Mkuu nahisi hamko serious, enzi za kuchagua kazi hasa hizi za majeshi ziliishapita siku nyingi sana. Lakini pia kama sikosei ule utaratibu wa kuajiri JWTZ moja kwa moja ni kama umesitishwa(mtanikosoa) wanachukuwa recruits kutoka JKT, so kwa mwenye bahati na godfather anachukuliwa kujiunga na JWTZ kwa wale wanaobaki kuna wanaopata ajira ya kudumu kwenye JKT na waliosalia tunakutana nao mitaani. Kwa upande wa Jeshi la Magereza nadhani bado wana utaratibu ule wa zamani wa kuchukua maoja kwa moja recruits kutoka mtaani-nahisi inaweza kuwa rahisi kucheza karata zako ili uchaguliwe.
Upande wa mafunzo siwezi ksema sana maana kama wengine wanamaliza iweje dogo ashindwe- anaweza wala asihofu. Mimi nachojua watu tunaangalia maslahi kwanza kabla ya ugumu wa kazi. Kiukweli JWTZ wanalipwa vizuri kuliko Magereza, hili liko wazi.
So, mi namshauri dogo kama anataka kazi asiwaze ugumu wa kazi, yeye akomae tu. Lakini pia kama anataka ulaini wa mambo mwambie arudi shule.