Magreth Simwanza Sitta anawahonga wajumbe Urambo kata ya Songambele

MTUNZA AMANI

Senior Member
Jun 2, 2012
187
21
Habari wanajf,

Muda huu niko eneo la tukio, Magreth Sitta amewakusanya wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa kata ya Songambele akiwataka wamchague kuwa mgombea wa ubunge kwa tiket ya CCM.

Mbaya zaidi amegawa rushwa kwa kuwapa viongozi 20000 Sh kila mmoja,viongozi hao wametoka vijiji vya Ukwanga,Jionenee, Igunguli,Songambele yenyewe.

Huyu mama anataka kumrithi mume wake kiti cha ubunge.Katika zoezi hilo ameshirikiana na Diwani wa kata ya Songambele bw ELIA KAFWENDA.

Nimeshuhudia mwenyewe na nilizamia kikao.

Update
Katika zoezi hilo eti anasema yeye anauzoefu sababu amewahi kuwa waziri wa elimu,rais wa CWT pia eti anasema yeye ndo kapigania kuundwa kwa tume ya waalimu bungeni. Pia kasema eti anawajali vijana na vionhozi kwakuwa amewanunulia viongozi wa mashina baiskeli.

Pia amethibitisha kuwa katika michezo ya UMISETA kuwa alitoa rushwa ya jez na mipira.
Mbaya zaidi eti amesema yeye alijenga hostel za waschana shuleni kitu ambacho siyo kweli.

Huyu mama kwakweli anjisifu waziwazi kwa rushwa pia amewaahidi kuwa amewaandalia fungu la kutosha, na amekuwa na wapambe akiwemo mwenyekiti wa UWT kata ya songambele pamoja na mumewe mzee aliyejitambulisha kwa jina la Simon Ntamogwa.
 
Tumewazoea bwana, Kama Mwenyekiti wenu Kikwete na Team yake Membe na Manji walikamatwa na Begi la kuhonga wajumbe Dodoma, itakuja hii hii ya huyo Magreth Sitta?
 
huyo mama hajaanza leo kugawa rushwa. hata uchaguzi uliopita alishikwa na takukuru akigawa simu za nokia ya tochi. ila kwa sababu ametoka kwenye mfumo uleule (ccm) wakamuachia kama ilivyokuwa kwa mwakalebele kule iringa. kwa lugha rahisi huyo mama ni sugu wa rushwa.

Habari wanajf,muda huu niko eneo la tukio, Magreth sita amewakusanya wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa kata ya songbele akiwataka wamchague kuwa mgombea wa ubunge kwa tiket ya CCM. Mbaya zaidi amegawa rushwa kwa kuwapa viongozi 20000 Sh kila mmoja,viongozi hao wametoka vijiji vya Ukwanga,jionenee, igunguli,songambele yenyewe,. Huyu mama anataka kumrithi mume wake kiti cha ubunge.Katika zoezi hilo ameshirikiana na Diwani wa kata ya Songambele bw ELIA KAFWENDA. Nimeshuhudia mwenyewe na nlizamia kikao.
 
Tumewazoea bwana, Kama Mwenyekiti wenu Kikwete na Team yake Membe na Manji walikamatwa na Begi la kuhonga wajumbe Dodoma, itakuja hii hii ya huyo Magreth Sitta?
begi lile lilikuwa la team lowasa. acha kupotosha. uliza aliyeshikwa alikutwa kwenye hotel iliyokuwa imepangishwa na wapambe wa nani?
hivi unafikiri kama lingekuwa la Kikwete nani angethubutu kushika? labda kama hajipendi!
 
Bag linakamatwa lowassa alishakatwa zamani, hapo lowassa anaonga ili iweje acha kupotosha na waliokamata ni wapambe wa lowassa
 
Hivi hiyo siyo fedha ya nauli na lunch kwa wajumbe? Ni rushwa kweli? Hebu chunguza chunguza kidogo.

Ccm imewafanya watanzania kama hayawani. Tunaishi maisha magumu sana. Hao wazee wametoka kule walikotoka, wameacha kazi zao kwa wito wa mama yao. Sidhani kama wanaweza kuwa na fedha za kujisafirisha na kujikimu huko walikkoitwa. Isije ikawa unaisema rushwa kumbe ni nauli na chakula.

Mara nyingi viongozi hutaka wapewe fedha wasafiri na kupata chakula wanachoona wao huku lengo likiwa ni kujinyima na kuweka akiba za kutumia nyumbani na familia zao.

Angalia tena upya kisha utujuze.
 
Halafu nyie wanyamwezi wa Urambo na Machinga wa Mtwara mnahongwaje buku 10 au 20? Wenzenu B wanaita pesa ya mboga si wafikishe hata laki? SHAME
 
huyo mama hajaanza leo kugawa rushwa. hata uchaguzi uliopita alishikwa na takukuru akigawa simu za nokia ya tochi. ila kwa sababu ametoka kwenye mfumo uleule (ccm) wakamuachia kama ilivyokuwa kwa mwakalebele kule iringa. kwa lugha rahisi huyo mama ni sugu wa rushwa.

Aisee unakumbukumbu, me nakumbuka Nokia ya tochi huyu mama alikua nazo nyingi sana kwenye boot ya gari .......rushwa tupu.
 
Tuwaombe wanchi wa tanzania mzima kuikataa ccm kupitia sanduku la kura,tusitegemee vyombo vya sheria kwani meno ya mbwa hayaumani
 
Back
Top Bottom