KIHINGA -KIGOMA
Yote hapo juu cha mtoto,Kihinga habari nyingine kabisaaa.
Mbali na mziki mnene wa Jela yenyewe,bado kuna Mashamba yao hasa yale ya Michikichi,Full Nyoka,tena Nyoka wa maana hasa na aina zote,na haitakiwi kuuwa nyoka hata mmoja.
Kuna watu wanaona bora akijipiga panga ajikate kidole ili asiende shift.Hahaha na ukirudi jela unakumbana na mziki mkubwa.Wengi wakitoka huko ni Maiti na akiwa mzima basi kichwa kibovu ua anakuja kufia uraiani.
Maana anakuwa Anashangaa jinsi watu uraiani wanavyoishi,basi unakuta muda wote kaduwaa kama vile katoka sayari ya Jupiter,hahaha
Waliofungwa miaka ya 90 huko wanalijua hili,sijui kama shows zake zipo kama ilivyokuwa.Maana mpaka wafungwa wachawi wamo humo,hahaha aisee we acha kabisa huko Balaaa