Alikosea kwa kuamini kuwa angeweza kuumaliza upinzani kwa kutumia Vyombo vya Dola badala ya kutumia nguvu ya hoja

Status
Not open for further replies.

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Rais Magufuli alianza kutekeleza azma yake hiyo kwa kutangaza hadharani kule Singida, katika sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa chama chake cha CCM, hapo Februari 5, mwaka 2016, kuwa ndani ya utawala wake, atahakikisha vyama vya upinzani vinakufa ifikapo mwaka huu wa 2020!

Utekelezaji wa azma yake hii, ambayo ipo kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977, ibara ya 3(1) ambayo inasema wazi kuwa nchi yetu itaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi ambayo aliapa kuilinda Katiba hiyo, kabla ya kukabidjiwa madaraka hayo ya kuongoza nchi hii, ulianza mara tu alipoanza kutekekeza majukumu yake ya kuongoza nchi hii.

Alianza kwa kufungia kuonekana kwa Bunge mubashara, kwa kisingizio cha wananchi wanapaswa kufanya kazi kipindi hicho cha kuonyesha Live vipindi hivyo vya Bunge, wakati alikuwa yeye mwenyewe akionekana mubashara katika matukio mbalimbali akiyokuwa akiyafanya yeye, wakati huo huo ambao alisema wananchi wanapaswa wafanye kazi badala ya kuangalia Live, televisheni zao!

Akaja na kuwazuia wapinzani wasifanye mikutano yoyote ya kisiasa, hata ile ya ndani, wakati akiruhusu chama chake cha CCM, kikiendelea kufanya mikutano mbalimbali kadri kitakavyo nchi nzima!

Akaleta sheria Bungeni kwa hati ya dharula zenye lengo la "kuviua" kabisa vyama vya upinzani, ili azma yake ya kuvimaliza litilmie kabla ya mwaka 2020, zikiwemo sheria ya maudhui ya Vyombo vya Habari na ile sheria ya mitandaoni, ambapo tulishuhudia katika kipindi hicho, ndipo magazeti makini ya kuleta Mageuzi nchini, yakifa, yakiwemo magazeti makini ya Mwanahalisi na Tanzania Daima, yakiuawa kabisa.

Hata hivyo umefika mwaka huu wa 2020 wa Uchaguzi umefika, bila azma na ndoto yake ya kuumaliza kabisa upinzani nchini kutimia, ndipo hapo anakuta wananchi wakiwa na hamu mno ya kumsikiliza mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, Tundu Lissu, ambaye naye alipitia madhara makubwa ya kupona kimuujiza wa Mungu wetu, katika lile jaribio la kushambuliwa kwa risasi 16 zilizomwingia mwilini mwake, katika jaribio la kumwua, lililofanyika hapo September 7 mwaka 2017.

Tunapata fundisho gani kwa hali hii inayotokea nchini kwetu hivi sasa?

Fundisho tunalolipata hapa ni kuwa mtawala yeyote ambaye unapewa dhamana ya kiongozi nchi hii, ubapaswa uwe mnyenyekevu, ambaye unapaswa uitii Katiba ya nchi ambayo unaapa kuitii na kuiheshimu kabla hujakabidhiwa madaraka hayo ya kuongoza nchi hii.

Kinachotokea hivi sasa ni kama watawala wetu hawaamini kinachotokea nchini kote, ambalo mwamko ni mkubwa mno, ambapo wananchi kwa mamilioni wamepania kutoipigia kura CCM, ifikapo hapo Oktoba 28, siku ambayo ndiyo itakuwa ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alichosahau Rais wetu ni kuwa kwenye siasa, silaha kubwa inayotumika ni nguvu ya kushawishi kwa nguvu ya hoja, ili chama pinzani kiishiwe hoja na hivyo chama hicho kijikute kinakumbana na "natural death"

Lakini kwa kutumia nguvu za dola kuvimaliza vyama vya upinzani nchini ni kujidanganya kuoita kiasi na kwa yanayotokea hapa bchini hivi sasa ni ushahidi tosha ambapo linatakiwa liwe fundisho kwa watawala weti kutothubutu kufanya hiyo "political gambling" tena maishani!
 
Kila mwaka huwa siend kupiga kula ila mwaka huu napiga kumuonesha jiwe kwamba upinzani upo vizuri Leo kuliko janaaa.....🤞
Yeye aliamini kwa kuwanunua wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani atakuwa ameumaliza upinzani nchini, kumbe ndiyo kwanza ameuongezea nguvu maradufu!

Kila mwenye haki ya kupiga kura mwaka huu, aende kupiga kura mwaka huu, ili kuudihirishia ulimwengu kuwa upinzani nchini ni "strongest ever"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom