Elections 2015 Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki

kipasola

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
538
500
ivi iyo mikutano au matashama ya bongo flv? Ili ujue kama chaguo la watu kama rais Lowasa, Mwambie afanye mkutano bila bongoflv alafu asibebe watu kwa Magar kama mfanyavyo kama mtapata mtu hata mmoja
Hawa jamaa ruksa kwa wao kubebaa watu kwenye magari
 
Attachments

Jigsaw

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
1,826
1,250
Jonson Mwambo

NIANZE kwa kuwaomba radhi wasomaji wangu kwamba sitaonekana tena katika safu hii kuanzia toleo lijalo hadi mwanzoni mwa Desemba mwaka huu.

Sababu yenyewe ni kwamba narejea kijijini kwangu wiki hii kwa ajili ya shughuli zangu za kilimo. Msimu wa kilimo utakapomalizika nitarejea tena Dar kuendelea na shughuli za uandishi wa habari.

Nimeona niyaweke wazi hayo kwa sababu kutoweka kwangu ghafla kwenye safu hii (bila maelezo) kunaweza kutafsiriwa vibaya mitandaoni. Uongo unaweza kutembezwa mitandaoni kwamba nimehongwa fedha ili nisiendelee kuandika kwenye safu hii hadi uchaguzi mkuu umalizike.

Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikiitumia safu hii kuweka msimamo wangu bila kificho kuhusu mgombea urais John Magufuli ambaye, kwa mtazamo wangu, naamini ndiye anayeweza kuaminika kukabidhiwa dhamana ya kuiendesha nchi yetu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Walio nje ya taaluma hii ya uandishi wa habari pengine walishangaa kuona mwandishi wa safu (Mbwambo) anamuunga mkono moja kwa moja mgombea urais wa CCM na kumkosoa wa Chadema. Hiyo ilikuwa tu katika kutekeleza wajibu wangu – yaani kuchangia katika juhudi za kuepusha nchi yetu isitawaliwe na mtu mwenye tuhuma za miaka mingi za ufisadi.

Napenda kuitumia fursa hii kuwafahamisha wasomaji wangu ya kwamba mwandishi wa safu kumuunga mkono mgombea fulani wa urais ni jambo la kawaida kabisa duniani katika taaluma hii. Wanafanya hivyo kule Uingereza, wanafanya hivyo kule Marekani, na hata hapa Afrika ni hivyo hivyo.

Gazeti au mwanasafu wa gazeti anaruhusiwa kabisa kuunga mkono mgombea fulani wa urais (endorse a candidate) ili mradi tu afanye hivyo wazi bila kificho, na wasomaji waelewe msimamo wa huyo mwanasafu au hilo gazeti tangu mwanzo kabisa.

Kwa mantiki hiyo, napenda pia nifafanue kwamba bodi ya wahariri ya gazeti la Raia Mwema haikupewa maagizo yoyote na wamiliki wa gazeti hili ya kumuunga mkono mgombea yeyote wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Na badala yake wahariri wetu wamepewa maelekezo ya kuwatendea haki wagombea wote kwa kuzingatia zile kanuni kuu za habari zinazofuatwa kote duniani.

Kwa ufupi, Raia Mwema halina rasmi mgombea urais wake – yaani haliku-endorse yeyote - awe Magufuli, Lowassa, Mama Anna Mghwira nk. Hata hivyo, kwa wanasafu wanaoandika maoni binafsi wa Raia Mwema, wao wana uhuru huo wa ku-endorse mgombea urais wanayemtaka. Na kama nilivyoeleza, hicho ni kitu cha kawaida kabisa katika tasnia yetu duniani.

Ni kwa sababu hiyo nimekuwa nikiitumia safu yangu hii ya Tafakuri Jadidi kuwaeleza Watanzania maoni yangu binafsi kwamba Edward Lowassa hafai kuwa rais wetu mpya kwa sababu, licha ya kuandamwa na kashfa za ufisadi kwa miaka 20, hana jipya ambalo hakuweza kulitenda katika miaka yake zaidi ya 20 ya uongozi serikalini.

Wakati huo ndio msimamo wangu binafsi, wanasafu wenzangu wengine nao wamekuwa wakitumia safu zao kwenye gazeti hili hili kuwahamasisha Watanzania wamkatae Magufuli na CCM yake na wamchague Lowassa. Narudia tena; yote hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika uendeshaji wa magazeti duniani.

Baada ya ufafanuzi huo, niseme kwamba ninaondoka Dar es Salaam kurudi kijijini nikiwa na imani kuwa mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli ataibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Nisichokuwa na uhakika nacho ni ushindi wake utakuwa ni wa asilimia ngapi.

Matokeo ya utafiti wa hivi karibuni wa asasi za TWAWEZA na IPSOS (SYNOVATE) yanaweza yasiwe na usahihi wa asilimia 100, lakini ukweli ni kwamba yanaakisi ukweli wa mambo ulivyo na utakavyokuwa Oktoba 25.

Sina lengo la kurudia hoja nilizokuwa nikizitoa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika safu hii zinazonifanya niamini kuwa Magufuli atambwaga Lowassa katika

Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Itakuwa ni kuwachosha tu bure kurudia hoja hizo.

Hata hivyo, jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba CCM kimejiandaa mapema kwa uchaguzi huu kuliko Chadema, na kinaendesha kampeni zake kisayansi; ilhali Chadema ni mbwembwe na usanii tu.

Hata uamuzi wa Chadema wa hivi karibuni wa kuongeza angani idadi ya helkopta za kampeni ni sehemu tu ya hizo mbwembwe. Kuna wakati kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kiliwahi kutumia helkopta tatu lakini kikaambulia ushindi kwenye kata tatu tu!

Vyovyote vile, ubashiri wangu ni kwamba Magufuli atashinda. Ubashiri wangu mwingine ni kwamba kuhamia kwa Lowassa katika Chadema na kampeni ya urais aliyoifanya hakutaleta mabadiliko makubwa kwa chama hicho kwa maana ya kuongeza viti vya ubunge.

Kwa hiyo, kwa upande wa Chadema, ujio wa Lowassa utakuwa umekidhoofisha tu chama hicho kiutendaji kiuliko kilivyokuwa huko nyuma. Baada ya Oktoba 25, hali ya Chadema itakuwa mbaya, na kama nilivyopata kusema awali, sitashangaa ACT Wazalendo kikiziba baadaye pengo la Chadema kama chama kikuu cha upinzani nchini. Ni suala la muda tu hilo kutokea.

Na hili linanikumbusha maneno ambayo (sina hakika na ukweli wake) niliyoambiwa hivi karibuni na swahiba mmoja wa karibu wa Lowassa kwamba mheshimiwa huyo alipoamua kujiunga na Chadema ili agombee urais alijua fika kwamba hatashinda urais huo kupitia chama hicho!

Kwa mujibu wa maelezo yake aliyodai kaambiwa na Lowassa mwenyewe, swahiba huyo anasema Lowassa aliamua kugombea urais kupitia Chadema ili ‘kukiadhibu' chama hicho kwa kumchafua kwa zaidi ya miaka tisa kuwa ni fisadi mkubwa.

Lakini pia aliamua kugombea urais kupitia chama hicho ili kupata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa Rais Kikwete ambaye aliweka kando uswahiba wao na kumtosa wakati ule alipoandamwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond kiasi cha kumlazimisha kujiuzulu uwaziri mkuu.

Swahiba huyo wa Lowassa aliniambia ya kwamba ‘adhabu' ya kwanza kwa Chadema ni huo mparaganyo uliosababisha Katibu Mkuu wa chama hicho aliyeshiriki sana kukijenga, Dk. Slaa kujiuzulu nafasi yake. Si siri kwamba mpaka sasa Chadema kinapwaya kwa kumkosa mtu wa sampuli ya Dk. Slaa kukaimu nafasi hiyo.

Adhabu ya pili au tuseme pigo la pili la Lowassa kwa Chadema ni hilo la ‘kuwalazimisha' kina Mbowe na Lissu ambao walikuwa vinara wa kumwita fisadi, kuyameza matapishi yao wenyewe kwa kumsafisha wakati wa kampeni za urais kuwa si fisadi.

Kwa mujibu wa swahiba huyo wa Lowassa, hakuna jambo linalomfurahisha mgombea urais huyo wa Chadema hivi sasa zaidi ya kuwaona Lissu na Mbowe wakihaha jukwaani kujaribu kuuaminisha umma kuwa walikosea kumwita Lowassa fisadi.

Yaani anafurahi kuwaona wakimeza matapishi yao wenyewe!

Kwa mtazamo wake, hiyo ni adhabu kubwa kwa kina Mbowe na Lissu kwa sababu heshima yao, weledi wao, uungwana wao, uadilifu wao na uaminifu wao kwa wanachama wa Chadema sasa uko shakani kwa sababu ya ‘kumeza' matapishi yao hayo.

Kwa maana hiyo, Lowassa anajiona ‘kalipiza kisasi' kwa vinara hao wa Chadema waliomwita fisadi, na kwa Chadema yenyewe ambayo anaamini itasambaratika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25!

Kuhusu kulipiza kisasi kwa Kikwete, swahiba wake huyo alinieleza ya kuwa kwa
kugombea urais kupitia Chadema, Lowassa amepata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa kumpaka matope Kikwete wakati wa kampeni kuwa utawala wake wa miaka 10 ulikuwa hovyo kabisa, na kwamba ndiye aliyemlazimisha kuutia saini mkataba wa kifisadi wa Richmond. Fursa hiyo asingeipata kwa kiwango anachopata hivi sasa wakati wa kampeni za urais.

Kama hayo aliyonieleza swahiba huyo wa Lowassa ni ya kweli, basi inamaanisha kuwa tangu mwanzo Lowassa alijua ya kuwa hatashinda urais kupitia Chadema, na alichokifanya, hivyo basi, ni kutafuta tu fursa ya kulipiza visasi kwa Chadema na Kikwete.

Bila shaka anafanya hivyo kwa sababu hana cha kupoteza. Sitashangaa baada ya Oktoba 25 akajirudia Monduli kustaafu kabisa mambo ya siasa; maana atakuwa amemaliza ‘kuwashughulikia' waliomwita fisadi kwa miaka tisa.

Kwa hiyo, imani yangu ya tangu mwanzo kabisa kwamba Lowassa hana na hatakuwa na faida yoyote kubwa kwa Chadema baada ya Oktoba 25 imeimarishwa na kauli hiyo ya swahiba wake huyo.

Tukirejea kwa CCM, ni kweli kuwa Magufuli atashinda lakini mambo hayawezi kubakia vilevile katika chama hicho na katika uendeshaji wa serikali yake. Kwa maneno mengine, mageuzi hayataepukika baada ya Oktoba 25 labda kama CCM kinataka kuishia vilikoishia KANU cha Kenya na ZANU cha Zambia.

Kwa maneno mengine, kampeni zilizoendeshwa na zinazoendeshwa na Lowassa na Chadema yake, ni maandiko mengine ukutani ambayo CCM lazima itakuwa imeyaona na kuyasoma vyema kwa sababu ya ukubwa wa herufi zake! Itakuwa imeweza kuyasoma hata kama ina makengeza!

Na maandiko hayo ukutani yanasomekaje? Yanasomeka hivi: "Ni wakati wa mabadiliko. Tumeichoka CCM kiasi kwamba hata shetani tuko tayari kumpigia kura aingie Ikulu".

Huo ni ujumbe mzito na unaotisha, na ni chama-mfu tu cha kisiasa ndicho kinachoweza kuudharau ujumbe wa namna hiyo. Watu wakishafikia hatua ya kukata tamaa kimaisha kiasi cha kusema kwamba hata kama ni shetani wako tayari kumwingiza Ikulu, ni lazima CCM kijiulize; kulikoni?

Na ujumbe huo si mtupu (hollow). Ni ujumbe unaoendana na hali ambayo imekuwa ikionekana katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa – yaani maelfu ya vijana waliokata tamaa ya maisha hufurika katika mikutano yake kumsikiliza.

Hata hivyo, kitakachoikoa CCM na kumfanya Magufuli ashinde urais Oktoba 25 ni kwamba, tofauti na Chadema, chenyewe kina muundo na mtandao wa hadi ngazi za vijiji na kata uliokiwezesha kuhahakikisha kila mwanachama wake amejiandikisha kupiga kura na siku ya kupiga kura kuhakikisha anajitokeza kupiga kura.

Chadema hakina muundo huo, na pia hakina mtandao huo wa hadi ngazi ya vijiji na kata. Kwa hiyo, kinabakia tu na imani (potofu!) kuwa vijana wote wanaofurika kwa maelfu katika mikutano ya kampeni ya Lowassa wamejiandikisha kupiga kura - kumbe ukweli ni tofauti kabisa na huo. Kasoro hiyo ndio iliyomwangusha
Dk. Slaa mwaka 2010, na ndio itamwangusha Lowassa Oktoba 25.

Lakini Chadema na ACT Wazalendo nk haviwezi kukubali kubakia na udhaifu huo huo kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020. Bila shaka navyo vitajitahidi kuweka ofisi na mitandao ya hadi ngazi za vijiji na kata, na hivyo uchaguzi mkuu mwingine wa mwaka 2020 unaweza kuleta matokeo tofauti kabisa na tutakayoyapata Oktoba 25 mwaka huu.

Na ndiyo maana nasema ya kwamba kama CCM kinataka bado kuendelea kukamata dola, ni lazima baada ya Oktoba 25 kifanye mageuzi makubwa yatakayoipa serikali yake mwelekeo mpya wa kutatua kero ambazo kwazo zilifanya vijana wafurike katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa wakiwa na mategemeo kwamba ndiye atakayetatua matatizo yao.

Yaani kama kama tatizo ni ajira, basi serikali ijayo ya CCM ni lazima ionekane kweli kweli ikitatua tatizo hilo. Kama tatizo ni maji, basi lazima liwe historia ifikapo mwaka 2020. Au kama tatizo ni kilimo duni na ukosefu wa masoko kwa wakulima, serikali ijayo ya CCM lazima ilitatue hilo kabla ya mwaka 2020. Na kama tatizo ni kutamalaki kwa ufisadi nchini, basi lazima janga hilo liwe limemalizwa ifikapo mwaka huo.

Vinginevyo, CCM kitakwenda na maji ifikapo 2020! Safari hii kitashinda uchaguzi kwa taabu, lakini safari ijayo kisipojirekebisha kitashindwa kiurahisi. Ndiyo maana naamini ya kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Lowassa ameisaidia/ataisaidia mno CCM kujiona kilivyo, na ndio sababu naamini kwamba baada ya Oktoba 25 ‘kitajivua gamba' lake la zamani.

Vyovyote vile, kwa kuwa hii ndiyo makala yangu ya mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, napenda nirudie kile ambacho nilikisema huko nyuma. Kitu hicho ni kwamba wagombea wote wawili wa urais – Lowassa na Magufuli wana mapungufu ya wazi.

Niliandika huko nyuma kwamba pamoja na wote kuwa na mapungufu makubwa kuna mmoja ambaye ni nafuu kidogo kuliko mwenzake (a lesser devil). Ombi langu ni lile lile: Kwa kuwa wote wana mapungufu makubwa tutajitakia balaa kama tutampa lesser devil wetu wingi wa wabunge wa chama chake bungeni. Yaani akivurunda tutakuwa hatuna njia ya kumdhibiti bungeni kwa sababu atakuwa na wingi wa wabunge.

Kwa hiyo, salama yetu ni kwamba yeyote tutakayempigia kura – awe Lowassa au Magufuli, tusimpigie kura mgombea ubunge wa chama chake. Kwa mfano, kama kura ya urais unampa Lowassa, basi kura ya ubunge mpe mgombea wa CCM au ACT Wazalendo. Na kama kura yako ya urais unampa Magufuli, basi kura ya ubunge kipe Chadema au ACT Wazalendo.

Kwa namna hiyo, tutajipa matumaini (japo kidogo) kwamba yeyote atakayeshinda urais kati ya hao wawili, Bunge litaweza kumdhibiti kama ataongoza nchi hovyo. Lakini kama akiwa na wingi wa wabunge wa chama chake bungeni (kama ilivyokuwa kwa CCM kwa miaka mingi), hatutaweza kumfunga ‘gavana' hata kidogo kama akivurunda.

Na mwisho kabisa nawatakia uchaguzi mwema na wa amani Oktoba 25. Nikirejea Desemba nitaendelea kuandika makala za kumkosoa (kwa hoja) mtawala wetu mpya bila kujali ni Magufuli au Lowassa; maana hiyo ndiyo kazi niliyojitwisha katika fani hii ya uandishi wa habari.

Sikuingia katika fani hii ili kuwaremba na kuwasifu watawala wakiwa madarakani. Nitawasifuje watawala kama wanatekeleza kile ambacho wananchi walikitarajia wakati wanawapa kura zao?

Nimeingia katika fani hii kuwakosoa watawala wanapovurunda ili wasilale usingizi; ilhali wananchi wanateseka. Kazi hiyo nitaendelea nayo bila kujali rais mpya ni Magufuli au Lowassa.

Vyovyote vile, rais akichapa vyema kazi hakuna ‘habari' hapo. ‘Habari' ni pale rais anapokuwa mvivu, mlevi, legelege, fisadi nk. Kwenye taaluma yetu ya habari tuna msemo maarufu; mbwa akimng'ata binadamu hakuna habari. Habari ni binadamu akimng'ata mbwa.

Kwa maana hiyo, nitaendelea kuwakosoa watawala wetu, na sitajali ni Magufuli niliyempigia kura yangu au Lowassa. Nitamkosoa (kwa hoja) yeyote kati ya hao wawili atakayefanikiwa kuingia Ikulu Oktoba 25; maana hakuna ‘habari' katika kumsifu.

Tafakari.
Atashinda kwa mafuliko haya ambayo watu wana zimia kwa kukosa hewa. Huu muda uliotumia ktk kuandika hii Topic ndefu kiasi hiki ungeutumia kutunga vitabu vya watoto kama vile vya kina Abengu na nzige.
 
Attachments

al4nce

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
397
195
Haina ubishi Magufuli atashinda tena kwa kura nyingi, 25 October ni mwisho wa maigizo na ndio mwanza wa watu kukimbia Account zao
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,102
2,000
Atashinda kwa mafuliko haya ambayo watu wana zimia kwa kukosa hewa. Huu muda uliotumia ktk kuandika hii Topic ndefu kiasi hiki ungeutumia kutunga vitabu vya watoto kama vile vya kina Abengu na nzige.
Kwa kauli hz tu ni kujifurahisha nafsi yako kwa kua unapenda upinzani,ni kweli tunataka mabadiliko lakini mahali kama bado panapwaya ni lazima tuseme na tubuni mbinu mpya ya kupata ushindi,ni kweli upinzani umejaa mbwembwe za kutafuta dola,lakini ccm bado wanatumia akili sana ktk kuendelea kuitafuta dola,kukubali kukosolewa ni muhimu sana ili ujifunze,lakini kujifanya unajua kila kitu na kutoa kashifa ni kujipotezea muda
 
mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
2,852
2,000
Mimi nitapigia ccm urais ubunge na udiwani japo siipendi ccm kabisa. Ila nataka tuwape shule wapinzani wasidharau wananchi ikiwa ccm mara hii imetuheshimu.
 
