Magufuli atashindwa kama Nyerere

Magufuli atashindwa kama Nyerere

Yes mikaeni upo sawa kabisa kwani kuna sehemu zinapaswa kuwa maeneo ya jumuiya sio binafsi zaidi.. magufuli noma
 
assad siku hizi umepatwa na nini? ulikuwa mfuasi mzuri wa ccm na magufuli wake... leo vipi ndugu!!
 
Acheni hayo yenu nchi itakwenda kama malaysia chini ya uongozi wa mh.magufuli tunamuombea.tembea nchi zote wananchi wa nchi hizo ndiyo wenye kushika uchumi wa nchi hata kama kunaubia tufike huko tusiache yote wageni ndiyo wenye "say'.enough is enough nimnukuu mh.raisi alipowatubia wafanyabiashara ikulu
 
Mkuu swala la beach huwezi kulilinganisha na mambo ya Nyerere miaka ya nyuma, Sio kila kitu utawapa investors kwa sababu tu wanataka, sehemu nyingine utaziacha public tu, sasa ku~privatize sehemu za free kama hizo mwisho wa siku utaenda utaambiwa ulipe mshiko wa juu kuwepo tu pale sijui utajisikiaje.

Na Magufuli alichoongea kua sometimes waangalie kuboresha na sehemu za nje ya miji kidogo, it was a good move, makampuni makubwa sana yakisema yanaanzishwa out of the city maana yake sio tu ongezeko la ajira ila social services zinasambaa kwa sababu kuna pesa kule pataanza kuangaliwa, jiji linazidi kupanuka vizuri bila kuleta inconveniences zozote kwa public.

Magufuli akifeli sitomlaumu, ni kazi kubwa sana kufix whats already broken, mimi nitawalaumu watanzania kwa kua hawako supportive kabisa. Kazi ya kujenga taifa sio ya Rais, Waziri mkuu na specie chache za bungeni peke yake, ni kazi ya kila mtu.

Swala ni mnyama. Pengine unamananisha suala
 
kwaio uwekezaji wa manji cocobeach ni wa hovyo?

Unalipuka tu! Toa mfano mzuri uwekezaji unaonna na huo katika Africa uliofanikiwa bila kuwabagua wenye nacho na wasio nacho! Kwenye hili hutaungwa mkono ng'o!!!
 
acha kujicontadict, kwanini azuie uwekezaji cocobeach?

Kutoa nafasi ya watu mbalimbali kupatumia bila masharti au gharama. ASSARDSyria: Magufuli yupo kwenye game acha kuandaa mapambano dhidi yake yenye chuki binafsi. Baba yenu hakufanya vizuri.
 
nyerere alikua sahihi kabisa, ila kwa bahati mbaya sana watanzania hatukumuelewa, kama tungemuelewa si ajabu na sisi tungekua na maendeleo kama china au japan,
 
kwa hiyo akishaboresha watu watakuwa wanaogelea bure kama sasa?jibu kwanza

Hakuna kabaila yoyote anayewekeza mahali kwa kisingizio cha kuwasaidia wanyonge. Anaweza kuwahadaa anataka kukusaidieni lakini longterm plans zake ni maslahi yake.
 
NYERERE ALIFELI VIBAYA SANA ECONOMICALLY INGAWA ALIFANIKIWA SOCIALLY.
MAREKANI NA WESTERN HUAMINI UKITAKA KUMTAWALA MTU MKONTROL ECONOMICALLY.

Magufuli nae anataka kumzuia Manji asiwekeze Coco Beach eti watu wa Mazenze wataogelea wapi? Uwekezaji huo ulikuwa haubadilishi matumizi ya public Bali kuboresha mazingira na yawe ya kuvutia.

Issue sio kuzuia uwekezaji bali mkataba na sheria nzuri za uwekezaji. Leo Meck Sadick nae kaogopa anamuomba Manji aache uwekezaji pale Coco Beach.

Hizi Sera za Nyerere si zilijifia kitambo kuzifufua na kujisumbua tu.

Argue,don't shout!


