Magesa Mulongo: Amani kwanza haki baadae

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
akihutubia baraza la madiwani na watendaji wa halmashauri ya meru katika ufunguzi wa tovuti ya halmashauri hiyo mkuu wa mkoa wa arusha ndg Magesa Mulogo amesema hakuna haki bila amani hivyo ameaonya wananchi kufuata sheria na kudumisha amani kabla ya kudai haki zao.amesisitiza kuwa huwezi kudai haki iwapo hakuna amani.

Source:mimi mwenyewe kutoka eneo la tukio.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
jf great thinkers mnaonaje kauli hii?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Magesa hawajui wameru, mwambie amuulize yule mkuu wa wilaya ya arumeru yule mama aletoka majuzi kwa nini kakimbia??

Na amuulize huyu dogo wao DC mpya ni nini amekutana nacho kwenye Sensa.

Nduu Weeera Kiinya.
 
Out of touch, out of reality!!!!!

Mkuu wa Mkoa wa karne ya 21 anathubutu kubariki udikteta,

Unbelievable
 
Haki ndiyo inaleta Amani. Hata hivyo sishangai sana kwasababu ni mmoja wa watu bogus waliopo ktk utawala huu.
 
Huyu Mulongo ni mtu wa aina gani? mbona ni kama kijana tu na ni msomi? Iweje atoe kauli kama hii wakati kinyume cha kauli yake ndiyo ukweli yaani hakuna amani pasipo haki.
 
Magesa hawajui wameru, mwambie amuulize yule mkuu wa wilaya ya arumeru yule mama aletoka majuzi kwa nini kakimbia??

Na amuulize huyu dogo wao DC mpya ni nini amekutana nacho kwenye Sensa.

Nduu Weeera Kiinya.
mia pupy kumbe ulikuwepo pale shule ya muungano usa river wakati makarani wanamtolea uvivu
 
Haki ni mama wa amani,
Haki kwanza ndo amani itafuatia.
Wimbo wa amani umetumika mda mrefu ili kupumbaza haki.
Nachukia sana lile neno 'uvunjifu wa amani'.
Ewe magesa, sisi tunapinga 'uvunjifu wa haki'.
Haki ikitendeka automatically amani itakuwepo.
Haki ni mama wa amani.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sisi ni wapambanaji wavamagwanda kazi yetu kupambana. Huo wimbo wa amani waachieni CCM.
 
Utakuwaje na amani wakati huo huo huna haki yani eti unaamani af hapo hapo uwaza kama utapata kitufulani sasa hapo amani utakuwa nayo kweli?
 
Hiyo aende akawahutubie kuruta jeshini, ambao wanatakiwa watekeleze adhabu kwanza ndio baadae wajitetee.
B.um.b.a.f.f!!!
 
Sidhani kama alishawahi kudhulumiwa haki yake, zaidi yeye kawadhulumu watu. Aibu kwa Rc kutoa kauli isiyo na hadhi.
 
Sisi ni wapambanaji wavamagwanda kazi yetu kupambana. Huo wimbo wa amani waachieni CCM.

Hahahha,ningekuwa ni wewe ningeficha welevu wangu.....kwani una macho huoni,una masikio husikii, kuna msemo mmoja wa kikwetu unasena...kwigwa kwa mbulu mpaga mininga mmatu....
 
Huyu Mulongo ni mtu wa aina gani? mbona ni kama kijana tu na ni msomi? Iweje atoe kauli kama hii wakati kinyume cha kauli yake ndiyo ukweli yaani hakuna amani pasipo haki.

Labda hayo ndiyo maagizo ya zile semina elekezi. Most of these appointees reflect dictatorship type of leadership but they are not openly (as their appointments are public for public office) reprimanded nor demoted!!! Why?
 
Achaneni na huyo kilaza...ndiyo maana yuko CCM. Binadamu anatakiwa achume kwanza juani ndio aweze kula kivulini.

Justice seeker is a peace maker.
If you know justice, you know peace.
Peace is not the absence of war, it is the presence of justice.
Without justice, there can be no peace - Martin Luther King Jnr.
 
Back
Top Bottom