Usanii tu Mkuu. Chama kinachotoa rushwa kwa Wabunge wake ili wapitishe muswaada uchwara kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinadhani bado tuko kwenye mfumo wa chama kimoja na hivyo kutoiheshimu katiba ya nchi kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinapora bilioni 16 za wahanga wa tetemeko kamwe hakiwezi kubadilika. Chama kinachodai kwamba mahakama ya ufisadi kutokuwa na kesi ni ishara nzuri wakati kuna mafisadi chungu nzima ambao hawaguswi na mkono wa sheria kamwe hakiwezi kubadilika.