Kizoku
Senior Member
- Apr 30, 2014
- 186
- 66
Mafuriko makubwa zaidi yaliyotokea leo katika eneo lote la Magomeni Kilosa ni ya kushtusha. Nadhani ni busara serikali ikachukua hatua madhubuti na za kudumu kuliondoa tatizo hili.
Ingawa kwenye mafuriko yaliyopita kulitokea ahadi mbalimbali ikiwepo ya kuwajengea makazi mapya wakazi hawa lakini baada ya kukaa makambini kule eneo la Kiwanda cha mazuria walirudishwa tena makwao.
Sijui safari hii mafuriko haya yatasababisha maafa kiasi gani lakini tayari yamesambaa mji mzima na nyumba kadhaa zimekwishaanguka.Ingalie pia busara za kujenga tuta upande mmoja ambao sehemu kubwa ndio njia rasmi ya maji na kuacha upande wa pili bila tuta na kuwa dhaifu kiasi kwamba maji yetu yakasambaa upande huo na kusababisha madhara makubwa kiasi hiki.
Pia namuomba mheshimiwa raisi aombe orodha ya walioathirika kwenye mafuriko ya mwanzo yote na kuhakiki mmoja mmoja kama walipewa viwanja kama walivyoahidiwa au viwanja viliishia kwa wajanja wachache.
Pia reli ambayo ilijengwa hapo zama za kale kwa teknolojia ya kale ingetafutiwa njia mbadala badala ya kuishia kuikarabati wakati tunajua ni zoezi lenye kushindwa.
Mungu watie wepesi wakaazi wa Kilosa.
Mafuriko yanazidi kufanya uharibu eneo la Magomeni Kilosa muda huu. Mji wa Magomeni umegeuka bahari na unaendelea kuangamia.

Last edited by a moderator: