Magereza wamwaga ajira

Jerry santonga

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
642
550
Habari za nelo waungwana japo ucku mwangaruka bankima na bagosha....kama we ni kidato cha nne au cha sita bac magereza hao wameachia nafasi unaapply vp we zama moha.go.tz
 
na wote watapishwanishwa na vituo waivyojiandikisha maana watakuwa depo
 
Nasikia hakuna kitu kama hicho kinachoendelea Magereza. Ni watu wamezusha kwa kuchukua tangazo la ajira mwaka jana wakalizungusha. Mleta Uzi fuatilia hilo kwa uhakika zaidi.
 
rafiki yangu yuko magereza alinieleza kuhusu hizi nafasi ila nilipomwambia anionyeshe zilipotangazwa alinionyesha za mwaka jana kwahiyo ndugu zangu hizi nitetesi zizokua na ukweli wowote
 
JESHI la Magereza limetangaza nafasi
mbalimbali za ajira katika jeshi hilo ambapo
watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo ya awali
ya askari magereza yatakayoendeshwa na Chuo
cha Magereza Kiwira, Tukuyu Mbeya.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamishna wa jeshi
hilo, John Minja, ilisema kuwa mwisho wa
maombi hayo ni Oktoba 15 mwaka huu.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa watakaofanikiwa
kuitwa katika usaili watajulishwa kupitia tovuti ya
Jeshi la Magereza. www. magereza. go. tz,
magazeti na katika mbao za matangazo ofisi za
wakuu wa magereza wa mikoa na bwalo kuu la
maofisa wa magereza lililopo Ukonga jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwombaji anatakiwa
kuwa raia wa Tanzania na kwamba awe na sifa
mbalimbali ambazo ni pamoja na kutoajiriwa
katika taasisi yoyote ya Serikali.
Sifa nyingine ni kwamba, asiwe ameoa au
kuolewa na wala asiwe na mtoto. Mwombaji
ambaye ni mhitimu wa shahada ya kwanza
anatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18
hadi 28 na wasiokuwa na shahada wawe na umri
18 na 24.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, mwombaji mvulana
awe na urefu usiopungua sentimeta 170.2 au futi
5 na inchi 7 na msichana awe na urefu
usiopungua sentimeta 167.64 au futi 5 na inchi 4.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, mwombaji ambaye
amehitimu elimu yake kati ya mwaka 2012 hadi
2014 awe na afya nzuri iliyothibitishwa na daktari
anayetambulika kisheria.
Taarifa hiyo ilizidi kufafanua kuwa, mwombaji
awe hajawahi kushtakiwa au kupatikana na kosa
lolote la jinai pia awe na tabia na mwenendo
nzuri.
Ilibainisha kuwa awe na shahada katika fani au
taaluma mbalimbali ambazo ni pamoja na
shahada ya sheria, utekelezaji wa sheria,
takwimu, uchumi na mipango, mazingira, usanifu
majengo, ukadiriaji majengo, mipango na
usimamizi wa miradi, uhandisi wa umeme,
uhandisi wa mitambo ya kilimo na tiba ya
mifugo.
Taaluma nyingine ni pamoja na misitu, uchumi,
kilimo, bima, uhasibu na usimamizi wa vyama vya
ushirika, uhandisi mazingira, sayansi na
kompyuta, udaktari wa binadamu, ualimu wa
masomo ya sayansi, kama fizikia, kemia, hisabati
na baiolojia.
Ilibainisha kuwa mwombaji awe na taaluma ya
ualimu wa masomo ya biashara na Kifaransa.
Ukutubi, mahusiano, biashara na masoko.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwombaji mwenye
stashahada (Diploma) anatakiwa kuwa na cheti
ambacho chuo chake kinatambulika na Serikali.
Mwombaji huyo anatakiwa kuwa na fani au
taaluma mbalimbali ambazo ni pamoja na
ukutubi, biashara na mipango, bima, uhasibu na
usimamizi wa vyama vya ushirika.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, taaluma nyingine ni
pamoja na Mipango na Usimamizi wa Miradi,
Utabibu, Uuguzi, Maabara na Mazoezi ya Viungo,
Uhandishi wa Habari, Ufundi Magari, Ujenzi,
Umwagiliaji, Mitambo ya Kilimo, Umeme, Usanifu
Majengo, Ushauri Nasaha, Uhandisi Mitambo,
Sanaa na Muziki, Ualimu wa Masomo ya
Biashara, Uchumi na Kifaransa,
Mwombaji mwenye astashahada anatakiwa kuwa
na fani mbalimbali ambazo ni pamoja na cheti
cha majaribio ya ufundi katika fani za Uhandisi
Maji, Ujenzi, Ufundi Magari, Umeme wa Magari,
Waunganishaji Nondo.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa fani nyingine ni
pamoja na Useremala, Bomba, Rangi, Ushonaji,
Utengenezaji Sabuni, Ufumaji, Utengenezaji
Viatu, Maabara, Muziki na Utamaduni, Uuguzi na
Ukunga, Utabibu Msaidizi.
Taarifa hiyo iliwataka waombaji kuzingatia
masharti yaliyotajwa ikiwa watabainika
wamefanya udanganyifu wowote ikiwamo wa
kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu maombi
yake yatatupwa.
Ilibainisha kuwa mwombaji ambaye atagundulika
alifanya udanganyifu huo baada ya kupatiwa
ajira, jeshi hilo litasitisha ajira yake, kuachishwa
kazi na kufikishwa mahakamani.
Taarifa hiyo iliwataka waombaji kuwasilisha
maombi yao moja kwa moja kwa Kamishna
Jenerali wa Magereza, Makao Makuu ya
Magereza kwa kutumia sanduku la posta 9190.
Ilieleza kuwa barua zote ziambatane na nakala
zote za elimu, ujuzi, cheti cha kuzaliwa cha
mwombaji pamoja na picha ndogo mbili za hivi
karibuni.
Vyeti halisi vitatakiwa kuonyeshwa wakati wa
usaili, hati ya mitihani haitapokelewa isipokuwa
kwa wahitimu ambao vyeti vyao havijatoka katika
vyuo husika pekee.

acha uongo hakuna kitu kama hicho ni tangazo la mda mrefu na mkuu wa kitengo ameambiwa akanushe habari hii na wenda itakanushwa soon
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom