Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, namsikiliza kupitia TBC1. Hakika Magufuli amejibu kikamilifu hoja zote za wabunge na kila mmoja ametulia na kuridhika majibu haya. Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga itakamilika ndani ya miezi miwili ijayo baada ya Kuwait Fund kutoa bilioni 16 ambazo zitatosha kwa ajili ya kazi hiyo.
Pia amesema kuwa hakuna mgogoro wa kusimamia sheria baina yake na Waziri Mkuu na ndo maana wanaenda kuimarisha mizani nchini. Pia ameeleza hatua zinazochukuliwa kupunguza msongamano Jijini Dar es Salaam na amesema kuwa jiji hilo halipo miongoni mwa majini yenye msongamano mkubwa wa Magari Duniani. Amesema Wakala wa Barabara vijijini utaanzishwa kupitia TAMISEMI.
Amewatahadhalisha wabunge kuwa kuwa ujenzi wa barabara si sawa na kupika chapati au maandazi. Una stage zake ambazo ni sehemu ya ujenzi. Amesema kuwa Korea ya Kusini ambao wamejenga daraja la Mkapa ndio watakaojenga daraja la Sealander.
Barabara zenye urefu wa Kilometa 86 ambazo zilikuwa za Manispaa jijini Dar es Salaam zimechukuliwa na TANROADS ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.