Magic Builders International wamenifanya niendelee kuamini zawadi zitolewazo na makambuni ni za mchongo

Dkt Mwijuma

Senior Member
Apr 9, 2023
198
561
Kwanza polen na msiba ndg zangu

Ilikuwa ni tarehe 18 ya mwezi wa pili pale viwanja vya Tunza Beach jijini Mwanza mbele ya mbunge wa Ilemela mama Mabula

Kampuni ya Magic Builders International walifanya semina ya mafundi rangi na wakawa wametoa simu kumi na tano pamoja na pikipiki tano kwa mafundi

Kuna mda sikuwa naamini lkn, kuna watu waliopewa zawadi nikawa nawafahamu, ikapelekea nianze kuamini kuwa ni kweli zawadi sio za kupangana wala mchongo

Lkn siku zinazidi kwenda baadhi ya waliopewa zawadi sioni wakizitumia, ikumbukwe pikipiki zilikuwa na stika za kampuni hivyo hazijifichi, mpaka leo naandika ni tarehe 1 mwezi machi sijaona pikipiki hata moja kati ya zile tano ikitumiwa na fundi

Maanake ni kwamba huenda walipangwa wapewe then wazirudishe ndio maana hawazitumiii
 
Back
Top Bottom