Pia Mhe JPM anaangalia maisha katika mitazamo ya ukinzani badala ya ukamilishano. Huu nao ni mtazamo hasi unaoweza kuwa kikwazo katika kuleta maendeleo. Kwa mfano, katika ziara yake ya juzi mikoani Iringa na Morogoro amedhihirisha udhaifu huu kwa kutoa kauli zinazohimiza ukinzani badala ya ukamilishano: Kiswahili vs. Kiingereza (badala ya Kiswahili na Kiingereza), shule za binafsi vs. shule za umma (badala ya shule za binafsi na shule za umma), mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi waliosoma shule za binafsi vs. waliosoma shule za umma (badala ya waliosoma za binafsi na waliosoma za umma), maendeleo ya ukanda wa kusini vs. maendeleo ya ukanda wa kaskazini (badala ya maendeleo ya ukanda wa kaskazi na maendeleo ya ukanda wa kusi). Mtazamo huu ndio unaomsukuma kuangalia chama tawala vs vyama vya upinzani (badala ya chama tawala na vyama vya upinzani). Maendeleo kwa kasi ya JPM hayawezi kuja kwa mitazamo ya ukinzani bali ya ukamilishano.
asanteBonge la observation. Nimependa ukinzani uliouonesha hapo. Ukweli mtupu
MTU anaejua kila kitu utampa sapoti ipi,Mkuu una mwandikia Autobiography JPM?
Kuna sehemu anapatia na kama binadamu kuna sehemu anakosea.
Tumpe sapoti pale anapopatia basi!
Lakini asidanganye kuwa anatumia fedha za ndani! Hivi sasa anahaha huku na kule kutafuta mikopo ambayo nina wasiwasi kama atapata!!!SGR, Stieglers Gorge, Bomba la Mafuta na mengine, ni kati ya mambo yakimalizika tutamkumbuka Magufuli.
Nguvu sio tija watu wamebaki wanamuangalia tu,Pale mheshimiwa anapotumianguvu( pysical) kuongoza badala ya akili( intelligence).
Ushauri mzuri lakin kwakua yeye anajiita jiwe na sifa za jiwe mnazifaham mojawapo jiwe halisikii nyingine halishauliki, unapoongea na jiwe watu watakuona umevamiwa na wazimu inakuwaje unaongea na jiwe, lakini tusikate tamaa yawezekana ipo siku likasikia na kupokea ushauri.Falsafa ya uongozi nyepesi kabisa: kiongozi anayefikiria nguvu ni suluhisho la kuleta ufanisi ni dhaifu. Kiongozi mzuri ni yule anayeunganisha watu kumfanyia kazi.
Mkulu kweli katengeneza maadui wengi na kwa wazi kabisa angalia ulinzi wake kwa sasa. Tulikuwa tunayaona huko nje ambako nchi hizo zinazo ongozwa kiimla lakini sasa tunayaona hapa. Akihutubu hadhara nusu ya watu hao ni walinzi wake! Najua sasa anaanza kubadilika kujaribu kutafuta marafiki, lakini kama ilivyo kwa mteja ukishampoteza ni ngumu kumrejesha.
Kitu kingine kinachoiangusha serikali yangu ni uongo. Wengine wanauita propoganda. Nakubali Serikali zote duniani zina propoganda ya aina fulani lakini inapogeuka kuwa uongo wa wazi unatengeneza kutoaminika. Mambo ya wazi unapoyatetea kuyafanya yawe 'kweli' wakati watu wanajua ni kinyume chake unawajengea usugu wa kukuamini.
Rais wangu waache wataalamu wafanye kazi bila wewe kuwalalamikia hadharani kila wakati. Hawa watakugeuka na utakosa support. Tanzania hatujafika mahali kuwa kama mtaalamu huyu anakosea fukuza uweke mwingine. Hawako wengi kiasi hicho.
Mwisho ni vizuri Rais ukapunguza hotuba zako ili watu wawe na hamu ya kukusikiliza utakapotoa hotuba. Bahati mbaya hotuba zako zinarudia yale yale na zina maudhui ya kulalamika, kutisha, kujisifu na kukujeli. Badilisha hili na uwe Rais wa kuunganisha, kumotisha na kuonesha maono ya maendeleo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mambo sasa atang'ata meno [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] ila tu atashindwa kukufikiaMambosasa atuache tumseme Pombe wetu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli kabisa kama mimi namuangalia tu nasema hiiiiiiiiiNguvu sio tija watu wamebaki wanamuangalia tu,
hapo sasaAnapokosea je! Tufanye nini??
Never!Kweli kabisa,ikiwa washauri wake wanaogopa kushauri au wanapuuzwa basi anguko lake halipo mbali inaweza kuwa 2020,kama tukijaaliwa kushikamana kiukweli.
Daaah ila huyu Rais.... yani Rais kushindwa kujua siasa za dunia ni aibu kubwaMaso! siasa za kiafrica zimejaa ghirba na unafiki! Mimi si mnafiki the guy is out of tune! I doubt if he knows what he is doing!
I started doubting him the day he utterer something odd! " Saddam was a Libyan president oooh no a quwait president! wasingekuwa akina sisi he would have been out Tayari!
Ha ha ha!Maso! siasa za kiafrica zimejaa ghirba na unafiki! Mimi si mnafiki the guy is out of tune! I doubt if he knows what he is doing!
I started doubting him the day he utterer something odd! " Saddam was a Libyan president oooh no a quwait president! wasingekuwa akina sisi he would have been out Tayari!