GE2025 Magdalena Rwebangira ametoa wito kwa Watendaji wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na miongozo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Magdalena Rwebangira, ametoa wito kwa Watendaji wa Uchaguzi kuhakikisha wanafuata kwa umakini Katiba, sheria, kanuni na miongozo yote inayosimamia mchakato wa uchaguzi nchini

Akizungumza akiwa Tabora wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya mikoa na majimbo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Mhe. Rwebangira amesisitiza umuhimu wa uelewa sahihi wa nyaraka za uchaguzi ili kuepusha mkanganyiko na changamoto zisizokuwa za lazima

"Someni kwa umakini katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizieni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine kutakuwa na changamoto" alisema Rwebangira

Pia amewakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuibua malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa au wadau wengine wa uchaguzi, akisisitiza kuwa uteuzi wa watendaji wa vituo uwe makini, ukizingatia maadili, uzalendo na weledi badala ya kuendekeza upendeleo wa kifamilia au kiundugu.

Mafunzo haya ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo watendaji kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, na yanatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 17, 2025

tume.png

Chanzo: ITV
 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Magdalena Rwebangira, ametoa wito kwa Watendaji wa Uchaguzi kuhakikisha wanafuata kwa umakini Katiba, sheria, kanuni na miongozo yote inayosimamia mchakato wa uchaguzi nchini

Akizungumza jijini Tabora wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya mikoa na majimbo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Mhe. Rwebangira amesisitiza umuhimu wa uelewa sahihi wa nyaraka za uchaguzi ili kuepusha mkanganyiko na changamoto zisizokuwa za lazima

"Someni kwa umakini katiba, Sheria, Kanuni, miongozo na Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizieni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine kutakuwa na changamoto" alisema Rwebangira

Pia amewakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuibua malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa au wadau wengine wa uchaguzi, akisisitiza kuwa uteuzi wa watendaji wa vituo uwe makini, ukizingatia maadili, uzalendo na weledi badala ya kuendekeza upendeleo wa kifamilia au kiundugu.

Mafunzo haya ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo watendaji kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, na yanatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 17, 2025

mwambieni hakuna atakaeenda kupiga kura,
 
Back
Top Bottom