edsoysoma

Senior Member
Oct 1, 2015
145
225
Je, hili la JPM kutokuwa fasaha kwenye English haliashilii kututia aibu kwenye meadani za kimataifa au haina neno?
 
vidal

JF-Expert Member
May 28, 2015
311
225
Atii vijana wabodaboda ukiwauliza kwann mnaichukia ccm, jibu lao wametukataza kufika mjni, kwa akili hii ndo unaitaji change
 
Cool Runnings

JF-Expert Member
Feb 4, 2013
278
195
Vyovyote vile, ubashiri wangu ni kwamba Magufuli atashinda. Ubashiri wangu mwingine ni kwamba kuhamia kwa Lowassa katika Chadema na kampeni ya urais aliyoifanya hakutaleta mabadiliko makubwa kwa chama hicho kwa maana ya kuongeza viti vya ubunge.

Kwa hiyo, kwa upande wa Chadema, ujio wa Lowassa utakuwa umekidhoofisha tu chama hicho kiutendaji kiuliko kilivyokuwa huko nyuma. Baada ya Oktoba 25, hali ya Chadema itakuwa mbaya, na kama nilivyopata kusema awali, sitashangaa ACT Wazalendo kikiziba baadaye pengo la Chadema kama chama kikuu cha upinzani nchini. Ni suala la muda tu hilo kutokea.

Na hili linanikumbusha maneno ambayo (sina hakika na ukweli wake) niliyoambiwa hivi karibuni na swahiba mmoja wa karibu wa Lowassa kwamba mheshimiwa huyo alipoamua kujiunga na Chadema ili agombee urais alijua fika kwamba hatashinda urais huo kupitia chama hicho!

Kwa mujibu wa maelezo yake aliyodai kaambiwa na Lowassa mwenyewe, swahiba huyo anasema Lowassa aliamua kugombea urais kupitia Chadema ili ‘kukiadhibu' chama hicho kwa kumchafua kwa zaidi ya miaka tisa kuwa ni fisadi mkubwa.

Lakini pia aliamua kugombea urais kupitia chama hicho ili kupata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa Rais Kikwete ambaye aliweka kando uswahiba wao na kumtosa wakati ule alipoandamwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond kiasi cha kumlazimisha kujiuzulu uwaziri mkuu.

Swahiba huyo wa Lowassa aliniambia ya kwamba ‘adhabu' ya kwanza kwa Chadema ni huo mparaganyo uliosababisha Katibu Mkuu wa chama hicho aliyeshiriki sana kukijenga, Dk. Slaa kujiuzulu nafasi yake. Si siri kwamba mpaka sasa Chadema kinapwaya kwa kumkosa mtu wa sampuli ya Dk. Slaa kukaimu nafasi hiyo.

Adhabu ya pili au tuseme pigo la pili la Lowassa kwa Chadema ni hilo la ‘kuwalazimisha' kina Mbowe na Lissu ambao walikuwa vinara wa kumwita fisadi, kuyameza matapishi yao wenyewe kwa kumsafisha wakati wa kampeni za urais kuwa si fisadi.

Kwa mujibu wa swahiba huyo wa Lowassa, hakuna jambo linalomfurahisha mgombea urais huyo wa Chadema hivi sasa zaidi ya kuwaona Lissu na Mbowe wakihaha jukwaani kujaribu kuuaminisha umma kuwa walikosea kumwita Lowassa fisadi.

