Magufuli ajibu shutuma za Zitto

Magufuli ajibu shutuma za Zitto

Maghufuli ni vigumu sana kumchafua, watu wanaomzunguka wanaoweza kumtetea ni wengi mno. Tumuache tu nyota yake iko juu jamani.

* Mjadala uliopo hauhusiani na mambo ya nyota....mambo ya nyota nenda kazungumze na mtoto wa Sheikh Yahya.....

* Baraza la mawaziri kuamua kujiuzia nyumba za serikali zilizopo kwenye maeneo ghali kwa bei ya maandazi ni ufisadi wa aina yake....

* Kusema sababu za kuuza nyumba ni gharama ya marekebisho haiingilii kwenye akili ya mtu yeyote mzima mwenye akili timamu.....
 
Unakurupuka kujibu bila fuatilia clip ya video ya Sumaye (Umecomment hivi kwenye thread fulani) alisema nini au uvivu wa kuchunguza mambo? Kipindi fulani Magufuli aliondolewa katika Wizara ya Ujenzi (2005-2010) ili wachunguze kama kulikuwa na wrongdoing mwisho wa siku wakaambulia patupu ikiwemo kumrudishia wizara anayoimudu - leo kila mtanzania asiye mnafiki anakiri mafanikio ya barabara ikiwemo ujenzi wa nyumba mpya za serikali.

Habari ya watu ndugu zake waliuziwa nyumba unazidi kupotea kabisa mambo haya yalichunguzwa vilivyo kipindi Magufuli kaondolewa wizarani, njooni na vitu vingine hili la nyumba mnapoteza muda wenu badala ya kuufanyia kazi zenye tija.
Mkuu, huyo Shakir ni miongoni mwa wanazi wa UKAWA, maji yanaanza kuwafika shingoni baada ya kutoamini kinachoweza kumtokea Maghufuli. Hivi Magnufuli akipitishwa na chama chake , hawa UKAWA watasimama wapi kuwaambia watanzania kiwa hafai? Wao watasema wanafaa kwa lipi zaidi ya Maghufuli? Kwa kifupj wameanza kuweweseka.
 
yani uamuzi wa baraza la mawaziri hata wa kijambazi ndio uutekeleze,si angejiuzulu!!!halafu huyu kilaza alituambia wakazi masikini wa kigamboni tupige mbizi.
Mkuu hoja yako kama ya zubeda au mtoto wa darasa la tatu c unaadika kama akili zimelowa maji.
 
* Mjadala uliopo hauhusiani na mambo ya nyota....mambo ya nyota nenda kazungumze na mtoto wa Sheikh Yahya.....

* Baraza la mawaziri kuamua kujiuzia nyumba za serikali zilizopo kwenye maeneo ghali kwa bei ya maandazi ni ufisadi wa aina yake....

* Kusema sababu za kuuza nyumba ni gharama ya marekebisho haiingilii kwenye akili ya mtu yeyote mzima mwenye akili timamu.....

Nyumba za serikali ziliuzwa kukwepa gharama kukiwa na mifano ya nchi:

1. Kenya,

2.Uganda

3.Zambia

4.Korea ya Kusini

5.Afrika ya Kusini n.k

Wewe unataka kusem nini hapa!
 
Maghufuli sasa yuko huru, mwenye kashfa nyingine dhidi yake aiibue tuijadili. Hongera JPM.
 
Nyumba za serikali ziliuzwa kukwepa gharama kukiwa na mifano ya nchi:

1. Kenya,

2.Uganda

3.Zambia

4.Korea ya Kusini

5.Afrika ya Kusini n.k

Wewe unataka kusem nini hapa!

Wamekosa hoja ya kumkandamiza Maghufuli hao.
 
Bado hajajibu swali,
Kwanini basi huyo wakala wa majengo asiwe yeye ndio mmiliki wa hizo nyumba za serikali? Yaani kwanini serikali isingeanzisha agency ya kuzisimamia hizi nyumba badala ya kuziuza?

Na ukiuza nyumba aliyokua akikaa labda mkuu wa wilaya, akija mpya atakaa wapi?

Inaingia vipi akilini uuze Nyumba kwa Million 20 (mapato) miaka 15 iliyopita, kisha uanze kuwalipia rent waliokosa Nyumba baada ya hizo kuuzwa labda jumla million 45 (matumizi) kwa kipindi chote hicho??

Unakiri kua idadi ya wafanyakazi wa serikali inaongezeka kila kukicha, kama waliokuwepo serikalini kipindi kile waliuziwa hizo nyumba, vipi walioko serikalini sasa watauziwa zipi? Huoni kama ni ubaguzi?

Nani alipanga bei za kuuzia hizo nyumba? Utauzaje nyumba iliyoko Prime location kama Bongoyo Street, Oyesterbay, Kiwanja Low Density (Sqm 4,000) kwa million 30?? Tena hela ambayo huikusanyi mara moja bali unakata kidogokidogo kwenye mishahara??

Category ya kuwachagua wafanyakazi wa kuzinunua ilikua ni nini? Wapo watu ambao waliuziwa kwanza Nyumba kabla ya kupata ajira serikalini. Magazeti ya Habari Corporation yakiwa chini ya Jenerali Twaha Ulimwengu yaliandika sana hii story, tena file la transfer of ownership alikua akilibeba Magufuli mwenyewe kulipitisha Department mbalimbali na ole wako ucheleweshe, huu ni ufisadi huu, hauwezi kufutika kwa sifa ya mtu tu kukariri idadi ya madaraja na kilomita za barabara, bado anabaki fisadi tu.

Hapa bana watu waliamua kujiuzia hizo nyumba kifisadi, na hata kama ni uamuzi wa baraza la mawaziri basi walihakikisha kila mmoja anapata nyumba kwake au kwa ndugu yake

Kwa hili naungana na Zitto, yeyote alieshiriki huu ufisadi akiwemo Fredrick Tuluway Sumaye hatufai, na sio ws kuombea apitishwe hiyo tarehe 12-July

Well said mkuu
 
Last edited by a moderator:
* Mjadala uliopo hauhusiani na mambo ya nyota....mambo ya nyota nenda kazungumze na mtoto wa Sheikh Yahya.....

* Baraza la mawaziri kuamua kujiuzia nyumba za serikali zilizopo kwenye maeneo ghali kwa bei ya maandazi ni ufisadi wa aina yake....

* Kusema sababu za kuuza nyumba ni gharama ya marekebisho haiingilii kwenye akili ya mtu yeyote mzima mwenye akili timamu.....
Tatizo lako umezoea kuoiga ramli ndiyo maana kila nyota inayoongelewa unawaza kwa sheikhe Yahaya.
 
Mimi na watanzania wengi tuna imani kubwa na Maghufuli tuombe tu Mungu CCM wampitishe, atatufikisha mahali haya mengine yanayosemwa ni kutapatap tu kwa wale walioingiwa hofu baada ya kuchukua fomu.
 
Kama wewe ni kipofu na kiziwi utajuaje kama amejibu?
Mkuu, wanasiasa ni watu wabaya sana, wanajaribu kutuharibia, huyu Maghufuli ndiye mtu muafaka kwa sasa, napenda sana udikteta wake.
 
Kama ni kosa lilikuwa la serikali nzima na sio Dr. Magufuli kama mtu binafsi. Kuna watu wanang'ang'ania kumbebesha mtu mmoja mzigo wa watu wengi
 
Nyumba za serikali ziliuzwa kukwepa gharama kukiwa na mifano ya nchi:

1. Kenya,

2.Uganda

3.Zambia

4.Korea ya Kusini

5.Afrika ya Kusini n.k

Wewe unataka kusem nini hapa!

* Tatizo sio kuuza nyumba...tatizo, zinauzwa kwa bei gani....
 
Dr. Magufuli na Dr. Mwakyembe ndio wanaweza kuiweka nchi hii sawa
 
Kuna watu wana ajenda mbaya na nchi hii. Wanataka watupe rais mzigo. Rais wa kutufukarisha zaid.
 
Tatizo lako umezoea kuoiga ramli ndiyo maana kila nyota inayoongelewa unawaza kwa sheikhe Yahaya.

* Hatuongelei nyota...tunaongelea facts basi....hayo mambo ya sheikh yahya achana nayo....

* Unajua bei ambayo 'baraza la mawaziri' iliuzia hizo nyumba?......
 
Zitto na filam zake kwa mafisadi.
Maigizo haya yanalenga zaid kuwasafisha mafisadi wa ccm ili wajiunge nae wakikosa urais ama wamsifie kama siku zote wanavyofanya.

Zitto, na ulaaniwe na watanzania wote waliokuwa wameamua kuunganisha nguvu ya vyama ili kumuondoa mkoloni ccm na badala yake unesaidia nguvu ya ccm kuigawa nguvu ya upinzani na kuwafanya watz mazuzu waanze safari upya ya kujenga chama na kuipa ccm nafasi ya kuendelea kuwaibia wananchi, huku ukijinasibu kutaja watu wajitete na wakati wajua haitasaidia kitu maana ndiyo wenye mamlaka.
Unaudhi sana
 
Wewe unasumbuliwa na Ushabiki wa kisiasa tu, hivi hata hayo aliyoyasema Waziri Mkuu aliyesimamia zoezi hilo bado unasema ni Maghufuli. Unakimbia kusema ni mfumo hata haujui mfumo ni nini, au unataka kutuambia Maghufuli ndiyo mfumo wenyewe. Acha na wewe comments blah blah.

Najua anatamani Magufuli aingie madarakan ili na wewe upate hata kanafasi ka kudeki choo ikulu, ila pole maana Magufuli haitotokea kamwe kukanyaga ikulu
 
Back
Top Bottom