Magufuli amvimbia Waziri Mkuu Pinda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]








Dkt.+Magufuli.JPG


Dkt. Magufuli:

Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizindua Kituo kipya cha Mabasi madogo ya abiria, eneo la Mbezi Mwisho, Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka (kulia) ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Harbert Murango, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki. Yusuph Mwenda na Mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika. (Picha na Prona Mumwi)


*Aagiza bomoabomoa ndani ya siku tano
*Ashangiliwa, aambiwa anafaa kuwa rais
Na Goodluck Hongo
WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, amempa muda wa siku tano Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) awe amebomoa nyumba zote zilizojengwa maeneo ya Hifadhi za Barabara hata kama yana bendera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa utekelezaji wa sheria haujali chama.

Dkt. Magufuli alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana waakati akifungua kituo kipya cha mabasi kilichopo Mbezi Mwisho.

“Kutokujua sheria si utetezi, kama mnataka upana wa barabara uwe rula, basi twendeni bungeni tukapitishe sheria hiyo na kila moja wetu aizingatie,” alisema Dkt. Magufuli akishangiliwa na wananchi waliokuwa katika uzinduzi huo na kusema “Uwe rais...uwe rais...uwe rais.”

Kauli ya Dkt. Magufuli inaonekana kupingana vikali na ile ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliyoitoa Machi 6,2011 alipomtaka Waziri huyo kusimamisha bomoabomoa katika Hifadhi za Barabara nchi nzima hadi itakapoamuliwa na Baraza la Mawaziri.

“Rais aliona kwenye sekta ya barabara pana legalega na kumrudisha Dkt. Magufuli kwenye Wizara hii, lakini ameanza kwa spidi kubwa hivyo tumeemwagiza asimamishe oparesheni hii hadi suala hili litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri,” alisema Pinda na kuongeza kuwa, kasi hiyo imeitisha Serikali.

Jana Dkt. Magufuli alisisitiza kuwa, lengo la hatua hiyo ni kuondoa msongamano wa magari unasababishwa na watu kutofuata sheria na kujenga majengo katika maeneo ya Hifadhi za Barabara na kufanya biashara viongozi wakiangalia.

Aliongeza kuwa, hali hiyo inasababisha Serikali kulipa fidia wakati watu wanaovunja sheria husika wakiachwa.

“Nakuagiza Mkurugenzi wa TANROADS, nakupa siku tano kuanzia leo kuvunja vitu vyote hata ikiwa bendera za CCM kwani sheria haina chama, viongozi acheni siasa bali simamieni sheria na bila kufanya hivi, hata wakiletwa malaika nao watakwama kwenye foleni,” alisema Dkt. Magufuli

Alisema Serikali ipo pamoja na wananchi wake kuhakikisha miundombinu inategenezwa ambapo katika mikoa mbalimbali nchini kuna miradi ya barabara ambapo zaidi ya sh. bilioni 240.6 zitatumika kujenga barabara kuanzia Kimara hadi Posta.

Aliongeza kuwa, barabara hiyo itakuwa na vituo vya mabasi 29 kati ya hivyo vitano vitakuwa vituo vikuu na kusisitiza kuwa, marufuku kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutumia pesa za Mfuko wa Barabara kulipana posho na kuacha kutengeneza barabara.

“Mkurugenzi wa TANROADS fuatilia fedha zote wanazopewa Wakurugenzi na kama watatumia vinginevyo, nipeni majina yao niyapeleke kwa Rais Jakaya Kikwete awafukuze kazi,” alisema.


Alitolea mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Longido kuwa ndizo zimetumia vibaya fedha za mfuko wa barabara.

Ili kupunguza msongamano katika barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze mkoani Pwani, Dkt. Magufuli alisema itapanuliwa hivyo aliwataka wenye nyumba zilizopo katika Hifadhi ya Barabara zibomolewe vinginevyo atazivunja kwa kuwa yeye ndiye msimamizi wa TANROADS.

Alipiga marufuku barabarani kuwekwa matuta akisema sheria haziruhusu kwani magari yanaweza kuharibika wakaidai TANROADS.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TANROADS Bw. Patrik Mfugale, alisema kituo hicho kina uwezo wa kuingiza magari 80 kwa wakati mmoja na zaidi ya sh. bilioni moja zimetumika kufanikisha ujenzi wake.

 
Tatizo la pinda hana maamuzi. Na hata akiwanayo ni yale ya kujutia baadaye mpaka analia mwanume mzima. Swala la kuvunja majengo ndani ya hifadhi ya barabara halikuwa na mjadara ni utekelezaji tu. Lakini pinda kwa upole, ufinyu wa kufikiri, uoga na uzembe wake kampiga magufuri stop. Magufuri sasa anatumia mwanya huo kujizolea sifa na kwa ushauri wa watu, tiss, marafiki, taasisi mbalimbali na kwa busara zake mwenyewe, rais anaweza kumfanya magufuri kuwa boss wa pinda katika hizi tetesi za baraza jipya.
 
Ukiwa na waziri mkuu ambaye yeye nikulia badala ya kusimama imara na kutua maamuzi basi ujue tunakwama.

Pinda kwa kweli hafai hata kidogo Maybe kwa sababu ya kufipa.
 
mi siku zote huwa namkubali maghufuli yachuma hata kama yashaba. Ukweli bila ya unafiki simfananishi na kiongozi yeyote iwe ndani ya chama chake hata nje ya chama chake. Kama nje ya nchi akina kiöngozi wa angola dosantos, kagame, sata, yule wa bostwana hata goodluck
 
he he he he he he he pind ahajatoa tamko bado nalisubiri kwa hamu sana na hasa baada ya hizo siku tano kuisha ili tuone utekelezaji utakuwa vipi
 
ni maneno ya kutafuta umaarufu kwa kupigiwa makofi kwa wingi.

wewe ulitaka afanyaje mkuu,akae kimya ili keshokutwa ukiwa ktk foreni uanze kupiga kelele tena?

Tatizo letu watanzania ni kwamba hatuwapendi wachapakazi,tunapenda sana kudanganywa danganywa na mwisho wa siku kupiga kelekele kwa makosa tuliyoyafanya wenyewe.mbona nchi za wenzetu haya mambo hayapo?

Jamani tembeeni muone,msikae tu mbagara ukazani ndio umemaliza Dunia.

images
M62_Station_Road_Flyover.jpg


Tukitaka barabara kama hizi ni lazima tumwache magufuri afanye kazi yake,kuliko kuleta siasa wakati bado msongamano wa magari unatuleta matatizo ktk jiji la DSM

katika nchi za wenzetu huwezi ona mtu kajenga ktk hifadhi ya barabara,na ndio maana hata barabara zao wanazipanua wakati wowote watakao kwani hakuna mwingiliano wa makazi na hifadhi za barabara.

lakini hapa bongo ni tatizo kubwa,tena watu hawataki kuguswa kabisa lakini ni wa kwanza kupiga kelekele pindi kunapotokea matatizo

Mimi ninge kuwa Magufuri,nisinge mwangalia mtu usoni,kwani barabara hizo si kwa manufaa ya magufuri ni kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake.

Nch hii ukitaka kuwaonea huruma waliojenga ktk hifadhi ya barabara kamwe hatutafika mahali popote pale
 
hii nchi ukiwa msema ukweli 2 unaambiwa unatafuta umaarufu,huyo magufuli ka umaarufu ashaupata na unapitiliza,kama mnataka foleni basi msilalamike kuwa mnachelewa kwenye mihangaiko yenu.......siasa inaimaliza tz
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom