Sasa hapo ndo kapangua nini? Pamoja na hiyo unayosema kapangua, bado kuna tatizo la foleni mjni Dar es Salaam. Tufikie mahali watanzania tuache ushabiki maana siasa haitatufikisha popote. Magufuli kuna mazuri anafanya. Ila Tatizo la nchi yetu huwa hatufikirii miaka mia moja (100) ijayo. Kwa mfano ni kwa nini kusiwe na mpango kabambe angalau miaka mia ijayo kwa mji wa Dar es Salaam ambao utahusisha usafiri wa train za umeme kwa maana ya underground, trum, na mabasi kama hayo ya DART? Hii ni pamoja na kuainisha miundo mbinu hiyo mapema ili baadaye kusiwe na gharama kubwa kuja kuijenga na kufidia watu. Bado tuna mawazo mafupi kama ndengu!!!! Dar es Salaam bado ni kakijiji fulani ambako kamejipa hadhi ya jiji. Hakuna chochote hapo ni uchafu na miundo mbinu isiyo na kiwango. Watu wanajenga ovyo tu, maji ni shida, barabara hata za vumbi zimetushinda, watu wengi masikini na serikali haioni shida angalau kuja na ramani mpya ya jiji ambayo utekelezaji wake hautajali nani ataongoza serikali. Wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? Kama gharama ni lami kwa nini tusianze hata kwa barabara za vumbi. Watu wapangwe vizuri nawenye kufidiwa wafidiwe ili jiji lipangwe vizuri!!! Acheni siasa na mtembee miji ya wenzetu muone.