Magufuli afumua sheria ya manunuzi

Magufuli afumua sheria ya manunuzi

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,953
Reaction score
6,996
TUME ya Kurekebisha Sheria imeanza mchakato wa kuifanyia marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 kama njia ya kuitikia mwito wa Rais John Magufuli ambaye aliahidi kuifanyia marekebisho sheria hiyo wakati analizindua Bunge la 11.

Tayari Tume hiyo imetoa tangazo linalowataka wananchi au taasisi mbalimbali kutoa maoni ndani ya siku 30 kuanzia jana. Maoni na mapendekezo hayo yanaweza kuwa ya jumla au kuhusu masharti mahususi ya sheria au mifumo ya kitaasisi iliyoundwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Akilihutubia Bunge, katika eneo la kuziba mianya ya rushwa, Dk Magufuli aliahidi kuifumua sheria hiyo ambayo inatoa mianya kwa watumishi wa umma kuiba fedha za umma. "Tutasimamia kwa ukamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma ili kuhakikisha kwamba mianya yote ya fedha za umma inayotokana na usimamizi hafifu tunaiziba.

Ni matarajio yangu tutakapoleta Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma Waheshimiwa Wabunge mtatuunga mkono," Dk Magufuli alisema katika hotuba hiyo.

Kwa mujibu wa tangazo la Tume hiyo, madhumuni ya utafiti huo ni kubainisha upungufu katika utekelezaji wa sheria, kubainisha madhara ya upungufu huo katika utekelezaji wa sheria kwa Serikali na taasisi zake.

Tume hiyo imeainisha maoni hayo kuhusu misingi ya soko, pamoja na mabadiliko endelevu ya kisheria, hatua mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa bidhaa au huduma, ulinganifu wa thamani ya fedha kwa bidhaa inayonunuliwa au huduma inayotolewa.

Maoni mengine ambayo Tume hiyo inaomba kutoka kwa wadau ni kuhusu mgogoro unaojitokeza katika sheria zinazohusiana na ununuzi wa umma na athari za kibinadamu katika mchakato wa ununuzi kama vile rushwa, mgongano wa maslahi binafsi na ukosefu wa maadili.

Sheria ya Ununuzi wa Umma inayotumika sasa ilitungwa na Bunge mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho makubwa na Bunge mwaka 2011 kwa lengo la kuweka mfumo wa kisheria na kitaasisi wa usimamizi wa ununuzi wa umma.

Katika utekelezaji wa sheria hio, Serikali na taasisi zake zimebaini kasoro ambazo zimekuwa kikwazo katika utekelezaji bora wa sheria hiyo tangu ilipotungwa kwa mara ya kwanza mwaka 2001.

Kasoro zimeendelea kuwepo hata baada ya Bunge kuifuta na kutungwa upya Sheria ya Ununuzi wa Umma mwaka 2004. Miongoni mwa kasoro hizo ni pamoja na mlolongo mrefu na gharama nyingi katika mchakato wa ununuzi kabla ya kufanya ununuzi unaokusudiwa.

Chini ya sheria hiyo, Serikali imekuwa inauziwa bidhaa mbalimbali kwa bei kubwa tofauti na bei halisi ya soko jambo ambalo limeifanya Serikali kutumia fedha nyingi kwenye manunuzi. Kwa mujibu wa Bodi ya Manunuzi ya Umma, Serikali inatumia asilimia 70 ya bajeti yake kwa ajili ya kufanya manunuzi mbalimbali.

Pia sheria hiyo inatoa mianya kwa baadhi ya maofisa wa Serikali kufisadi fedha za umma na kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha. Udhaifu mkubwa katika sheria hiyo ni pale Serikali inapotakiwa kulipia riba katika ununuzi wa bidhaa mbalimbali jambo ambalo limekuwa linaigharimu serikali fedha nyingi.

Miongoni mwa mapungufu ya sheria hiyo ni adhabu zinazotolewa kwa watu wanaoisababishia hasara Serikali ambayo kwa mujibu wa sheria hiyo, anatakiwa kufungwa jela kifungo kisichopungua miaka saba na kulipa faini isiyopungua Sh milioni 10.

Chanzo:HabariLeo
 
magufuli wanyooooooshe na ukabe mpaka penati, walizoea kutunyonya sana
 
Sheria ya manunuzi imekaa kingese sana lazima ifumuliwe mapema kabisa mwakani tuanze na sheria mpya.
 
TUME ya Kurekebisha Sheria imeanza mchakato wa kuifanyia marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 kama njia ya kuitikia mwito wa Rais John Magufuli ambaye aliahidi kuifanyia marekebisho sheria hiyo wakati analizindua Bunge la 11.
Tayari Tume hiyo imetoa tangazo linalowataka wananchi au taasisi mbalimbali kutoa maoni ndani ya siku 30 kuanzia jana. Maoni na mapendekezo hayo yanaweza kuwa ya jumla au kuhusu masharti mahususi ya sheria au mifumo ya kitaasisi iliyoundwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma.
Akilihutubia Bunge, katika eneo la kuziba mianya ya rushwa, Dk Magufuli aliahidi kuifumua sheria hiyo ambayo inatoa mianya kwa watumishi wa umma kuiba fedha za umma. ?Tutasimamia kwa ukamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma ili kuhakikisha kwamba mianya yote ya fedha za umma inayotokana na usimamizi hafifu tunaiziba.
Ni matarajio yangu tutakapoleta Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma Waheshimiwa Wabunge mtatuunga mkono,? Dk Magufuli alisema katika hotuba hiyo.
Kwa mujibu wa tangazo la Tume hiyo, madhumuni ya utafiti huo ni kubainisha upungufu katika utekelezaji wa sheria, kubainisha madhara ya upungufu huo katika utekelezaji wa sheria kwa Serikali na taasisi zake.
Tume hiyo imeainisha maoni hayo kuhusu misingi ya soko, pamoja na mabadiliko endelevu ya kisheria, hatua mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa bidhaa au huduma, ulinganifu wa thamani ya fedha kwa bidhaa inayonunuliwa au huduma inayotolewa.
Maoni mengine ambayo Tume hiyo inaomba kutoka kwa wadau ni kuhusu mgogoro unaojitokeza katika sheria zinazohusiana na ununuzi wa umma na athari za kibinadamu katika mchakato wa ununuzi kama vile rushwa, mgongano wa maslahi binafsi na ukosefu wa maadili.
Sheria ya Ununuzi wa Umma inayotumika sasa ilitungwa na Bunge mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho makubwa na Bunge mwaka 2011 kwa lengo la kuweka mfumo wa kisheria na kitaasisi wa usimamizi wa ununuzi wa umma.
Katika utekelezaji wa sheria hio, Serikali na taasisi zake zimebaini kasoro ambazo zimekuwa kikwazo katika utekelezaji bora wa sheria hiyo tangu ilipotungwa kwa mara ya kwanza mwaka 2001.
Kasoro zimeendelea kuwepo hata baada ya Bunge kuifuta na kutungwa upya Sheria ya Ununuzi wa Umma mwaka 2004. Miongoni mwa kasoro hizo ni pamoja na mlolongo mrefu na gharama nyingi katika mchakato wa ununuzi kabla ya kufanya ununuzi unaokusudiwa.
Chini ya sheria hiyo, Serikali imekuwa inauziwa bidhaa mbalimbali kwa bei kubwa tofauti na bei halisi ya soko jambo ambalo limeifanya Serikali kutumia fedha nyingi kwenye manunuzi. Kwa mujibu wa Bodi ya Manunuzi ya Umma, Serikali inatumia asilimia 70 ya bajeti yake kwa ajili ya kufanya manunuzi mbalimbali.
Pia sheria hiyo inatoa mianya kwa baadhi ya maofisa wa Serikali kufisadi fedha za umma na kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha. Udhaifu mkubwa katika sheria hiyo ni pale Serikali inapotakiwa kulipia riba katika ununuzi wa bidhaa mbalimbali jambo ambalo limekuwa linaigharimu serikali fedha nyingi.
Miongoni mwa mapungufu ya sheria hiyo ni adhabu zinazotolewa kwa watu wanaoisababishia hasara Serikali ambayo kwa mujibu wa sheria hiyo, anatakiwa kufungwa jela kifungo kisichopungua miaka saba na kulipa faini isiyopungua Sh milioni 10.
Napendekeza asilimia 99% ya vifaa vya maofisini na ujenzi katika mashirika yoote ya uma ukijumuisha na wataalamu iwe ni MADE IN TANZANIA
 
kwani walio itunga wako hai au wafu ? CV Za walio ipitisha zikoje ? Magufuli kipindi inapitishwa hakuwemo bungeni ? Alitoa maoni gani kama msemaji WA sirikali ?

Nakubaliana NA Lowassa kuhusu ELIMU, ELIMU, ELIMU
 
kwa kwi kwi hiyo sharia Mnyika alipiigia kelele weee wabunge wa CCM na ndiooooooooooo yo zao wakaipitisha sasa munasema Magufuli wenye nchi walishaiona mbaya haifai achene kumpaisha mtu aliyeishabikia ikapitishwa unafiki mkubwa
 
jamani hata X ray machine,POP,GIC,Hand piece,bandage na kumwaga oil zinahitaji idara ya manunuzi
 
kwani walio itunga wako hai au wafu ? CV Za walio ipitisha zikoje ? Magufuli kipindi inapitishwa hakuwemo bungeni ? Alitoa maoni gani kama msemaji WA sirikali ?

Nakubaliana NA Lowassa kuhusu ELIMU, ELIMU, ELIMU

Kama ungekuwa na hiyo ELIMU wewe, ungejikita kwenye mada iliyo mezani, nayo ni "Sheria ya manunuzi ya Serikali"! Kwanza kunyoosha vidole hakuisaidii kuwa bora kama yenyewe ni mbovu, au mbovu kama yenyewe ni bora! Ungetumia hiyo ELIMU yako kuichambua sheria husika kuonesha "ubovu" wake au "ubora" wake, ungalionesha tofauti kuwa wewe ni GT!!!
 
kwanza ni vyema sheria hii ikaruhusu yafuatayo: -

1. Utaratibu wa tenda wa sasa kwa taasisi za umma ufutwe.

2. Suppliers wote wa goods na services waweke bei za bidhaa/huduma zao hadharani kila baada ya miezi 6.

3. Suppliers wote wanaotaka kuuza bidhaa/huduma zao kwenye taasisi za umma waweke wazi/hadharani kila baada ya miezi 6 kanzi data yao na taarifa za biashara zao kuepusha conflict of interests.

4. Taasisi zote za umma ziruhusiwe kununua bidhaa/huduma wanayohitaji kutoka kwa supplier kutokana na ubora wa bidhaa/huduma aitakayo bila kushurutishwa kununua kwa mtoa huduma kwa sababu yoyote ile. Kuwepo na value for money na kwamba manunuzi yote yafanyike ndani ya nchi kwa fedha ya kitanzania isipokuwa kwa huduma isiyopatikana nchini mwetu.

5. Muda wa manunuzi uwe si zaidi ya mwezi 1 toka taasisi ya umma inapokusudia kununua bidhaa/huduma waitakayo kwa kutangaza azimio la kuhitaji huduma husika kwa jamii.

6. Iwe ni marufuku kwa watu/kampuni ya kati kuonyesha nia ya kutaka kutoa huduma husika kwa taasisi ya umma wakati bidhaa/huduma husika inatengenezwa/inatolewa na kampuni/mtu iliyopo ndani ya tanzania.

7. Manunuzi yote ya umma yawe yanahakikiwa kupata ubora stahiki na pia kusiwepo na conflict of interest kutoka kwa mnunuzi na muuzaji wa huduma husika.

8. Zitolewe leseni mpya kila mwaka kwa wato huduma zikionyesha aina ya huduma na asili ya huduma husika. Pia mtoa huduma asiruhusiwe kurukia huduma ambayo hajajiandikisha nayo TRA/Baraza la biashara na kwenye leseni yake.

9. Uwepo uhakiki wa huduma itolewayo kama ni ya viwango au la na kampuni husika kuhakikiwa kila mwaka kuepusha vishoka wapiga dili katika taasisi za umma.

10. watoa huduma katika taasisi za umma wahakikiwe kuepusha mahusiano ya kindugu katika utoaji huduma kwa upendeleo.
 
Kama ungekuwa na hiyo ELIMU wewe, ungejikita kwenye mada iliyo mezani, nayo ni "Sheria ya manunuzi ya Serikali"! Kwanza kunyoosha vidole hakuisaidii kuwa bora kama yenyewe ni mbovu, au mbovu kama yenyewe ni bora! Ungetumia hiyo ELIMU yako kuichambua sheria husika kuonesha "ubovu" wake au "ubora" wake, ungalionesha tofauti kuwa wewe ni GT!!!

Hana elimu ndiyo maana anashindwa kuchangia hivyo anaomba sheria ya lowasa elim elim imsaidie
 
sheria za manunuzi ni kandamizi, uwezi kupata makampuni mapya ya vijana walijiajiri, badala yake utakuta, BMTL, CC, CATS, COSTECH haya yanafanya hawa waonekane Mungu mtu, kampuni mpya hazikui eti kigezo ni kubobea. Ndio maana hata watu wanashindwa kuservice na kutengeneza MR Scan za muhimbili kwa sababu ya kuhozi biashara.
 
kwani walio itunga wako hai au wafu ? CV Za walio ipitisha zikoje ? Magufuli kipindi inapitishwa hakuwemo bungeni ? Alitoa maoni gani kama msemaji WA sirikali ?

Nakubaliana NA Lowassa kuhusu ELIMU, ELIMU, ELIMU

Hiyo sheria ilivyotungwa Lowassa alikuwa sehemu ya serikali ya CCM. Hivyo sijui unataka kujaribu kusema nini hapa!?
 
Maccm h?ta upeleke utumbo gani wao ni ndiyoooo mapofu ya kusoma
 
kwani walio itunga wako hai au wafu ? CV Za walio ipitisha zikoje ? Magufuli kipindi inapitishwa hakuwemo bungeni ? Alitoa maoni gani kama msemaji WA sirikali ?

Nakubaliana NA Lowassa kuhusu ELIMU, ELIMU, ELIMU

Sasa tubaki tu na hiyo sheria hata kama ni mbovu?
 
kwani walio itunga wako hai au wafu ? CV Za walio ipitisha zikoje ? Magufuli kipindi inapitishwa hakuwemo bungeni ? Alitoa maoni gani kama msemaji WA sirikali ?

Nakubaliana NA Lowassa kuhusu ELIMU, ELIMU, ELIMU

Vp wewe pia hukuwe na EL unayekubaliana naye pia hakuwepo? :spy:
 
HEKO MH.RAIS JPJM!
TUA-DOPT DIRECT KUTOKA KENYA!
HAKUNA HAJA YA KUUMIZA VICHWA LET ""COPY N PASTE""
why? because,ipo vema sana!_/ na wamekuja ipata baada ya kutaabishwa mno na wajanja!
 
Back
Top Bottom