Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,152
- 44,110
Mpaka sasa mwenendo wa kimantiki Wa kampeni za mgombea urais Wa CCM hauleweki
kabisa. Wapiga kura, Wapambe na wapiga debe wa CCM wamebaki njia panda sana. Hawana mahali pa kusimamia kabisa, baada ya Magufuli ambaye ndiye mgombea urais wa CCM kushindwa kuonyesha msimamo katika Sera za CCM.
Kwa mfano.
1/Magufuli amekuwa akijinadi na kunadiwa kama mgombea binafsi kuliko kunadiwa kama mgombea wa CCM. Mabango ya kampeni za Magufuli yamekwepa kabisa kutaja neno CCM, Nembo ya kampeni za Magufuli ni Mwenge badala ya Jembe na Nyundo ambayo ndio nembo rasmi ya CCM siku zote.
Hali hii inawasumbua sana makada wengi wa CCM ambao bado wanaamini CCM pekee bado ni mtaji wa kura kuliko Magufuli Pekee yake.
2/Kauli za Magufuli za wazi wazi majukwaani za kuikosoa serikali ya CCM iliyopo madarakani na watendaji wake. Hali hii inawapa wakati mgumu makada Wa CCM kutumia tena mafanikio ya serikali ya Kikwete iliyopo madarakani kama mtaji wa kuombea kura. WanaCCM wanasema mtindo wa kuikosoa serikali ni utamaduni wa upinzani hivyo hauwezi kuongeza chochote kwa CCM zaidi ya kuwafumbua Akili wananchi ambao mwisho wa siku wataamua kuchagua UKAWA maana serikali inayokosolewa ni serikali ya CCM pia.
3/Kuiga vionjo, kauli mbiu na Sera za UKAWA za kusema Watanzania wanataka MABADILIKO. Hii kitu inawapa makada wa CCM wakati mgumu zaidi maana imekuwa ikiongeza hamasa zaidi kwa Watanzania kuamua kuchagua UKAWA waana wao ndio waasisi na wapiga debe zaidi Wa MABADILIKO.
4/Magufuli amekuwa akiwataja wazi wazi katika vikao vya ndani na hata majukwaani makada wa CCM wa juu anaohisi wanamsaliti katika harakati zake za kampeni.
Makada wengi wa CCM wanasema kitendo hicho kimewafanya wasiaminiane, watengane na hata kufuatiliana wao kwa wao badala ya kufanya siasa za msingi.