanayofanyika TRA na kwingineko sasa hivi nnakusihi rejea ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo Magufuli aliikuwa akiinadi wakati wa kugombea Urais, labda ukisha isoma na kuona kazi zilizokusudiwa kufanywa na CCM utanielewa.
 
Back
Top Bottom