Yaani anafurahi kuwaona wakimeza matapishi yao wenyewe!

Kwa mtazamo wake, hiyo ni adhabu kubwa kwa kina Mbowe na Lissu kwa sababu heshima yao, weledi wao, uungwana wao, uadilifu wao na uaminifu wao kwa wanachama wa Chadema sasa uko shakani kwa sababu ya ‘kumeza' matapishi yao hayo.

Kwa maana hiyo, Lowassa anajiona ‘kalipiza kisasi' kwa vinara hao wa Chadema waliomwita fisadi, na kwa Chadema yenyewe ambayo anaamini itasambaratika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25!

Kuhusu kulipiza kisasi kwa Kikwete, swahiba wake huyo alinieleza ya kuwa kwa
kugombea urais kupitia Chadema, Lowassa amepata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa kumpaka matope Kikwete wakati wa kampeni kuwa utawala wake wa miaka 10 ulikuwa hovyo kabisa, na kwamba ndiye aliyemlazimisha kuutia saini mkataba wa kifisadi wa Richmond. Fursa hiyo asingeipata kwa kiwango anachopata hivi sasa wakati wa kampeni za urais.

Kama hayo aliyonieleza swahiba huyo wa Lowassa ni ya kweli, basi inamaanisha kuwa tangu mwanzo Lowassa alijua ya kuwa hatashinda urais kupitia Chadema, na alichokifanya, hivyo basi, ni kutafuta tu fursa ya kulipiza visasi kwa Chadema na Kikwete.

Bila shaka anafanya hivyo kwa sababu hana cha kupoteza. Sitashangaa baada ya Oktoba 25 akajirudia Monduli kustaafu kabisa mambo ya siasa; maana atakuwa amemaliza ‘kuwashughulikia' waliomwita fisadi kwa miaka tisa.
Uandishi muflisi kabisa huu, ni bora ukienda kulima huko usirudi tena kwenye tasnia ya habari!
 
Clemence Baraka

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,600
1,500
ivi iyo mikutano au matashama ya bongo flv? Ili ujue kama chaguo la watu kama rais Lowasa, Mwambie afanye mkutano bila bongoflv alafu asibebe watu kwa Magar kama mfanyavyo kama mtapata mtu hata mmoja
Lakini Buholela anaonyesha makundi mengi makubwa njiani yanayomsimamisha mgombea kutaka awazungumzie. Njiani hakuna bongo fleva. AU?
 
Jonas kitiga

Member
Aug 14, 2015
5
0
Pole mbwambo kwa kuzeeka vibaya kujaribu kuwaaminisha vijana wa tz ambao ndo wengi na ndo wanataka mabadiliko
Huo usaliti wa taaluma zenu utawagharimu mbele za haki
Unajifanya unazungukazunguka kurefusha makala zako kujiokotea sh.5000 za bia na zawad kwa wapenz wenu
Jiandaen kuishi uhamishon
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,228

Jonas Kitiga, pole zako huyo mbwa wako haingii Ikulu ya Magogoni labda aingie ya Monduli. Utaishia kubywa viroba tu kwenye bodaboda
 
Jigsaw

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
1,826
1,250
Kwa kauli hz tu ni kujifurahisha nafsi yako kwa kua unapenda upinzani,ni kweli tunataka mabadiliko lakini mahali kama bado panapwaya ni lazima tuseme na tubuni mbinu mpya ya kupata ushindi,ni kweli upinzani umejaa mbwembwe za kutafuta dola,lakini ccm bado wanatumia akili sana ktk kuendelea kuitafuta dola,kukubali kukosolewa ni muhimu sana ili ujifunze,lakini kujifanya unajua kila kitu na kutoa kashifa ni kujipotezea muda
Kama wewe ulivyojipotezea muda katika kunifundisha kipi napaswa kuamini sio. Hakuna anaye jua kila kitu, Labda mungu tu. Week end njema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom