MAGIC FM: Anayekunwa na anayekuna nani anasikia raha?

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
MagicFM wana tangazo lao ambalo husema anayekuna na anayekunwa nani anasikia raha????

if someone can read between the lines ni rahisi sana kuelewa kwamba hili tangazo ni matusi matusi, ingawa sio moja kwa moja lakini ni matusi.

Niliwahi kuandika kwa TCRA kutoa malalamiko haya, walinijibu kwamba watafanyia kazi. ni muda sasa umepita na hili tangazo bado linaendelea kupigwa.

inawezekana ni mimi tu nina tatizo na hili tangazo? Haiwezekani kuwa mbunifu bila kuweka lugha zenye viashiria vya matusi?
 
Si kila unayodhani matusi ni matusi ila matusi hutegemea wewe mwenyewe.
 
Vp na ile ya fupi tamu, ndefu inakera!!

Original comedi walikujaga na " nasikia raha , nasikia utamu"
 
Hata id yako kwangu ni tusi,nimwombe nani alishughulikie hili?
 
MagicFM wana tangazo lao ambalo husema anayekuna na anayekunwa nani anasikia raha????

if someone can read between the lines ni rahisi sana kuelewa kwamba hili tangazo ni matusi matusi, ingawa sio moja kwa moja lakini ni matusi.

Niliwahi kuandika kwa TCRA kutoa malalamiko haya, walinijibu kwamba watafanyia kazi. ni muda sasa umepita na hili tangazo bado linaendelea kupigwa.

inawezekana ni mimi tu nina tatizo na hili tangazo? Haiwezekani kuwa mbunifu bila kuweka lugha zenye viashiria vya matusi?

Kweli mkuu ni matusi matupu.
 
Mjukuu wangu, maneno hayo wameyatoa kwenye taarabu ya zamani kidogo. Imejaa tafsida, si rahisi kusema matusi moja kwa moja, lakini wako ni mtazamo. Kuna taarabu nyingi inasema, manahodha wa mashua kwanini wakae nyuma, ukisikia wimbo kwa kina utaona wanakemea tabia fulani katika mahusiano.

The comedy show ya EATV wanasema fupi tamu ndefu inakera, wote hao wameficha ujumbe wao na wanaelewana wao wenyewe. Inawezekana TCRA wanatafuta hoja za msingi katika kulishughulia jambo hilo. Tusi linategemea na mazingira, nenda shimoni kariakoo ukasikie lugha zao, nenda bandarini, wasikie mafundi wa TANESCO wakiwa site.

Hoja yako nimeielewa kwa mtazamo wako, lakini inawezekana isiwe sahihi kwa mitazamo ya wenzako. Ngoja tuwasubiri hao uliowashtakia wa TCRA.
 
Back
Top Bottom