Maghufuli ''is next level''

Binafsi namkubali sana MAGUFULI kwa utendaji wake.Tungekua nawaziri kumi na moja tuu kama huyu Tanzania ingekua kisiwa cha maendeleo na uchumi wa kuigwa hapa EA na Afrika kwa ujumla. Ila siipendi CCM
 
Kuna ukweli wa kiasi fulani katika hoja zako lakini pia ni ukweli kuwa Magufuli anahudumia serikali ya kifisadi! Hivyo anadumisha ufisadi Tanzania!
 
Ni waziri anayetambua kwa nini sisi ni masikini ilhali tuna rasilimali chekwa, samaki milioni+++, dagaaa+++ na mifugo ya kufa mtu. Japo huwezi kumfananisha na PK wa Rwanda, jamaa anajitahidi kusimamia anachoamini. Hutaki, PIGA MBIZI
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wanaomchukia Magufuri ni wale waliozoea kuambiwa hamna taabu huo ni moshi tu hata kama nyumba inaungua. Kwa kifupi ndani ya CCM hakuma kiongonzi anayeweza kukiokoa chama chao zaidi ya Magufuli.
 
Ukweli ni kwamba Magufuli ni mchapakazi, mfutiliaji, anajiamini, hana woga wala longolongo, haoni haya kuwaonea haya wazembe, wavivu, wezi na wadanganyifu. Katika CCM ya leo, Magufuli anaweza kabisa kuuzika na kukubalika kwa wananchi.[/QUOT

I gree with you, kweli hakunaga kabisa kama Dr.Pombe Magufuli.mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Ni juzi tu kashinda kesi ya samaki na kutaifisha meli......big up pombe
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wanaomchukia Magufuri ni wale waliozoea kuambiwa hamna taabu huo ni moshi tu hata kama nyumba inaungua. Kwa kifupi ndani ya CCM hakuma kiongonzi anayeweza kukiokoa chama chao zaidi ya Magufuli.

ndugu taratibu, huu ukweli wapiganaji (al shabaab!?) hawataki kuusikia kabisaaa.. atalishwa sumu ntuu bureee...
 
Nani Kama John Pombe Magufuli..,
1.Kiongozi mchapakazi anayejituma
2.Kiongozi ambaye hajajilikimbizia mali, tujiulize magufuli anamiliki kampuni gani..?
3.Anatanguliza mbele maslahi ya Taifa, na maslahi ya chama. kwani hajihusishi na makundi kuleta mgawanyiko katika chama
4.Kiongozi anyesimamia ukweli na mwenye msimamo thabiti..!
5.Kiongozi huyu hatumii pesa kujisafisha au kujijengea njia kuwa raisi 2015, zaidi ya uongozi wake bora na sio kumwaga fedha na kuunda mitandano au makundi
6.Anajiamini (self confident) hatawachekea mafisadi na wazembe serikalini, na hata wananchi wavivu na wabishi mfano wa kigamboni waliombishia kuhusu nauli, watanzania tunapendwa kubebwa kila wakati kwenye sehemu ambako hatubebeki, ndio chanzo kikubwa cha umaskini
7.Ni mfuatiliaji mzuri wa matatizo, kama alipanda lori na kujifanya abiria kukamata wanaochukua rushwa kwenye mizani,..kiongozi gani ambaye atakuwa tayari kufanya jambo kama hili serikalini..? zaidi ya kuandaa warsha na vikao kutatua matatizo

Napenda kumfananisha John Magufuli na Paul Kagame, kwa style zao za uongozi bora na kupambana na ufisadi,rushwa na hujuma dhidi ya taifa...!

Magufuli ameweza kuwa mtu pekee mwenye kukiletea heshima chama cha mapinduzi (ccm), kama kufanikisha ushindi Igunga,na pia atakuwa ndio striker kwnye uchaguzi Arumeru..,kweli anatimiza Ilani ya CCM kwa asilimia 100..!

Watanzania Kama tunapenda maendeleo, tumpe moyo viongozi kama hawa wenye kujituma na kutetea maslahi ya Taifa...!
Ningepanda nishauri Mh.John Magufuli apewe Ulinzi maalumu maanake wasije wakamfanyia mabaya hasa wale wanaokamia urasi 2015..! kwakuwa wanaamini ni tishio kwao



Unaposema ni kiongozi mchapakazi una maana gani kwamba anaotoa uongozi shirikishi na kushiriki kutekeleza kanuni za kazi na au anatekeleza propaganda za CCM. Nafikiri la pili ndio sahihi kuwa anatumia raslimali za serikali kubwa na nyeti kwelikweli kukimbizana na vitu vidogo. Kwenye nchi iliyojaliwa rasmimali za kutosha angehamasisha kuzalisha mitaji ya ndani isiyokuyowa na riba na kuitumia kubuni, kutengeza miundo mbinu na kuhifadhi iliyopo. Lakini he's another mouthy emperor seeking media publicity na ndio maana anatumia misaada yenye masharti magumu na yenye maumivu makali kwa vizazi vilivyopo na vijavyo kutengeneza miundo mbinu ambayo iko outdated. Wakati majirani zetu wanakibizana na barabara za juu (flyovers) na three to four lanes mwenzetu anabaki domokaya wa vichochoro, kuondoa service roads ili kuongezea kipande cha barabara na zenye viwango duni.

2. Unaposema hajimbikizii mali unamliganisha na nani? Usimlinganishe na maskini mwenye kipato kisichompeleka katikati ya mwezi ukasema hajilimbikizii mali. Kuwa na adabu na mwenye upeo. Unataka akutajie ana hard cash kiasi gani bank? Unataka akwambie anayo mashamba mangapi Tanzania na nyumba ngapi, mbuzi wangapi, ngo'me wangapi ili uone hajilimbikizii mali? Ile nyumba ya serikali aliyochukua kwa bei ya kutupa unaona ni haki, upendo na hofu ya Mungu?

3.Naona hujuiani maslahi ya nchi ni yepi. Uwe CCM na uwabeze wanaoikosoa CCM useme kuwa unasimamia maslahi ya nchi.Nchi ipi? Ina maana maslahi ya Tanzania ni kuwa shamba la bibi? Maslahi ni mikataba tata? Maslahi ni kuijiuzia nyumba zetu kwa bei ndogo na msilipe? Maslahi hayo kwa nani? Kujifanya anasimamia sheria bila sense of reasonability. Kiongozi huwa ni reasonable, critical minded, proactive, simple, devoted na awe na self negation na reservation. Haya siyaoni kwa Magufuri bali naona mtu mwenye majivuno, intellectually pompous, mechanical type of manager with fire brigade management
 
Mdau anamfahamu Magufuli kwa aliyoyataja hapo juu. Wewe unayemfahamu kwa upande mwingine weka hadharani unayoyafahamu tumpime. Hatutaki porojo hapa lete facts.

1) Amefanikiwa kuondoa foleni za magari katika barabara za jiji la DSM ndani ya miezi miwili tangu alipokabidhiwa wizara kama allivyoahidi
2) Amefanikiwa kujenga fly overs kadhaa tangu awe waziri wa wizara yake kama alivypoahidi. n.k. hongera sana
 
Mmedanganyika tena?

Nipeni msimamo wa magufuli kuhusu
1/ wezi wa epa
2. Wizi wa deep green
3. Nyumba za serikali alizowauzia vimada wake akina stella
4. Wizi wa richmond
5. Etc etc
huyu ni debe tupu kamaalivyokuwa mrema lyatonga, kila zama na debe lake. Wakati utawala unapokuwa hafifu na laghai kama uliopo, manabii wengi wa uongo kama magufuli huvuma, utwajuaje manabia i wa uongo

1. Huwa wanapenda kutembea na wandishi wa habari hata bila sababu
2. Wanaepuka kuwachukiza watawala waliopo, wanaepuka kuzungumzia wizi wa epa kwa kuwa jk atachukia
3. Wanazungumzia tu vidagaa kama wezi kwenye mizani, kubomoa nyumBa za maskini kando ya baranra, hata siku moja hutamsikia magufuli akizungumzia kuhusu wawekezaji wanaowatesa wananchi


chunga sana watu wa namna hii, ukombozi wa kweli utaletwa na watu makini na si wapemda sifa na kutukuzwa
 
Wakenya wanazindua fly overs march 12th, 2012! Mnamo miaka 2 iliyopita nairobi ilikuwa haifai kwa foleni leo wanaachana na foleni, endeleeni kusikiliza alinacha za maghufuli! Ohoo!
 
Nani Kama John Pombe Magufuli..,
1.Kiongozi mchapakazi anayejituma
2.Kiongozi ambaye hajajilikimbizia mali, tujiulize magufuli anamiliki kampuni gani..?

Hivi unajua unachoandika au unabwabwaja tu? Katika Serikali ya CCM hakuna MSAFI hata mmoja. Jiulize kwanini Magufuli hakemii UFISADI?

Hivi ulishafika Chato katika jimbo lako? Magufuli ana Estates ya nyumba zipatazo 30. Baadhi ya nyumba hizo ndiyo maofisi ya Idara mbalimbali za Wilaya ya Chato. Jengo la Mkuu wa wilaya na Makazi yake yamejengwa kwenye mashamba ya Magafuli? Muulize Magufuli mwenyewe kama anaweza ku-account huo UFIASDI wake. Ndiyo maana hata siku moja hutamsikia Magufuli akikemea UFISADI sahau kabisa. Ulizeni watu wa Chato watawaeleza Magufuli ni mmoja wa mawaziri matajiri sana.

Achilia mbali hilo la kuuza nyumba zetu hadi akafikia kumuhonga kimada wake SUNDI ambaye wakati huo alikuwa sio mwajiliwa wa Serikali alikuwa mwanafunzi chuo cha ARDHI.

CCM HAKUNAGA MSIDANGANYIKE.
 
Yaani hata mkimsifia vipi huyu waziri mie wala siungi mkono hoja kwa sababu moja kubwa nayo ni kuvalia njuga uuzwaji wa nyumba za serikali! Muda si mrefu Oysterbay itakuwa kama manzese maana kila mtu anaongeza majengo ki mpango wake!
 
Back
Top Bottom