Magufuli ameanza kazi: Amtosa Chenge hadharani huko Mjini Bariadi

Jamar Said

Member
Sep 2, 2015
19
35
Katika kile ambacho wachunguzi wa mambo ya kisiasa wamekiita tukio la kimapinduzi na mwanzo wa mabadiliko mapya ndani ya CCM, Mgombea wa Urais kwa ticket ya CCM Dr. John Magufuli amefanya kile ambacho Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa wameshindwa, kumtosa Andrew Chenge hadharani.

Mwanasheria huyo mkuu wa zamani ambaye anahusika kwenye kashfa mbalimbali zilizozikumba taifa hili, ambaye ndio alikuwa mratibu wa kampeni za Urais za Edward Lowassa alipokuwa CCM alijikuta kwenye wakati mgumu leo pale ambapo Dr. Magufuli alipogoma kumpandisha jukwaani na kumkabidhi ilani ya CCM kama anavyofanya kwenye majimbo mengine. Magufuli ambaye mpaka sasa ameweka wazi adhma yake ya kuanzisha Mahakama ya Mafisadi, inasemekana aliweka msimamo wake wazi mbele ya Mwenyekiti wa kampeni za CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwamba hana mpango wa kuwanadi wana CCM wowote ambao wana kashfa za ufisadi, na amepewa baraka zote za kukisafisha Chama cha Mapinduzi ili kuonyesha tofauti na mgombea wa UKAWA ambaye ana kashfa lukuki za ufisadi.

Tukio hili la leo linaelezewa na wachambuzi wa Siasa kama mwanzo mzuri wa Magufuli kujitofautisha na makada wa CCM wasio wasafi na kurejesha imani ya Watanzania kwamba yeye ndio atakayeleta mabadiliko bora zaidi kwa Wananchi.

Itambuliwe pia, Dr. Magufuli amefanya kazi katika awamu zote mbili za Rais Mkapa na Kikwete na hajapata kashfa yoyote, tofauti na mgombea wa UKAWA ambaye kwa kipindi cha miaka 40 aliyokuwa ndani ya CCM amepata kashfa lukuki ikiwemo ya Richmond, Ranchi za serikali, na kwa sasa kuna sintofahamu kubwa kuhusu kauli zake za kuomba kura- kanisani na hali yake ya kiafya.

Kwa sasa Dr. Magufuli amefaulu kizingiti hiki kikubwa cha Mheshimiwa Chenge, na kugoma kwake kumnadi kunatuma ujumbe kwa wale mafisadi wote wa ndani na nje ya chama kujipanga kwani anaonekana ana nia ya dhati kusafisha Chama na Serikali ili kuwapa Watanzania mabadiliko chanya wanayoyahitaji.
 
watz wanataka mabadiriko hawataki hadaa za kisiasa. Mfano magufuli alimuomba chenge kuwa sitakunadi ili watz wafikiri sipendi ufisadi ila baadaye utakuwa waziri wa sheria.
 
Safi sana Magufuli mwanzo mzuri sasa wale wengine sijui watakimbilia wapi baada ya kukimbia chamani
#HapaKaziTu Mabadiliko huja kwa kazi.
 
Hawa ndio wanamabadiliko tunaowataka, sasa hapa mtanzania jiulize nani bora kati ya yule anayemkataa fisadi na yule aliemkaribisha fisadi alafu bado anajiita mwanamadiliko. Huu ni unafiki uliopindukia sana kwa watu kujiita wanamadiliko alafu wamemkumbatia fisadi, au ndo mabadiliko hayo? Hongera kwako magufuli kwa kuanza kuwapunguza mafisadi mmoja baada ya mwingine. Bado mahakama yatakiona cha moto. Huyu ndio Magufuli, na huyu ndio Tumaini letu
 
watz wanataka mabadiriko hawataki hadaa za kisiasa. Mfano magufuli alimuomba chenge kuwa sitakunadi ili watz wafikiri sipendi ufisadi ila baadaye utakuwa waziri wa sheria.

Kuna cyber crime mnamjaza magufuli maneno ambayo hakuyatamka hapa ni kuwakomesha Tu mafisadi!
 
Magufuli ni jembe kweli na hana masihara na watu ambao anawatilia shaka kiutendaji. Safi sana magufuli kwa kuliona hilo, Chenge hana tija yoyote muache ajinadi na kujipigia kampeni mwenyewe.
 
Back
Top Bottom