Naona taratibu Lumumba wanasoma namba! Vipi tena hii si ndiyo jembe mlilotuaminisha itawakomesha mafisadi?
Hofu yenu nini-Manji kasaambiwa Bongo hii kuna fukwer kibao zilizowazi kwanini anga'anie Coco Beach!

Eti itakuwa bado ni kwa matumizi ya Public-kichekesho gani hiyo-vipi Serena siyo public place ? Je ni waswahili wangapi wanakwenda Serena kama siyo Mafisadi na wale wananyakazi wa sijui TRA,TPA,BOT etc-sehemu wanakouza bia tu kwa zaidi ya 5000ts?.

Bila kupapasa macho Raisi aamuru mara moja Coco Beach kubakia chini ya Manispaa ya Kinondoni ,na serikali kupitia Wizara ya Utalii iwekeze huko wakishirikiana na Manispaa -kwa kuhakikisha Beach ina miundo binu muhimu-na kuwakodishia wafanyabiashara wadogo wadogo watakao uza biadha kwa bei ya uswahilini.

Hata hivyo waweke viingilio vya bei ya chini!.

Kuwe na maeneo ya huduma /starehe;
-Ukumbi wa Musiki
-Sehemu za Vyakula
-sehemu ya Michezo -wakubwa na watoto
-Sehemu ya kupungia upepeo e.tc


 
Kama huu upuuzi wa kuivuruga sector binafsi utaendelea,hafiki popote.Kaanza na Elimu then atahamia kwenye Afya baadaye biashara,uchumi banks kwamba zote ziwe state owned.Binadamu hajawahi kuwa sawa na haitakaa itokee labda mbele ya samaki.Leo hii hotuba zote za Nyerere zinazohubiri ujamaa zimesha-expire huyu naye anataka kutupeleka huko.Bila sector binafsi imara ni ndoto kwa hii serikali kufika popote.BTW:Ngoja suala la ufukwe wa Coco nisiligusie kwanza maanake sielewi hata Manji kalitwaaje sababu matangazo ya Tv wanadai kuwa litaendelezwa na Halmashauri ya Kinondoni kwa ufadhili/ushirika wa TIB.
 
Kwa taatifa yako ni kwamba mannji alitaka kuweka uzio na ili kuingia ilikuwa ni kiingilio
 
Manji ni mshenzi na ana tamaa ya kupindukia, raisi kishamwambia kuna maeneo mengine mengi yana fukwe nzuri zinaziweza kuendelezwa kupunguza congestion ya watu kwanini apang'ang'anie coco? Hii biashara ya the tich get richer the poor get poorer lazima iishe nchi hii majambazi kama manji inabidi wazuiwe pesa wanayoitengeneza ni nyingi mno ataendelea kununua vipande vya nchi mpaka wamiliki nchi nzima huyu mtu ni cancer na inabidi itolewe mapema!! Nashukuru sana meya wa jiji tutampata kutoka upinzani maana hili jitu lingetumaliza.
 
JPM nenda!,nenda!,nenda! Mkombozi!,heshima ya nchi ni uchumi mzuri..!,Shkamoo ni makelele tu!.
 
Ninachoweza kusema ni kwamba kuiongoza TZ ni kazi kubwa sana. Ni nchi ambayo imekuwa ikihujumiwa kiuchumia muda wote tangu uhuru hadi leo, miaka 54 baadaye. Kwa hivyo si rahisi kuijenga kwa kipindi kifupi. Magufuli anajaribu kuweka msingi mpya - ikiwa hatahujumiwa na matajiri na CCM wenzake, na kama wananchi tutamsaidia, kila mmoja alipo kwa nafasi yake - atafanikiwa, tutafanikiwa.
Mungu Ibariki Tanzania

Hapo hauko sawa.

Misingi mibovu ya zamani imeshabomolewa na Kikwete kisha jenga mipya, sasa Magufuli anajenga nyumba tu. Misingi imara na thabiti imeshawekwa ndiyo maana unaona watu kama Mramba na Yona wananyea debe. Unaona watu kama Lowassa wakitemwa na CCM na unaona watu kama Kingunge na Sumaye wakiingia mitini wenyewe.
 
Back
Top Bottom