Magufuli atafia ufisadi, mimi nitafia demokrasia

Magufuli atafia ufisadi, mimi nitafia demokrasia

Makala
zitto.jpg

Magufuli atafia ufisadi, mimi nitafia demokrasia
Zitto Kabwe
Toleo la 461
8 Jun 2016

MWAKA 2015 tulikwenda kwenye uchaguzi kuchagua madiwani, wabunge na Rais. Baada ya Uchaguzi kumalizika serikali mpya iliundwa pamoja na serikali za mitaa kuundwa. Baada ya uchaguzi tumeona viongozi wapya wakichukua hatua mbalimbali nzuri na mbaya, zenye kujenga na kubomoa, zenye kuimarisha demokrasia na zinazobomoa demokrasia.

Tumeshuhudia maamuzi mengine ambayo yanatia hofu kwamba ingawa tunaona dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi, lakini pia tunaona mbinu za chini chini za kutokomeza demokrasia ya nchi yetu ambayo tumeijenga kwa jasho na damu.

Leo nitagusia baadhi ya maeneo ambayo nadhani ni vihatarishi vya ustawi wa wananchi wetu na ambavyo lazima tuanze kuvipinga mapema sana kabla havijaota mizizi.

Baadhi ya maeneo ninayotaka kuyazungumzia leo ni wabunge kusimamishwa kazi za Bunge, maamuzi ya serikali kuhusu Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hali ya Zanzibar, mwelekeo wa Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Rais John Magufuli na tishio la nchi kuelekea kwenye utawala wa imla wa MTU mmoja.

Wabunge kusimamishwa kazi
Mei 30 mwaka huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Naibu Spika lilipitisha Azimio la Bunge la kuwasimamisha kazi wabunge saba kwa vipindi mbalimbali. Wabunge wawili, Esther Bulaya na Tundu Lissu walisimamishwa kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge.

Wabunge wanne; Halima Mdee, Pauline Gekul, Godbless Lema na mimi tulisimamishwa kuhudhuria mkutano mmoja –ambao ni huu unaoendelea wa bajeti na mbunge mmoja, John Heche, amesimamishwa vikao 10 vya mkutano huu wa tatu unaoendelea.

Sababu iliyoelezwa na Bunge ni kwamba wabunge hawa walifanya fujo siku ya tarehe 27 Januari 2016, kutokana na hoja niliyoitoa bungeni ya kutaka mjadala kuhusu sababu za hovyo za uongo zilizotolewa na Serikali kuhusu uamuzi wa kuzuia Shirika la Utangazaji la Taifa ( TBC ) na televisheni binafsi nyengine kuonyesha moja kwa moja mikutano ya Bunge.

Mimi binafsi pamoja na wabunge wengine sita tuliosimamishwa kwa vipindi tofauti, hatukufanya fujo yeyote ndani ya Bunge. Kosa letu kubwa ni kutaka kuhoji maamuzi ya serikali ambayo kwa maoni yetu hayana msingi wowote.

Serikali inasema ninyi wananchi hamfanyi kazi kwa sababu Bunge linaonyeshwa wakati wa kazi. Hata hivyo, serikali hiyo hiyo inatuaambia kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita uchumi wa Tanzania ulikua kutoka shilingi 16 mwaka 2005 mpaka shilingi trilioni 99 mwaka 2015.
Kipindi chote hiki Bunge lilikuwa linaonyeshwa moja kwa moja na televisheni za TBC na StarTV. Kama mngekuwa hamfanyi kazi, uchumi usingekua kwa kiwango hicho cha asilimia 600 ndani ya muongo mmoja wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Utawala wa Rais Magufuli unataka kutuaminisha kuwa ukiwa na Bunge ‘live’ watu hawafanyi kazi lakini uongozi uliopita umedhihirisha kwa ushahidi kuwa ukipanua demokrasia na kuwaonyesha wananchi kila kinachoendelea bungeni, uwezo wa kazi unaongezeka na uwezo wa wananchi kuwajibisha viongozi wao unaongezeka.

Hivyo Serikali kuamua kuficha Bunge ni mbinu za kuendesha serikali kwenye giza ili kufanya maamuzi ambayo baadaye ionekane serikali tu au Rais tu ndiye mfanya kazi. Ndio maana mikutano yote ya Rais anapohutubia huonyeshwa moja kwa moja lakini sio Bunge.

Wabunge wamesimamishwa kwa sababu ya kukataa Bunge kuendeshwa kwenye giza. Wabunge waliosimamishwa walisimama kidete kuhoji sababu za serikali kufikia maamuzi hayo.
Walitaka kujua kwanini Serikali imekuwa kigeugeu kwa kubadilisha badilisha sababu zake za kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Wakati mmoja serikali ilisema sababu ni gharama, kama ni hivyo ni kwanini walizuia StarTV na AzamTV kuonyesha moja kwa moja?

Ni dhahiri serikali inataka kuendesha mambo yake kwa uficho kwa sababu kuna maamuzi inataka kufanya na haitaki wananchi mjue mapema maamuzi hayo. Serikali inaturudisha nyuma badala ya kwenda mbele.

Wabunge waliosimamishwa ni wabunge wenye uwezo wa kujenga hoja. Kuna wengine wamebaki bungeni wenye uwezo mkubwa tu wa kujenga hoja, lakini hawa saba waliosimamishwa ni wabunge waliojidhihirisha kwa muda mfupi kwa baadhi yao kama Heche, wanaweza kusimamia hoja zao bila woga.

Swali la kujiuliza ni hili, tukio ambalo limetokea mwezi Januari ni kwanini adhabu yake itolewe mwezi Juni –tena wiki moja tu kabla ya Waziri wa Fedha kuwasilisha bungeni Bajeti ya Serikali?
Katika waliosimamishwa, Halima Mdee ni Waziri Kivuli wa Fedha, na mimi huko nyuma niliwahi kuwa na wadhifa kama huo. Kuna nini? Nitawaeleza katika hoja ya bajeti.

Kimsingi Utawala wa Rais Magufuli umepanga kupandisha kodi za wananchi masikini na uliona uwepo wetu bungeni utatibua mipango yao. Rais na wenzake ndani ya CCM hawapendi kusikia hoja zinazowapinga, hawana uvumilivu wa kukosolewa na hivyo walipanga kuhakikisha kuwa baadhi yetu hatutakuwepo kwenye mjadala wa bajeti ili kufanikisha malengo yao ya kufanya maamuzi yatakayowandamiza wananchi.

Nitaeleza vizuri hili zaidi baadaye kwenye makala hii. Nataka Watanzania wajue kuwa kusimamishwa kwetu ni ajenda maalumu ya serikali ya Rais Magufuli kufunika mjadala wa bajeti kwa sababu anajua kuwa tunajua wanachotaka kufanya dhidi ya “walalahoi” wa nchi yetu.
Sisi hatutakaa kimya, tutatumia wenzetu waliopo bungeni kuyasema haya na pia tutazungumza na wananchi kuwaeleza pia. Tutatumia mikutano yetu mbalimbali bila kujali itikadi za vyama vyetu kuhakikisha kuwa wananchi wanajua kila kinachoendelea na kuwataka kuunganisha nguvu kukataa udikteta unaonyemelea nchi yetu.

Wanafunzi 7800 kufukuzwa Chuo Kikuu Cha Dodoma
Mmesikia sakata la wanafunzi wa UDOM waliokuwa wanasomea programu maalumu ya ualimu wa Sayansi. Hawa ni watoto wa Watanzania masikini waliokubali kuacha kwenda ‘A level’ na kukubali kusomea diploma ya Ualimu ili wakawafundishe watoto wa masikini wenzao.
Wanafunzi hawa hawakuanzisha wao program hii. Ilianzishwa na serikali na kupitishwa na Baraza la Mawaziri ambalo Rais Magufuli alikuwa mjumbe na alishiriki kikao hicho kwa mujibu wa kumbukumbu za Baraza la Mawaziri.

Rais Magufuli hakupinga mpango huu na aliubariki kama wenzake walivyofanya na kuanza kutekelezwa. Lengo la program hii ni kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi. Tanzania ina uhaba wa walimu wa Sayansi 26,000 na tukienda kwa utaratibu wa kawaida tutahitaji miaka 20 kuziba pengo hilo.

Program hii ilianzishwa ili kuziba pengo hili kwa muda mfupi na vijana waliitikia wito huu wa kizalendo kuhakikisha wadogo zao hawakosi walimu siku za usoni.
Serikali ya Awamu ya Tano imewafukuza vijana hawa 7800 kutoka chuoni ndani ya masaa 24 kwa makosa ambayo si yao. Sisemi kuwa program haikuwa na kosoro. Zilikuwepo ikiwemo kudahili wanafunzi wengi zaidi ya ilivyotarajiwa.

Lakini aliyedahili si watoto hawa bali ni serikali yenyewe, kwanini waadhibiwe watoto? Bunge lilipotaka kujadili hoja hii au hata kuipeleka kwenye Kamati ya Bunge kuifanyia uchunguzi na kutoa mapendekezo, Naibu Spika, Tulia Ackson, alizuia hoja ya mbunge Joshua Nasari bila sababu za msingi.

Wabunge wote, bila kujali vyama vyao, walitaka hoja ijadiliwe ili kuweza kupata majawabu. Mbona wakati wa uongozi wa awamu ya nne tulijadili hoja ya mgomo wa madaktari na kisha kupelekwa kwenye kamati husika ya bunge kupata suluhisho la kudumu?

Kwanini utawala wa Rais Magufuli hautaki Bunge lifanye kazi yake? Mbona yeye Rais kaenda kujadili jambo hilo huko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani)?
Rais Magufuli anafikia kuita watoto wetu ******? Rais huyu anayesema yeye ni Rais wa masikini anaita watoto wa masikini ******. Vijana hawa wazalendo waliojitoa muhanga kuacha kwenda kidato cha tano ili wasome kuwa walimu na kulea kizazi kijacho Rais wao anawaita ******.

Rais sifa zimempanda kichwani. Rais Magufuli hana budi kuwaomba radhi vijana hawa na wazazi wao. Rais ni mwalimu, anajua madhara ya kisaikolojia kufuatia maneno aliyoyasema. Ni sawa na Jenerali wa Jeshi anayetukana askari wake walio mstari wa mbele.
Hata Baba wa Taifa hakuthubutu kamwe kuita wanafunzi ****** hata kama walimuudhi kiasi gani. Rais Magufuli anaongea mno na hii si sawa kwa kiongozi.

Rais ajue kuweka akiba ya maneno. Yeye ni kiongozi wa wote, wenye akili na ******. Yeye anapaswa kuwa wa mwisho kuongea ili watu waweze kukataa rufaa kwake. Yeye akishaongea wananchi walioonewa waende kwa nani? Waende kwa Mungu?
Tunamtaka Rais awarudishe wanafunziwa UDOM mara moja na wale wanafunzi ambao itaonekana hawakuingia kwenye program kihalali waondolewe badala ya kuadhibu watoto wote kwa makosa ya wachache ambao ni asilimia tano tu ya wote.

Makosa madogo ni mambo ya kawaida katika jamii. Yeye Rais ni mfano mzuri wa hili kwani naye mbona aliteua waziri mlevi na kurekebisha kwa kumfukuza peke yake, mbona hakufukuza baraza zima la mawaziri kwa ulevi wa waziri mmoja?

Zanzibar
Mnajua mara baada ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar kufutwa chama chetu cha ACT-Wazalendo kiliweka msimamo wa wazi kwamba kinatambua ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad kama Rais aliyechaguliwa na Wazanzibari na anayepaswa kula kiapo na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Tuliandika pia masuala 10 muhimu kwa Rais kuyafanyia kazi na moja ya jambo tulilomtaka Rais Magufuli kufanyia kazi ni suala la demokrasia ya Zanzibar. Rais hakusikia wito wetu na aliruhusu ufutwaji usio halali kisiasa wala kisheria wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015.
Nasisitiza ACT Wazalendo hakiutambui uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika mwezi Machi mwaka 2016 na matokeo yake yote yaliyofanyika. Kwa maana hiyo hatutambui Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na hata Rais wa Zanzibar.

Hivi karibuni kumekuwa na kuongezeka kwa sintofahamu huko Zanzibar kufuatia mgombea Urais aliyeshinda na kunyang’anywa ushindi wake kwenda kwa wananchi kuzungumza nao.

Hali hii imesababisha Jeshi la Polisi kumhoji Maalim Seif na siku mbili baadaye Dk. Ali Mohammed Shein kutamka kuwa hamwogopi Maalim Seif kwa sababu hana vifaru na mizinga.
Ninalaani kauli hii ya Dk. Shein ya kutisha kwa vifaru na mizinga. Kamwe huwezi kuzima haki za wananchi kwa vifaru na mizinga. Shein akumbuke kuwa Sultan alikuwa na jeshi, vifaru na mizinga na ulinzi wa dola kubwa kama Uingereza lakini aliangushwa na wananchi wa Zanzibar mwaka 1964.

Shein akumbuke kuwa nchi kadhaa duniani zilikuwa na madikteta wenye vifaru na mizinga lakini waliondoka. Ninamtaka Shein afute kauli yake hii na kuacha vitisho badala yake aanze mchakato wa kupata maridhiano ya jamii ya Zanzibar. Hatutaki kurithi damu, tunataka kurithi nchi yenye amani, haki na demokrasia.

Ninajua hali mbaya ya kisiasa iliyopo Zanzibar na mkwamo uliopo hivi sasa. Hata hivyo ni lazima tupate jawabu kupitia sanduku la kura.
Napendekeza kuwa vyama vikuu vya siasa Zanzibar vikubali ‘kufa kidogo’ yaani ‘to die a little’ kwa vyote kukubali kuwa chaguzi za mwaka 2015 na ule wa mwaka 2016 zilizofanyika visiwani humo zote zilikuwa batili, zifutwe na Uchaguzi Mkuu mpya uitishwe.

Uchaguzi huo utanguliwe na Serikali ya Mpito itakayohusisha vyama vyote vya siasa na baadhi ya wanajamii wanaoheshimika na Wazanzibari wote ili kujenga kuaminiana. Hii itatupa nusura ya Zanzibar.

Nawaomba Wazanzibari watumie mwezi mtukufu wa Ramadhani kutafakari maoni haya na wote kwa pamoja baada ya Ramadhani kuja na jawabu ya hali ya kisiasa.
Tunatamani Zanzibari irudi kwenye hali ya kawaida na ishamiri. Zanzibar ikiingia kwenye mtafuruku, Tanzania nzima itakuwa kwenye mtafaruku. Ni dhahiri kuwa Rais Magufuli ameshindwa kutoa uongozi kwenye suala hili na hivyo ni wajibu wa Wazanzibari wenyewe kukaa na kupata mwafaka wa kijamii na kusonga mbele.

Bajeti ya 2016/17
Kuanzia Juni 8, 2016 Bunge litakuwa kwenye mjadala wa bajeti ya kwanza ya Serikali ya Rais Magufuli. Rais ameleta mapendekezo ya bajeti ya shilingi trilioni 29.5.
Katika makadirio haya, vyanzo vya ndani ni shilingi trilioni 18.5 na misaada ni shilingi trilioni 3.6. Serikali inatarajiwa kukopa jumla ya shilingi trilioni 7.4.
Mwaka 2015/16, serikali ilitarajiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 13.8, hivyo ndani ya mwaka mmoja wa fedha, utawala wa Rais Magufuli unataka kukusanya shilingi 4.7 trilioni zaidi –sawa na ongezeko la asilimia 25.
Kwa ufupi ni kwamba serikali haina budi kuongeza kodi kwa kiwango cha asilimia 25 ili kuweza kutimiza malengo yake ya makusanyo.
Mtakumbuka kuwa mara baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani, tulikuwa tunaelezwa kodi iliyokusanywa kila mwezi na tuliona wafanyabiashara wakikabwa koo kwa kukwepa kodi.
Hata hivyo, ongezeko la makusanyo lilikuwa kwa miezi miwili tu ya Novemba na Desemba kwani kuanzia mwezi Januari makusanyo yalianza kuendana na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na ndio maana mbwembwe za makusanyo hazisikiki tena hapa nchini.
Ukweli ni kwamba Rais alikuwa anakusanya fdha ambazo hazikuwa zimekusanywa na hapakuwa na hapajakuwa na mbinu mpya za kukusanya mapato ya serikali.
Maeneo muhimu yanayopoteza mapato kama vile makampuni ya nje kutumia mbinu za kihasibu kukwepa kodi hayajatazamwa kabisa na Rais na wasaidizi wake. Hivyo, serikali imeamua kurudi kwa wanyonge kuwaminya na kodi ikianzia kuchukua kodi zote majengo kutoka kwenye halmashauri zetu.

Kodi za majengo ndio chanzo kikuu cha mapato ya Halmashauri zetu za Miji. Manispaa na Majiji. Uamuzi wa serikali kuchukua chanzo hiki cha mapato utasababisha halmashauri zetu kushindwa kuzoa taka na hata kutoa huduma kwa wananchi.

Hata hivyo, uamuzi huu inaonekana umechukuliwa kwa sababu halmashauri nyingi za miji mikubwa zinaongozwa na vyama vya upinzani kama vile Manispaa ya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Iringa, Arusha, Ilala, Kinondoni, Mbeya Jiji na kwingineko.

Utawala wa Magufuli unataka kuhakikisha kuwa manispaa zinaoongozwa na vyama vya upinzani zinashindwa kutoa huduma. Duniani kote kodi za majengo hukusanywa na Serikali za Mitaa. Katika Bajeti ya mwaka huu kodi hizi zitaongezwa maradufu.

Serikali inatarajia kupandisha ushuru kwenye soda, vilevi na sigara pia kwa mujibu wa vitabu vya bajeti vilivyogawiwa kwa wabunge. Hata kodi kwenye gharama za kupiga simu zitaongezwa kwa zaidi ya asilimia 10.

Eneo la ushuru peke yake serikali inataka kukusanya shilingi trilioni 1.2 kutoka shilingi bilioni 900 za mwaka uliopita. Hii ni nyongeza ya shilingi 300 bilioni zaidi kutoka bajeti ya mwaka 2015/16.
Maeneo haya mawili peke yake ( kodi za majengo na ushuru wa bidhaa ) yataongezewa kodi kiwango cha kuumiza sana wananchi wa kawaida. Hii ndio sababu serikali imefukuza baadhi ya wabunge mahiri bungeni ili kulainisha upitishwaji wao wa viwango hivi vya kodi.
Hata hivyo tutatumia wabunge wenzetu waliobakia bungeni kuhakikisha kuwa kodi kwa wananchi masikini haziongezwi kiholela. Sisi tunaamini kuwa bajeti ya shilingi 29.5 trilioni ya Utawala wa Magufuli si bajeti halisi kwani makadirio yao hayazingatii ukuaji wa uchumi na yana lengo la kuchukua fedha kutoka kwa wananchi kupeleka serikalini, jambo ambalo litadidimiza uchumi wa nchi yetu.

Tishio la Demokrasia
Jambo la mwisho ambalo ninataka kuwaeleza ni tishio lililopo mbele yetu dhidi ya demokrasia ya vyama vingi. Hatua mbalimbali ambazo utawala wa Magufuli unachukua ni ishara ya kutengeneza utawala wa imla.
Rais ndiye anayejua kila kitu na ndiye anayeamua kila kitu. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu na ni lazima kuchukua hatua mahususi kumkatalia Rais mwanzoni kabisa ili asizoee.
Nilimwunga mkono toka mwanzo katika vita dhidi ya ufisadi kwani ni vita muhimu na lazima ipiganwe bila kujali itikadi za vyama. Hakuna namna unaweza kumlaumu Rais anapochukua hatua za kusafisha uvundo katika nchi. Pasipo shaka yoyote nitaendelea kumwunga mkono katika eneo hilo.

Hata hivyo, Rais anatia hofu mno katika ujenzi wa mfumo wa uwajibikaji. Tanzania ina vyombo vya kuimarisha uwajibikaji ikiwemo Bunge na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT).
Rais anataka kupigana dhidi ya ufisadi nje ya mfumo jambo ambalo ni la hatari sana kwa nchi kwani akitoka yeye tutaanza upya. Inawezekanaje kiongozi anayepambana na rushwa akavunja nguvu ya NAOT kwa kumpunguzia bajeti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)?

Rais amediriki hata kuvunja Katiba na Sheria ya Ukaguzi kwani bajeti ya CAG haipangwi na serikali bali hupangwa na Kamati ya Bunge. Hata hivyo Rais ameenda kinyume na sheria na badala yake kapanga mwenyewe bajeti ya CAG? Tangu lini mkaguliwa akapanga bajeti ya anayemkagua? Kamati ya Bunge ilipanga bajeti ya shilingi bilioni 69 kwa CAG lakini serikali ( mkaguliwa ) imeipiga panga mpaka shilingi bilioni 32.

Hii ni moja ya mfano dhahiri kabisa wa serikali kuanza kuvunjavunja vyombo vya uwajibikaji. Hivi sasa kuna ukosefu wa sukari nchini. Rais alisimama kwenye majukwaa ya siasa na kutoa matamko makali kwamba kuna wafanyabiashara wameficha sukari na tukaonyeshwa sukari hiyo.
Hata hivyo baada ya siku chache vyombo kama PCCB na TRA vikasema sukari ile ni halali. Inakuwaje Rais alitamka maneno yale bila ya kushauriana na vyombo? Ni dhahiri Rais anaongea tu na kutaka kujenga utawala wa imla. Leo bado kuna shida ya sukari na sukari ambayo serikali inasema iliagiza haionekani. Ipo wapi?

Rais alikwenda BoT na kusema nusu ya wafanyakazi pale ni hewa. Mpaka leo hatujaona hao wafanyakazi hewa wa BoT wakielezwa. Rais alikwenda tu kwa kupata maneno yasiyo na ushahidi na kutoa matamko ambayo yanashusha hadhi ya Benki Kuu lakini anashindwa kutoka mbele kusema alikosea.

Leo nataka kumwambia Rais kuwa aongoze, asitawale. Rais awe na utu na wananchi wake. Rais awe anasikiliza kwanza na kuchambua mambo kabla ya kusema chochote mbele ya hadhara.
Rais awe wa mwisho kusema ili kama kuna rufaa watoe waseme kwake. Vinginevyo Rais anataka kujenga utawala wa imla na tutamkatalia wazi wazi.
Rais amesema kuwa yeye amejitoa muhanga kupambana na ufisadi. Sisi tunalazimika kujitoa muhanga kulinda demokrasia. Ni imani yetu kuwa ufisadi utapigwa vita kikamilifu si kwa kutegemea nia ya mtu mmoja bali kwa kuboresha na kutumia misingi ya demokrasia kwa kujenga taasisi madhubuti zitakazomaliza janga la ufisadi bila ya kutegemea nia ya Rais.
Naamini kuwa ni jukumu letu kusimama na kujitoa mhanga kuzuia maafa ya kitaifa yatakayoweza kutokea kutokana na makosa ya kukandamiza demokrasia na uhuru wa mawazo kwa kuhoji, kukosoa na kurekebisha makosa hayo sasa bila kuchelewa.

Mwandishi wa makala hii ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo

umeandika sana lakini hunapoint yeyote. kama serikali inaweza kudhibiti rushwa na kuleta maendeleo, what else?. badilisheni hizo siasa mlizozianza upinzani vinginevyo mtaishia kulalamika. nenda kigoma kawasaidie wananchi kubuni miradi. tena raisi akiweza kumaintain speed hii kwa suport ya wananchi,2025 tunatengeneza kagame wetu.
 
Hujitambui wewe hivi huu ubakaji demokrasi nchini hadi sasa umemuathiri Zitto tu!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka.

Jema lipi hapa unalozungumzia? La kuwakwepa mafisadi wa Lugumi, escrow, UDA, Pride, MV Dar au Rais kukwepa kulipa kodi!?

Wakati mwingine najiuliza sijui hata shule mlienda kufanya nini ? Etii mshahara wa rais kwanini haukwati kodi hivi umesoma katiba ya nchi kujua mshahara wa rais unakatwa kodi au la! Au ndio mpka mropokaji tundu lissu akufafanulie

Pia unapozungumzia ufisadi nchi hii back to early 1990 ambapo , kundi rasmi la kifisadi lilianza kujijenga ndani ya CCM na king maker wake alikuwa nani? Na sasa huyo king maker yuko chama gani ? Alafu ukishayajua ndio uropoke ,

Nyie mnahitaji somo kubwa sana la kubadili akili zenu ambazo Ni sawa na elasticity
 
Sheria ipi iliyovunjwa? Mbona mikutano na maandamano ya MACCM yanaruhusiwa na polisi lakini wakati huo huo vyama vya Wapinzani haviruhusiwi kukutana na kuandamana? Hebu twambie Zitto kavunja sheri ipi nchini? ilipitishwa lini bungeni sheria hii? Wabunge wa upinzani wamevunja sheria ipi Bungeni mpaka wafukuzwe ndani ya Bunge?

Hiyo kamati ya maadili Bungeni mbona haiwafukuzi Wabunge wa CCM (Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengineo) ambao wamekiuka maadili ya Bunge kwa kupokea rushwa toka kwa fisafdi Rugemarila? Au kupokea rushwa kwa Wabunge wa CCM ni mojawapo ya maadili yao yaliyotukuka? wabunge wa CCM wanaorusha matusi ya nguoni bungeni mbona hawajafukuzwa bungeni kwa kukiuka maadili ya Bunge? Au Wabunge wa CCM kurusha matusi ya nguoni Bungeni ni moja ya maadili yao yaliyotukuka ndani ya Bunge?

Acha kutetea wahuni na mafisadi wewe. Jitambue Tanzania ya 2016 haiwezi kuburuzwa kwa ubakaji wa demokrasi na sera za kukurupuka na kutegemea nchi ipate mafanikio.

Hivi wewe unajielewa kweli , uvunje sheria uachiwe kwa misingi ya demokrasia hivi unaijua demokrasia kweli ? Au unafikiri demokrasia Ni mikutano ya siasa , yaani hujui hata Uhuru ulionao wa kuandika humu Ni demokrasia , na kila ulifanyalo kwa Uhuru hujui Ni demokrasia , kutukana viongozi wa nchi na kuwaita majina ya kejeli hujui Ni demokrasia ?

Au umekaririshwa demokrasia Ni kupayuka kwenye majukwaa na kuvunja sheria , nyie ukawa sijui huwa mnawaza nini?
 
Sheria ipi iliyovunjwa? Mbona mikutano na maandamano ya MACCM yanaruhusiwa na polisi lakini wakati huo huo vyama vya Wapinzani haviruhusiwi kukutana na kuandamana? Hebu twambie Zitto kavunja sheri ipi nchini? ilipitishwa lini bungeni sheria hii? Wabunge wa upinzani wamevunja sheria ipi Bungeni mpaka wafukuzwe ndani ya Bunge?

Hiyo kamati ya maadili Bungeni mbona hawafukuzi Wabunge wa CCM (Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengineo) ambao wamekiuka maadili ya Bunge kwa kupokea rushwa toka kwa fisafdi Rugemarila? Au kupokea rushwa kwa Wabunge wa CCM ni mojawapo ya maadili yao yaliyotukuka? wabunge wa CCM wanaorusha matusi ya nguoni bungeni mbona hawajafukuzwa bungeni kwa kukiuka maadili ya Bunge? Au Wabunge wa CCM kurusha matusi ya nguoni Bungeni ni moja ya maadili yao yaliyotukuka ndani ya Bunge?

Acha kutetea wahuni na mafisadi wewe. Jitambue Tanzania ya 2016 haiwezi kuburuzwa kwa ubakaji wa demokrasi na sera za kukurupuka na kutegemea nchi ipate mafanikio.
Mkuu naona unarukaruka na kuhama mada kama vile unakwepa unachoulizwa kuhusu king wa ufisadi , jibu unalo sihitaji kusumbuka , pia kama unaamini demokrasia Ni mikutano ya hadhara , basi taasisi za kidini wanazijua sana demokrasia maana wao hufanya sana mihadhara na mikutano

Pia umehamia bungeni ambako naamini story nyingi wewe huzikuta hapa jf , pia lazima utambue bunge Ni mhimili na una kanuni zake na hubadilika kutokana na wakati wa bunge husika ,

Kwa kukutoa tongotongo tena Ni kuwa bunge likishapita na watuhumiwa baada ya uchaguz Mkuu na kupata wabunge wapya au walewale kwa uchaguz , kwa tamaduni za mabunge ya jumuiya ya madola , wanakuwa hawana hatia na wako huru hata kugombea na kuchaguliwa ,

Kuhusu wabunge wa ukawa kufukuzwa hilo Ni kanuni za bunge ambazo ndizo zimewatoa , nashangaa wewe unaenda kwa upepo na hizo kanuni wametunga wao , omba msaada upatiwe kitabu cha kanuni za bunge ili unapojibu hoja ujue unazungumza nini ?

Badilika usipelekwe na upepo , kuwa huru na huru itakuweka huru
 
Hivi nikimuita magufuli fisadi wa democracy nitakuwa nimekosea?
 
Hii hali inatuimanisha kuwa magufuli hakushinda uchaguzi wa Tz 2015 ndyo maana hajiamini coz anajua waliompa kura ni wachache sana so anahofu ya kwanini watu wapo kimya akidhan strike inaweza ibuka muda wowote. Anajitahdi kuhakikisha mikutano ya wapinzani isitokee mahali popote hata kama ni msiba naisi hata hili mmeisha jionea.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Endelea kuamini hivyo hasa katika jf ambayo story za vijiweni Ni nyingi kuliko uhalsia
 
Hakuna upepo wewe mpumbavu yote ninayoyaandika hapa yapo hadharani na Watanzania wote ambao ni wafuatiliaji wa mambo nchimi wanayaelewa.

Aliyekwambia demokrasi ni mikutano ya hadhara ni nani wewe k.i.laza? Acha kutaka kuweka maneno yale ambayo mimi sijawahi kuyaandika hapa.

Magufuli ni fisadi kakwapua nyumba za Serikali, kanunua boti liliooza na sasa hasira zake anatafuta watu wamshinikize CAG Assad eti ajiuzulu na wakati huo huo akipunguza bajeti yake kwa zaidi ya 50% kisa tu kaandika ripoti mbaya kuhusu ufisadi wa Magufuli.

Wewe mpumbavu kweli, hushangai hizo kanuni za Bunge zinawahusu Wabunge wa upinzani tu? Kwanini Wabunge wa CCM haziwahusu na wao kufukuzwa bungeni?

Unaonyesha jinsi ulivyo na uelewa finyu sana wa nini kinachoendelea nchini kuhusu ubakaji wa demokrasi nchini. Ni kwa taarifa yako Demokrasi ina maana pana sana na si tu mikutano au maandamano ya vyama vya Wapinzani tu.

Kwa akili yako fupi mimi kila kitu nakuta hapa JF, kweli una akili za kushikiwa wewe. Usijifanye unanijua wewe wakati huujui chochote kuhusu mimi.

Mkuu naona unarukaruka na kuhama mada kama vile unakwepa unachoulizwa kuhusu king wa ufisadi , jibu unalo sihitaji kusumbuka , pia kama unaamini demokrasia Ni mikutano ya hadhara , basi taasisi za kidini wanazijua sana demokrasia maana wao hufanya sana mihadhara na mikutano

Pia umehamia bungeni ambako naamini story nyingi wewe huzikuta hapa jf , pia lazima utambue bunge Ni mhimili na una kanuni zake na hubadilika kutokana na wakati wa bunge husika ,

Kwa kukutoa tongotongo tena Ni kuwa bunge likishapita na watuhumiwa baada ya uchaguz Mkuu na kupata wabunge wapya au walewale kwa uchaguz , kwa tamaduni za mabunge ya jumuiya ya madola , wanakuwa hawana hatia na wako huru hata kugombea na kuchaguliwa ,

Kuhusu wabunge wa ukawa kufukuzwa hilo Ni kanuni za bunge ambazo ndizo zimewatoa , nashangaa wewe unaenda kwa upepo na hizo kanuni wametunga wao , omba msaada upatiwe kitabu cha kanuni za bunge ili unapojibu hoja ujue unazungumza nini ?

Badilika usipelekwe na upepo , kuwa huru na huru itakuweka huru
 
Hakuna upepo wewe ******** yote ninayoyaandika hapa yapo hadharani na Watanzania wote ambao ni wafuatiliaji wa mambo nchimi wanayaelewa.

Aliyekwambia demokrasi ni mikutano ya hadhara ni nani wewe k.i.laza? Acha kutaka kuweka maneno yale ambayo mimi sijawahi kuyaandika hapa.

Magifuli ni fisadi kakwapua nyumba za Serikali, kanunua boto liliooza na sasa hasira zake anatafuta watu wamshinikize CAG Assad eti ajiuzulu na wakati huo huo akipiunguza bajeti yake kwa zaidi ya 50% kisa tu kaandika ripoti mbaya kuhufu ufisadi wa Magufuli.

Wewe ******** kweli, hushangai hizo kanuni za Bunge zinawahusu Wabunge wa upinzani tu? Kwanini Wabunge wa CCM haziwahusu na wao kufukuzwa bungeni.

Unaonyesha jinsi ulivyo na uelwa finyu sana wa nini kinachoendelea nchini kuhusu ubakaji wa demokeasia nchini. Ni kwa taarifa yako Demokrasi ina maana pana sana na si tu mikutano au maandamano ya vyama vya Wapinzani.

Kwa akili yako fupi mimi kila kitu nakuta hapa JF, kweli una akili za kushikiwa wewe. Usijifanye unanijua wewe wakati huujui chochote kuhusu mimi.
Usitoke povu , maana naona mpaka umeanza kutukana kama kawaida yenu

Nyumba Za serikali
Hili nalo unahitaji uelimishwe au umetoka nyamilolelwa juzi , hili alilijibu vizuri kada mwenzako ,Mr Zero ( sumaye) wakati anatangaza nia ya urais pale regency hotel na aliulizwa swali hilo akalijibu vizuri , huyo kwa sasa Ni mjumbe wa kamati kuu chadema na kabla ya hapo alikuwa Waziri Mkuu wakati nyumba zinauzwa na kukuongeze a , MZEE mkapa juzi kwenye kigoda cha Mwalimu alikiri alikosea kuuza nyumba za serikali na ubinafsishaji , hivyo usiwe na akili ya 0.2 KB kujua nani alikuwa muhusika na nani aliambiwa atekeleze baada ya baraza la mawaziri kuridhia na kumbuka fisadi papa , lowasa naye alikuwa Waziri

Kitu ambacho huelewi Ni kuwa unawaongelea viongozi wa CCM waliokimbilia chadema kwa sababu ya ulafi wa madaralka ,alafu hao ndio walikataa katiba ambayo Leo ingekuwa muarobaini kwa sababu waliogopa ikipita na wao wana ndoto za urais itawabana Leo ndio viongozi wako , shwain!

Tanua akili usitanue vidole vya kati
 
Msome hapa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salvatory Rweyemamu kuhusu ukwapuzi wa nyumba uliofanywa na fisadi Magufuli. Na huyu si wa kutoka upinzani bali ni kada wa MACCM.

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI

Msome hapa CAG kuhusu ufisadi wa Magufuli wizara ya ujenzi, na ripoti hii na zile mbili za ukwapuzi wa nyumba na ununuzi wa boti lililooza kwa bilioni 8 ndiyo visasi vya Magufuli kumpiga vita huyu CAG Assad eti ajiuzulu na pia kukata bajeti ya taasisi yake kwa zaidi ya 50% Acha kukurupuka wewe kutetea mafisadi na wabaka demokrasi nchini.

By Ibrahim Yamola, Mwananchi
In Summary

Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Dar es Salaam. Machungu ya Watanzania yakiwa hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya wizara ya ujenzi.

Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Kutokana na ufisadi huo, habari zilizolifikia Mwananchi zinasema CAG amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa wizara ya ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi katika bajeti kwa jamii na wahisani.

“Wizara (ya ujenzi) ililidanganya Bunge kuwa kuna ujenzi wa barabara hizo wakati wakijua kwamba walikusudia kulipa madeni ya wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara...mpango mkakati wa wakala wa barabara wa mwaka wa fedha 2011/12 pamoja na manunuzi ulioidhinishwa havikuonyesha utekelezaji wa mradi huo,” chanzo cha habari kilikariri ripoti ya CAG.

Matumizi hayo yasiyo sahihi yaliibuliwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Novemba 22, 2013 baada ya kutilia shaka kiasi hicho cha fedha na ofisi ya CAG kuagizwa kufanya ukaguzi.

Katika kikao hicho ambacho wizara ya ujenzi iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake wa wakati huo, Balozi Herbert Mrango alihojiwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa CAG mwaka 2011/12.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo Sh348.1 bilioni zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililokuwa limetajwa kuwa ni la mradi maalumu hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo (ilikuwa Novemba 22 mwaka 2013) uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975 bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto.

Alisema katika majumuisho ya bajeti wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Harrison Makyembe aliyekuwa Naibu waziri wa wakati huo aliyekuwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha hizo.

Zitto alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara.”

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Makyembe ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifafanua majumuisho.

“Hizi ni fedha kwa ajili ya Counterpart fund,” alimkariri Lukuvi ambaye sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa ripoti ya CAG imeeleza kuwa, “Katika kikao cha kuanza ukaguzi huo Aprili 3, mwaka jana uongozi wa wizara ulithibitisha kwamba hakukuwa na barabara mpya bali walifanya hivyo baada ya kuona madeni yamekuwa makubwa kiasi cha Sh420 bilioni kama yalivyokuwa kwenye hesabu za wakala wa barabara za mwaka wa fedha 2010/11.”

Katika ukaguzi huo imebainishwa kuwa Sh3 bilioni hazikujulikana matumizi yake.

Taarifa zaidi zinasema baada ya wizara kupeleka fedha kwa wakala wa barabara, fedha hizo zilifanyiwa mchakato wa kuzigawa upya lakini nyaraka halisi zilizotumika kugawa fedha hizo hazikuwasilishwa kwa ukaguzi.

“Hata hivyo, kati ya Sh175.3 bilioni zilizopitia kwenye akaunti ya maendeleo ya wakala wa barabara, kiasi cha Sh3,048,365,229 hakikuweza kupatiwa maelezo jinsi kilivyotumika.

“Pia, kati ya malipo ya Sh77.7 bilioni yaliyofanyika kwa wakandarasi au washauri wa barabara moja kwa moja kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Novemba 30, mwaka 2011 kupitia barua ya kumbukumbu namba GA.65/263/01/VOL.XI Gavana Mkuu wa BoT, alikanusha kulipa asilimia 30 ya fedha hizo Sh30.6 bilioni.

“Gavana wa BoT amekanusha kulipa Sh30.6 bilioni kwa kampuni ya M/S Strabag Internationl Gmbn na M/S China-Engineering Corporation Co, kati ya Sh77.7 ambacho kilipelekwa BoT kwa ajili ya malipo kwa wakandarasi au washauri mbalimbali,” alifafanua zaidi mtoa habari hizi na kuongeza:

“Ukaguzi maalumu umeshindwa kuthibitisha malipo yenye jumla ya Sh47.1 bilioni sawa na asilimia 61 kama yalilipwa kwa walengwa waliokusudiwa kwa sababu Gavana wa BoT amesema kuwa kisheria hatakiwi kutoa taarifa za wateja.”

Pia, habari za ndani kutoka ofisi ya CAG zinadai kuwa, Sh13.4 bilioni za ujenzi wa barabara za mikoa zilitumika kulipia barabara binafsi na za halmashauri za wilaya ambazo hutengewa fedha kupitia mfuko wa barabara kinyume na makusudio yaliyopitishwa na Bunge.

“Pia, nimebaini kwamba baadhi ya miradi haikuwamo kwenye kasma zilizopitishwa na Bunge kwenye makisio ya mwaka wa fedha 2010/11 na miradi mingine ilitengewa fedha kidogo lakini wakala wa barabara alitumia fedha nyingi kulipia miradi hiyo bila kuonyesha jinsi alivyozipata,” chanzo cha habari kimekariri ripoti ya CAG.

Katika ukaguzi huo, ufisadi mwingine wa Sh36.6 bilioni ambazo ni malipo ambayo hayakutolewa taarifa kwenye ripoti za washauri au wakandarasi, jambo linaweza kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa wakandarasi kuidai Serikali zaidi ya mara moja na kuitia Serikali hasara.

Mtoa habari wetu alisema kuwa Sh6.2 bilioni zilitumika kuwalipa wakandarasi ambao hawakuonyeshwa katika orodha ya madeni yaliyowasilishwa bungeni pamoja na malipo ya Sh6.6 bilioni yaliyokwishalipwa yaliombewa tena.

“Madeni hayo yalikuwa yamelipwa na wakala wa barabara katika mikoa husika. Hali hii inaashiria kwamba kwa hati ya madai moja kuna uwezekano wa mkandarasi kulipwa mara mbili au zaidi.

Katika mapendekezo ya jumla, chanzo chetu kimesema ofisi ya CAG imeishauri Serikali kusimamisha kuingia mikataba mipya ya ujenzi wa barabara na ilipe madeni ya wakandarasi yaliyopo kwa sasa ili kuepuka ukuaji wa deni hilo kwa siku za baadaye na kuwa mzigo kwa Taifa na wananchi.

“Serikali ihakikishe inaheshimu mikataba iliyowekwa kati yake na wakandarasi ili kuepuka malipo yenye riba na kushtakiwa na wakandarasi kutokana na kuvunja masharti yaliyowekwa kwenye mikataba,” kilifafanua chanzo chetu na kuongeza:

“Zabuni za ujenzi wa barabara mpya ziendane na fedha zilizotengwa katika mwaka wa fedha husika kama itakavyokuwa imeainishwa katika mpango wa manunuzi wa mwaka huo.”

Ukaguzi huo maalumu uliohusisha miradi 46 ya ujenzi wa barabara kuu na barabara za mikoa ambazo wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara walitoa huduma kwa wakala wa barabara.

“Mbali na miradi hii 46, miradi yote ya wakala wa barabara ilikuwa imezalisha madeni ya jumla ya Sh420 bilioni kama yalivyo kwenye hesabu za wizara kufikia mwaka wa fedha 2010/11,” kilieleza chanzo chetu.

Sakata hili limeibuka wakati lile la uchotwaji wa fedha za Akautni ya Tegeta Escrow halijapoa na hadi sasa limesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri kufuatia kumfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka huku Profesa Sospeter Muhongo alitangaza kuachia wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini.

Mbali na hao, pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alitangaza kujiuzuru huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi wa sakata hilo.

Katika mlolongo wa hatua za kinidhamu kuchukuliwa, baadhi ya watumishi wa umma wamefikishwa mahakamani na wengine mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Usitoke povu , maana naona mpaka umeanza kutukana kama kawaida yenu

Nyumba Za serikali
Hili nalo unahitaji uelimishwe au umetoka nyamilolelwa juzi , hili alilijibu vizuri kada mwenzako ,Mr Zero ( sumaye) wakati anatangaza nia ya urais pale regency hotel na aliulizwa swali hilo akalijibu vizuri , huyo kwa sasa Ni mjumbe wa kamati kuu chadema na kabla ya hapo alikuwa Waziri Mkuu wakati nyumba zinauzwa na kukuongeze a , MZEE mkapa juzi kwenye kigoda cha Mwalimu alikiri alikosea kuuza nyumba za serikali na ubinafsishaji , hivyo usiwe na akili ya 0.2 KB kujua nani alikuwa muhusika na nani aliambiwa atekeleze baada ya baraza la mawaziri kuridhia na kumbuka fisadi papa , lowasa naye alikuwa Waziri

Kitu ambacho huelewi Ni kuwa unawaongelea viongozi wa CCM waliokimbilia chadema kwa sababu ya ulafi wa madaralka ,alafu hao ndio walikataa katiba ambayo Leo ingekuwa muarobaini kwa sababu waliogopa ikipita na wao wana ndoto za urais itawabana Leo ndio viongozi wako , shwain!

Tanua akili usitanue vidole vya kati
 
Kupinga ufisadi unamsaidia mnyonge kama ilivyo kwa kujenga demokrasia. Sasa utamsaidiaje mnyonge kwa kupigana na ufisadi huku umemkandamiza labda kama zana ya demokrasia haijaeleweka. Unampa chakula kizuri huyo mnyonge huku akiwa na minyororo miguuni na kunfungia kwenye chumba ambacho hakina madirisha halafu unatoka na kutamba kwamba unauchungu na mnyonge na unampigania, utampigania vp wakati umemfunga minyororo miguuni. Vita vya ufisadi na demokrasia ni kama betrii na gari vinaenda pamoja. Kusukuma gari kila wakati ili kuliwasha ni kazi ngumu.
 
Wewe ni sawa na yule aliyesema kuwa hana haja ya kudoma uzi wa ZZK; ye yuko na JPJM. kuna siku utakuja kuuliza eti zzk alisema nini siku ile!!!! We endelea na mtakatifu wako.

Wewe endelea na shetani wako
 
Hili somo halitaeleweka kwa mtu ambaye ni low IQ ,kuna uhusiano mkubwa sana wa demokrasia na maendeleo - Human centred development and democracy ,we kama huamini pima matokeo ya one party system and military rule Africa kwa zaidi ya miongo 3 ,unajua Africa iliishia wapi?vipi kule Nazi ,Latin countries na East Asia?
Ndo maana Generali ulimwengu akasema tunarudishwa nyuma miaka 50 ya Uhuru,Democracy principally is about participation in decision making and Emancipation from oppression ,suppression ,humiliation ,poverty etc
 
Msome hapa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salvatory Rweyemamu kuhusu ukwapuzi wa nyumba uliofanywa na fisadi Magufuli. Na huyu si wa kutoka upinzani bali ni kada wa MACCM.

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
Akili yako ina walakini na hujui historia , salva rweyemamu mwandishi aliyekuwa raia mwema waliompiga rais Magufuli kwenye magazeti kwa kuhofia akichukua fomu atakuwa tishio huyu mwana mtandao aliyepewa fungu na lowasa na rafikiye Jk kipindi hiko , ndio unamtumia kama rejea hakika kapimwe akili , huijui nchi hii nishakwambia acha kurukaruka

Suala la nyumba ,muulize mbatia,mboe, na fuata upepo wa chadema na ukimaliza muulize sumaye atamalizia jibu lako, waandishi njaaa wasikusumbue ambao hutumia kalamu zao kuandika kutokana na uzito wa bahasha ya kaki

#Hapa Kazi Tu
 
ufisadi upi alioufia magufuli? labda watumishi hewa....kwingine kote sijaona kitu...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Very true, it is very difficult for people with low IQ to comprehend the relationship between lack of democracy and development.

Hili somo halitaeleweka kwa mtu ambaye ni low IQ ,kuna uhusiano mkubwa sana wa demokrasia na maendeleo - Human centred development and democracy ,we kama huamini pima matokeo ya one party system and military rule Africa kwa zaidi ya miongo 3 ,unajua Africa iliishia wapi?vipi kule Nazi ,Latin countries na East Asia?
Ndo maana Generali ulimwengu akasema tunarudishwa nyuma miaka 50 ya Uhuru,Democracy principally is about participation in decision making and Emancipation from oppression ,suppression ,humiliation ,poverty etc
 
Mnafiki tu huyu Mkuu, kelele za kujinadi kuhusu kupambana na mafisadi nyingi sana tukija kwenye utendaji halisi ni SIFURI.

ufisadi upi alioufia magufuli? labda watumishi hewa....kwingine kote sijaona kitu...
 
Back
Top Bottom