Magufuli amsifu JK kutembeza bakuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli amsifu JK kutembeza bakuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Karibuni masijala, Sep 20, 2012.

 1. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi, "Tanzania ni Zaidi ya Uijuavyo" Nikiwa nimetulia nasikiliza habari, Mlimani Tv, Ziara ya Rais kufungua Barabara ya Msata kwa kiwango cha Lami kwa Magari ya kwenda mikoani hasa ya Kaskazini mfano Tanga na Kilimanjaro na Arusha badala ya kupitia ya Ubungo chalinze itakuwa Mwenge Msata au Msata mwenge then Ubungo; Mara baada ya kutua na helkopta ya Jeshi la Police, Alikaribishwa Waziri Makufuli akasoma hotuba kumkaribisha Rais na kumpa Tadhimini ya mradi huo; cha ajabu akaanza kumsifu Rais kwa Safari zake nje ya nchi akiwambia, waliokuwa wanamsikiliza ni Kazi ngumu kuzungumza na Wazungu kiingereza Rais amejitahidi kusafiri na matunda ya safari zake ni miradi; mara baada ya kumsifu; akatamka mradi huo unafadhiliwa na Bank ya Dunia na Serikali. Wadau ina maana Makufuli haoni tatizo la Rais wetu kuamini wazungu ndio wataleta maendeleo, haoni ziara za rais nje za utegemezi tangu asafiri mpaka sasa hazijatatua matatizo yetu zimelalamikiwa ni mzigo kwani ni nyingi zimevunja hata rekodi za waliomtangulia kama si za Afrika Mashariki na Afrika, kwani amekuwa Rais mwaka wa 7 amesafiri zaidi ya mara 360: Ukifanya hesabu za kukadiria Rais amekaa nasi mda gani kushiriki shughuli za ndani za ujenzi wa Taifa utashangaa! Kama si kuhamaki mfano: amesafiri mara 360 tukadirie safari moja mpaka arejee inamchukua siku 4( siku anayosafiri, za kushinda huko 2 anayorejea Jumla 4) Hivyo (siku 4 zidisha kwa idadi ya safari 360= siku1640 amekaa nje zibadili katika miaka mwaka una siku 360 hivyo chukua siku alizokaa nje kama amesafiri mara 360 tu na kila ziara akaka siku 2 jumlisha ya kusafiri na kurudi 4 kwa kukadiria hivyo ni sawa na siku 1640 yuko safarini na nje gawanya kwa siku za mwaka mmoja360 ili upate miaka = 4 Hivyo kama Rais amesafiri mara 360 nje na wastani wa safari ni siku 4 atakuwa mpaka sasa amekaa nje ya nchi miaka 4 akiwa Rais na huu ni mwaka wa 7 wa Urais atakuwa amekaa Tanzania miaka 3 nje miaka 4. Kukaa nje miaka 4 na 3 Tanzania inaonyesha hajashiriki sana shughuli za ndani ni rais wa nje au wa nchi? Hebu karibu na hoja za kuelimisha, kukosoa, kusifu ili tuelimishane, tukosoane, tusahishane mwisho tukubaliane huku tukisamehana kwani tukimsifu Rais kwa Safari anaweza akazizidisha na pia kuomba omba sio Issue, Issue ni kujenga Taifa lisilokuwa la omba omba. Source: Mlimani Tv Habari Ziara hiyo ilizungumziwa kwa kina.
   
 2. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods; Hebu paste iwemo pia Jukwaa la Siasa
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2015
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  kumbe hajaanza kumsifia leo
   
 4. Upepo wa Pesa

  Upepo wa Pesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2015
  Joined: Aug 8, 2015
  Messages: 9,130
  Likes Received: 9,906
  Trophy Points: 280
  Bora Lowassa anayesema anachukia umaskini kuliko huyu mwenye mawazo ya kuukumbatia umaskini!!! ngoja UKAWA waingingie madarakani!!
   
 5. s

  sungwa32 Member

  #5
  Aug 22, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine eti wanasapoti upuuzi Kama huu.safari kila siku rais gani huyu
   
Loading...