Magufuli akabidhiwa haya majina ya wauza 'unga'

Hill jipu ni kubwa tena limekaa pabaya,
Jpm ataliweza?ataweza kutafuna mfupa uliomshinda fisi?
Wananchi tuko na wewe Raisi wetu tunakuunga mkono pia tunafuatilia kwa makini.
 
nawasiwasi nahayo majina si yakweli naona yameegemea zaidi upande mmoja tu...and I hv not seen even one veteran....
 
Kama kuna wengine walishapiga hela ya kutosha na wakaachana na hiyo biashara ina maana watachunguzwa kwa mali zao wamezipataje, kwa mfano magari yao nyumba zao na fedha walizo nazo?
Tutaona mwisho wao ingawa ni bora wangedhibiti tu zaidi uingizaji wa hayo madawa na pia wangeweka rehabilitation centers kwa watumiaji walioathirika ili wataalamu wawasaidie kuacha tabia hiyo
 
Watawataja ila hawawezi kuwakamata ata wakiwakamata hawawezi kuwafunga. Hao maboss wa unga wengine hawajawai ata kuuona huo unga unafananaje utamfungaje mtu bila ushahidi ndio maana yule Waziri jana alisema kuwa na list peke yake sio dawa. Watu wanaleta siasa wanajifanya wana uchungu sana. Bongo biashara ya unga ni njia tu hamtakaa muwakamate ma big wig mtaishia kukamata nyoka wanaofunga vumbi la Pakistan.
mkuu ni kweli kabisa ma big wig wote 90%ya unga wao ni njia tu unapita hapa wao ela zao wanapata kwa kuuza nje,makilo kwa makilo na wao unga wao unaletwa na majahazi na wapakistani..utakuta only 10%ya mzigo wote unaoingia ndo unauzwa hapa na hawa wadogo wadogo ndo hao wanatajwa
 
JPM katuchosha bure. Alisema ooh! Mniombee. Sasa tumemuombea anaishia kukamata mateja. Kova tafanya kazi gani sasa?
 
haya mambo yanahitaji umakini sana maana hiyo orodha imetoka kwa nani? na je ina ukweli kiasi gani?

sidhani kama kuna mtu binafsi anaweza kujua orodha kubwa ya mtadao wa wauza madawa ya kuevya labda kama ni muuza unga mwandamizi na aliyekuwa au bada ana cheo kikubwa katika mtandao wa unga.

taasisi za kiuchunguzi pengine zinaweza kujua orodha kama hii.

baada ya kujua kuwa ni vigumu kujua orodha kubwa kama hii tunaweza kujiuliza hii orodha inayowekwa hadharani kama vile ni jambo rahisi kuipata inaweza kuwa imetoka wapi
1. yawezekaa ikawa ya ukweli hatuwezi kuondoa hilo kama hatuna ushahidi.
2. yaweekana kutengenezwa na wauza unga wenyewe wakiorodheshwa watu feki ili kupotosha vita ya kupambana nao ijielekeze kwa watu wasiohusika kama njia ya kudonosha vitambulisho maeneo ya matukio ya wizi. nguvu za dola zinabaki kuangaika na watu wsiohusika huku wahusika wakiendeza shughuli zao.
3. Yawezekana baadhi wapatengeneza orodha kwa malengo ya kutengeneza heading za kibiashara.

ushauri wangu vita ya kupambana na vievi hivi intakiwa kuwa makini wasipuuze taaifa wanazoletewa lakini wafanye uchunguzi wa kina sio kutegemea taarifa za kupewa tu

 
Hatua zichukuliwe maana hata JK alikabidhiwa.Hadi sasa jitihada za Amina Chifupa hakuna aliyethubutu kuziendeleza.Sasa tuone...

Hongereni Jamhuri kwa kulisaidia Taifa,Hongereni kaka zangu Manyerere na Balile

Tena gazeti liwe publicised kwa nguvu leo hata kwa social media ili lisomwe kwa wingi tuitie serikali pressure ya kuchukua hatua.
CCM wameshindwa kabisa hii vita,Tunaomba WATETEZI WA WANYONGE KINA BABA MBOWE;MSIGWA;TUNDU LISSU,SUGU,LEMA na makamanda wengine WAWEKE HADHARANI orodha ya wauza sembe watuokoe.................................
 
Akachukue Na Yale Aliyokabidhiwa Mzee Wa MSOGA, Maana Hayajafanyiwa Kazi Mh. MAGUFULI!!! Kama Ulikabidhiwa Basi TUNAOMBA Uanze Nayo, Kwani Siku Zimeenda Mno!!!
 
Mbona Hiyo ORODHA Haipo Ktk Huu Uzi Wako!!?? Kumbe WATANZANIA Ni Waooga Tu, Maana Kama Unasema Gazeti Limetoa ORODHA, Why Ww Haukuiweka Hapa WATANZANIA Tusio Na Access Ya Kusoma Hayo Magazeti Yenu!!!! ALAFU Kama Ni ORODHA Mbona Hata Mzee Wa MSOGA Alikabidhiwa Na TUME Yake Aliyoiunda Mwenyewe!!!? Lkn Hadi Ameondoka Hakutajwa Hata Mmoja!!! TULIMSIKIA Waziri Lukuvi Akisema BUNGENI, Kuwa Eti Hiyo ORODHA Endapo Itasomwa Na Kuwekwa HADHARANI, Kuna WATU Humu BUNGENI Mtaadhirika, Kwa Maana Yake Kuwa Humo BUNGENI Kuna Mataikuni KIBAO!! Ila Wanalindwa Tu!! NDIO Maana WATANZANIA Tunaamini Kuwa BIASHARA Ya UNGA Inafanywa Na Vigogo Ktk. Nchi Serikalini!!! NDIO Sababu VITA Vyake Ni Vigumu Kufanikiwa!!!!!

Ungekuwa unasoma post zote kabla ya ku comment ungeona majina yaliyorushwa.
 
kukabidhi majina bila kuwakamata na kidhibiti ni sawa na kazi na bure, jeshi la posili liweke mechanisms za kudhibiti na kukamata kwa ushahidi na vidhibiti na hatua zichukuliwe.


Hatua zichukuliwe maana hata JK alikabidhiwa.Hadi sasa jitihada za Amina Chifupa hakuna aliyethubutu kuziendeleza.Sasa tuone...

Hongereni Jamhuri kwa kulisaidia Taifa,Hongereni kaka zangu Manyerere na Balile

Tena gazeti liwe publicised kwa nguvu leo hata kwa social media ili lisomwe kwa wingi tuitie serikali pressure ya kuchukua hatua.
 
Mmh! mbona wale wakuu wa hicho kitengo hawapo wakati wanaboard yao kabisa na makao makuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom