Maghorofa ya Lugumi kupigwa mnada kesho

Maghorofa ya Lugumi kupigwa mnada kesho

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Kampuni ya Udalali ya Yono kesho itapiga mnada maghorofa yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi.

upload_2017-9-8_14-41-1.gif


Maghorofa hayo mawili ambayo yapo sehemu tofauti moja likiwa mtaa wa Mazengo Upanga na lingine likiwa Mbweni jijini Dar es Salaam..

Mkurugenzi wa Yono, Scolastica Kevela amesema leo Ijumaa kuwa wametumia njia mbalimbali ili kufanikisha mnada huo kufanyika hasa kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Amesema hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) hivyo hao ndio wanaoweza kutoa majibu hayo.

"Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndio wanatakiwa kutolea majibu,"amesema Kevela.

Amesema fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo
 
Watu wanahofia kujitokeza kununua maana na wao pia wataanza kufatiliwa account zao,biashara zao
 
Hayajajengwa kwenye hifadhi ya barabara kweli naweza kuingia mkenge.
 
atanunua kwa mgongo wa ndugu yake .. labda huyo ndugu amdhulumu
 
Back
Top Bottom