Magesa akanusha kufuga chatu Nyumbani kwake

Magesa akanusha kufuga chatu Nyumbani kwake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,455
Mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha kwamba nyoka aliekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na imani za kishirikina, ameuwawa na Wananchi. Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipandevipande ambapo baada ya hizi taarifa kusambaa mmiliki
wa nyumba hii aliomba kuongea na mtandao wa ili kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe. millardayo.com

Mr. Joseph Paschal Magesa anasema "Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi na mzee wa kanisa na niliondoka nyumbani jana na mke wangu kutoka
Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho kitu ila nilipofika maeneo ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka
huku ndani ya eneo la garden nyumbani, kuna vijana niliwaacha wawili pale nyumbani nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo nyoka'
‘Wakamuita jirani yangu hapo ndipo nae akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua ametekeleza kumbe aliondoka, baadae napiga tena simu nauliza vipi naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia wamemvuta mkia wamemuweka nje ya geti' ‘Nikawauliza anavutika asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata ndo ikawa mwisho wake hapo'.

‘Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza….. sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu angekufa na yeye? mimi nasema namwachia Mungu tu sijawahi kusikia Nyoka kuishi maeneo hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8,
hata na mimi inanitatiza manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa chenye maandishi mekundu kama ya kiarabuarabu hivi' ‘Taarifa kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani, hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikifunja mimi wakati napanga mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu'
 
Ukweli unaufahamu wewe na mungu wako.. Mengine ni ya kufurahisha baraza tu..
 
wale waliobaki ilikuwa mmoja atolewe kafara,wamshukuru Mungu kwa kweli kawaokoa
 
Mmiliki wa mojawapo ya
nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha
kwamba nyoka aliekua akimfuga kwa
siku nyingi na kuhusishwa na imani za
kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha
kumkata kata vipandevipande ambapo
baada ya hizi taarifa kusambaa mmiliki
wa nyumba hii aliomba kuongea na
mtandao wa ili kutoa
maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli
wenyewe.
millardayo.com
Mr. Joseph Paschal Magesa anasema
"Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi
na mzee wa kanisa na niliondoka
nyumbani jana na mke wangu kutoka
Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui
lolote kuhusiana na hicho kitu ila
nilipofika maeneo ya Mwanga na Same
nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka
huku ndani ya eneo la garden nyumbani,
kuna vijana niliwaacha wawili pale
nyumbani nikawaambia waambieni watu
wawasaidie kumuua huyo nyoka'
‘Wakamuita jirani yangu hapo ndipo nae
akanipigia simu nikamwambia bwana
wewe si una bunduki nisaidie kumuua
huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua
ametekeleza kumbe aliondoka, baadae
napiga tena simu nauliza vipi naambiwa
bado yupo na watu wamejaa nikawauliza
kwani hao watu hawawezi kumuua
mpaka bunduki wakasema wanaweza
ndio baadae wakanambia wamemvuta
mkia wamemuweka nje ya geti'
‘Nikawauliza anavutika asije akawa
analeta shida wakasema anavutika,
nikawaambia mpelekeni kanisani kwa
sababu nyumbani kwangu ni jirani na
kanisa ndio wakamvuta hadi kanisani
wakammwagia maji ya baraka kisha
wakamkatakata ndo ikawa mwisho wake
hapo'.
‘Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba
huyu nyoka ni mtoto wangu wa
kwanza….. sasa kama ni mtoto wangu wa
kwanza si inamaana na mtoto wangu
angekufa na yeye? mimi nasema
namwachia Mungu tu…….. sijawahi
kusikia Nyoka kuishi maeneo hayo toka
nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8,
hata na mimi inanitatiza manake
nimetumiwa picha Nyoka amefungwa
kitambaa chenye maandishi mekundu
kama ya kiarabuarabu hivi…..'
‘Taarifa kwamba Nyoka huyu amevunja
kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo
kitu eti kwamba ametokea ndani, hayo ni
mambo ya watu tu… hicho kioo nilikifunja
mimi wakati napanga mizigo ya ofisi
yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu
Nyoka, Watanzania waniamini haya
ninayosema ndio yanayotoka moyoni
mwangu'

Pole sana, uwezi kusingizia na jamii yote ile, Usijisafishe "Mara nyingi ni ngumu kusikia Mwizi akikubali kosa la kuiba, ama mtuhumiwa akikiri uovu wake"
 
Pole sana, uwezi kusingizia na jamii yote ile, Usijisafishe "Mara nyingi ni ngumu kusikia Mwizi akikubali kosa la kuiba, ama mtuhumiwa akikiri uovu wake"

Wakat anasema wasimuue ni mtoto wake wa kwanza,naona alikuwa amechanganyikiwa sana, ikabid aseme ukwel, sasa iv tena anasema aliomba wampige bastola wamuue mmh
 
Kwanini yeye na mke wake waondoke kwenda Dar, na nyoka atokee huko home? Kuna ukweli upo nyuma ya pazia..mengi tutayajua tu!
 
Wakat anasema wasimuue ni mtoto wake wa kwanza,naona alikuwa amechanganyikiwa sana, ikabid aseme ukwel, sasa iv tena anasema aliomba wampige bastola wamuue mmh

Dahh hapo sasa!!Warumi upo poa??
 
Watanzania tuache imani potofu, kila kitu tunawaza ushirikina. Hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu kamwe , kwa nini tusiwaze tu positive, jamani tubadirike.
 
Simba akila mtu watu hawashangai na wanaona ni kitu cha kawaida! Lakini Mtu akila Simba inakua ni historia! Najuta kuzaliwa Tanzania!
 
watanzania wanaweza kukusingizia kitu na wakaishi kama ni ukweli kabisa, inauma acheni nyie
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ukweli anaujua magesa mwenyewe, si sawa kusema kwamba magesa ni mshirikina, naomba kuuliza tuna hakika gani na chanzo cha hii habari? je aliyesema kuwa magesa aliagiza kuwa nyoka asiuliwe kwa kuwa ni mtoto wake wa kwanza alisema kweli?
Utetezi wa magesa unaweza kuwa ni wa uongo hata kama tuhuma anazopewa ni za uongo, kwani anafanya hivyo ili kuficha aibu ambayo ni ya uongo, ama akawa anajitetea kuficha ukweli na aibu.
Kama wafanyakazi tu hawajui kuwa kulikuwa na joka, ina maana ni hiyo ni siri ya magesa.
 
Mimi namuamini Magesa kwa sababu hata nisipomuamini haita niongezea wala kunipunguzia kitu.
 
Back
Top Bottom