Magufuli ana hali mbaya sana ya kisiasa tunapoelekea mwaka 2020. Ametumia nguvu nyingi kudhibiti vyama vya upinzani, bila kujua, kupambana na upinzani

Anaandika Dr.Christopher Cyrilo
Magufuli ana hali mbaya sana ya kisiasa tunapoelekea mwaka 2020. Ametumia nguvu nyingi kudhibiti vyama vya upinzani, bila kujua, kupambana na upinzani ndio kuiongezea nguvu. hakujua ndani ya chama chake kuna upinzani mkubwa zaidi dhidi yake.
Tayari makundi ya urais yameanza kujengwa ndani ya CCM, machache yenye nguvu. Wengine wapo ndani ya serikali na wanampa ushirikiano wote, wanasubiri wakati muafaka wampe 'surprise'.

Muda uliobaki ni mchache. Wakubwa waliompigania hadi kupata nafasi ya kugombea Urais, amewakorofisha.

Vijana waliompigania, hadi kupelekea Jaji Lubuva kutangaza kura za uongo ili Magufuli awe Rais, amewakorofisha.

Tayari kuna jitihada za kudunisha/kupunguza hadhi ya Magufuli. Suala la upotevu wa Trilioni 1.5 litaibuliwa upya. Na hili ni kaa la moto kwa Magufuli. Baadhi ya viongozi wa chama na serikali wataanza kutoa kauli zinazodunisha hadhi ya serikali, na kumpunguzia Magufuli Umaarufu.

Sasa amebaki na wasaka tonge, wasio na uzoefu kwenye masuala ya siasa, wala mbinu za ushindi. Na baadhi ya wasomi anaowapa mlo, wameanza kumtafutia majukwaa ya kumnadi kwa wananchi, mfano ni Kongamano la kumsifia lilopangwa kufanyika katika chuo cha Dsm.

Anachoweza Magufuli sasa ni kutumia vyombo vya dola ili abaki madarakani, na safari hii, vyombo vya dola vinaweza kutumika dhidi ya CCM yenyewe. Tutarajie misiba mingi ya wanasiasa kuliko ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2015.

Ikumbukwe kuwa, Magufuli alikuwa mtu mdogo ndani ya CCM kabla ya kuwa Rais. Na hata baada ya kuwa M/kiti bado kuna mambo mengi hayafahamu ndani ya chama chao.Hadi leo bado anajifunza.

Salama yake ni vyombo vya dola. Atahitaji kukubali mambo yajiendee yenyewe au atumie mabavu ili kujihakikishia nafasi ya Urais wa awamu nyingine.

Chadema ina kazi kubwa moja, tunasema "Adui yako akiwa anakosea usimstue". Tunawaachia watoane damu, waangushane wenyewe, halafu atakapobaki mmoja wao, tunakula kichwa kiulaiani.
Lubuva alitangaza kura za uongo means magufuri hakushinda, sasa hao wenye utaalamu wa siasa walisaidia nini? Maana washindwa kumshindisha means hata 2020 watashindwa pia.

Acha wasiojua siasa nao wajaribu pengine lubuva akatangaza matokeo ya ukweli.
 
;) dalili zipo wazi ukiona baadhi ya maeneo nati zinalegezwa ujue hali ni tete! ...kelekea 2020 unaweza uza chupi za mitumba hata kwenye Geti la TBS,au unamwaga sagulasagula za mashati mlangoni kwa RC,alimuradi unakitambulisho! Afu kama kuna fursa ya kulima kwenye kingo za mto we piga kazi lile zuio halipo tena hadi 2022!
Wameanza kulegeza shetani kavaa joho la malaika,greda za bomoabomoa zimeenda service, ruksa kujenga hadi mitoni barabarani,machinga huru popote, wafugaji mifugo bure kuogesha,kikokotoo kiko likizo,hizi rasharasha si ajabu Nape kupewa uwaziri asaidie bao,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Dr.Christopher Cyrilo
Magufuli ana hali mbaya sana ya kisiasa tunapoelekea mwaka 2020. Ametumia nguvu nyingi kudhibiti vyama vya upinzani, bila kujua, kupambana na upinzani ndio kuiongezea nguvu. hakujua ndani ya chama chake kuna upinzani mkubwa zaidi dhidi yake.
Tayari makundi ya urais yameanza kujengwa ndani ya CCM, machache yenye nguvu. Wengine wapo ndani ya serikali na wanampa ushirikiano wote, wanasubiri wakati muafaka wampe 'surprise'.

Muda uliobaki ni mchache. Wakubwa waliompigania hadi kupata nafasi ya kugombea Urais, amewakorofisha.

Vijana waliompigania, hadi kupelekea Jaji Lubuva kutangaza kura za uongo ili Magufuli awe Rais, amewakorofisha.

Tayari kuna jitihada za kudunisha/kupunguza hadhi ya Magufuli. Suala la upotevu wa Trilioni 1.5 litaibuliwa upya. Na hili ni kaa la moto kwa Magufuli. Baadhi ya viongozi wa chama na serikali wataanza kutoa kauli zinazodunisha hadhi ya serikali, na kumpunguzia Magufuli Umaarufu.

Sasa amebaki na wasaka tonge, wasio na uzoefu kwenye masuala ya siasa, wala mbinu za ushindi. Na baadhi ya wasomi anaowapa mlo, wameanza kumtafutia majukwaa ya kumnadi kwa wananchi, mfano ni Kongamano la kumsifia lilopangwa kufanyika katika chuo cha Dsm.

Anachoweza Magufuli sasa ni kutumia vyombo vya dola ili abaki madarakani, na safari hii, vyombo vya dola vinaweza kutumika dhidi ya CCM yenyewe. Tutarajie misiba mingi ya wanasiasa kuliko ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2015.

Ikumbukwe kuwa, Magufuli alikuwa mtu mdogo ndani ya CCM kabla ya kuwa Rais. Na hata baada ya kuwa M/kiti bado kuna mambo mengi hayafahamu ndani ya chama chao.Hadi leo bado anajifunza.

Salama yake ni vyombo vya dola. Atahitaji kukubali mambo yajiendee yenyewe au atumie mabavu ili kujihakikishia nafasi ya Urais wa awamu nyingine.

Chadema ina kazi kubwa moja, tunasema "Adui yako akiwa anakosea usimstue". Tunawaachia watoane damu, waangushane wenyewe, halafu atakapobaki mmoja wao, tunakula kichwa kiulaiani.
AISEE UMEANDIKA MASIALA MASIALA ILA HUO NDIYO UKWELI MTUPU!!!!!!!!!!!!
JIWE SIKU ZAKE ZINA HESABIKA.
 
Back
Top Bottom