Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,155
- 128,815
Naunga mkono hoja. Kwa kadri watu wanavyopigika, ndivyo uhalifu unavyoongezeka, badala ya serikali yetu kuongeza magereza, wange invest kwenye kuboresha uchumi, watu wapunguze kupigika, vibaka wapungue.Inasikitisha sana wakati wenzetu ulaya magereza yanakosa wafungwa wanayafunga na kubadilisha matumizi.Gharama ya kujenga hayo magereza wangefunga cctv kila mji.Pia kuwekeza katika elimu mikoa ya ziwa victoria penye mauaji kila siku
Pia serikali iwekeze kwenye elimu ya uraia ya good citizenship, na adhabu mbadala, badala ya kuwafunga mwizi wa kuku, unampatia shughuli ya kumuingizia kipato kumuweza kununua kuku ale.
Wafungwa waliojazana magerezani, wapewe adhabu mbadala, watumikie vifungo vya nje.
Kanda ya ziwa, wale jirani zetu wanaopenda kuuana kwa wivu wa mapenzi, wapewe tuu semina za upendo, hata ukimkuta mwizi wako anakula mali zako, usimuue kwa hasira, msubiri tuu amalize, na kumruhusu aende zake tuu bila kumfanya chochote,, kwa sababu hata ale vipi, hawezi kumaliza, chakula cha kuwatosha wote mshibe bado kinakuwepo, na vyakula vingine sio big G kusema itaisha utamu, akimaliza kula, mpe muda wa kumpumzika, na wewe utaendelea kufaidi tuu, kwa sababu utamu haushi, na habandui kuondoka nayo, na kuna vitu vingine, hakuna makombo, hivyo mauaji ya wivu wa mapenzi, yatakwisha.
P

