Magazeti yetu yamekuwa hovyo

Magazeti yetu yamekuwa hovyo

UDOM ilijengwa na fedha za NSSF sasa jiulize marejesho ni shilingi ngapi ? Badala yake magazeti ya hovyo yanakuja na habari za kutimuliwa Mkurugenzi Mkuu.Pengine Magazeti yanataka kuaminisha wasomaji wake tatizo ni Irene na si serekali inayokopa bila utaratibu wa kurejesha.Daraja la Nyerere fedha za NSSF jiulize kiasi gani kimerejeshwa ?.
Na ule mradi bubu Dege kigamboni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ngongo, kwanza naunga mkono hoja,

Tanzania tuna a very serious problem kwenye media zetu, hatuna waandishi na wahariri competent wenye uwezo wa kufanya news analysis.

Mfano jana kama mlimsikia waziri Mhagama na Mkurugenzi wa SSRA kuhusu reasons za kikokotoo kipya ni hali mbaya ya mifuko ya PSPF na LAPF, baada ya kufanywa kwa actorial valuation ya afya ya mifuko hiyo, na ikabainika ilikuwa ife kufuatia formula yake ya 1/500.

Kwa vile mifuko hiyo miwili tayari ilikuwa on death bed, na sasa imekuwa merged into PSSSF, ili kuizuia PSSSF isife, baada ya jana rais kukirudisha kikokotoo cha zamani kilichokuwa kiuwe mifuko hii, ilitegemewa serious media ije na analysis of what does that mean.

Media zetu nyingi uwezo wake ni news reporting tuu na sio news analysis na hili niliwahi kulizungumza humu.

Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa Habari, News Analysis-Jicho Letu - JamiiForums

P

Ahsante sana Ndugu Pascal nilifikiri pengine ni Mimi nimeuona huu upumzike wa vijarida vyetu kumbe tuko wengi.
 
Hakuna Cha kumuogopa Rais wala nini
Tanzania Hakuna Waandishi competent kuanzia Habar Za uchunguzi, Uchambuzi wala Za burudani

Tuna reporters wa Matukio tu
Fungueni vyuo vya uandishi au katuleteeni hao wazuri toka Rwanda na India
 
Yule Azori Gwandu si alitaka kuandika habari za kiuchunguzi comprehensively? Jambo lililompata sote tunalijua

Kwa ukongwe wako kwenye tasnia ya uandishi utakua unamkumbuka marehemu Stan Katabalo and what was his fate. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Uhuru wa kuchunguza unamipaka tena mipaka mingine ni ya siri na ya hatari sana
Watu wanafiki wanajitoa ufahamu,watu wapo na wana uwezo sasa je mnawapa uwanja mpana kuyaonesha wayajuayo.Nani anataka kufa.
 
Ukitaka kufanya analysis data zako utazipata wapi? Umeshachunguza websites za mashirika ya Tz ukaona jinsi zilivyo? Nyingine data zake ziko miaka hata mitatu au zaidi nyuma. Kama utatumia data nyingine sheria ya takwimu inaweza kukufunga. Ukifanya analysis ya kuonyesha weaknesses unaweza kujikuta kwenye shida. Unakumbuka mambo yaliyompata yule kijana aliyepiga picha za "expansion joints"? Hiyo ilikuwa picha tu. Sembuse uje kufanya analysis ya ku reveal uzembe mkubwa au ufisadi? Kwa hiyo kama wewe ni mwandishi wa habari kwa nini ujitie kwenye shida wakati ukiandika habari za matukio tu familia yako itaishi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Ingependeza kama mtoa mada angeandika vichwa vya habari vilivyoandikwa na wahariri wa magazeti aliyoyataja. 2. Mimi sijawahi kukisikia kikokotoo cha 1/500 akichokitaja Paschal Mayala.Labda, lakini kama sivyo basi hakuna mwandishi wa kumcheka mwenziye. Wote hamko makini na hamjatulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A journalist ndiye huyo huyo reporter, being a reporter ndio the first stage ya journalist kwenye print media, baadae unapanda grades unakuwa staff reporter, unakuwa senior reporter, unakuwa specialized reporter, unakuwa sub editor, unakuwa chief sub, unakuwa editor, unakuwa Chief editor, hadi Editor in Chief.

Kwenye broadcast media unaanzia announce kutangaza kifuatacho, baadae unakuwa presenter, unakuwa program host, unakuwa producer, director, executive producer, manager, hadi mkurugenzi.

Kadri unavyopanda ndipo majukumu yanaongezeka

Kwa Tanzania kadri unavyopanda na kubobea ndivyo uoga unavyo ongezeka, kwa wale waliokuwepo wakati wa Kiti Moto, unadhani Pasco huyu wa sasa anaweza kuendesha kipindi kama kile?.
P
Ha ha ha haaaa... Nimecheka sana, uko very royal Mkuu, kwakweli Pasco huyu wa sasa hawezi kuthubutu tu hata kufikiria akilini mwake kufanya kipindi kama kile.

So kwa kifupi tuseme HAKUNA UHURU WA MWANDISHI nchini.
 
Mleta mada pia unatujaza ujinga. Vichwa vya habari uvione wewe, sisi hatujaviona wala hujavigusia unatuambia vinasononesha na kusikitisha.

Kulikoni?
 
Wakati katika nchi za wenzetu vyombo vya habari vikichukuliwa kama mhimili wa nne wa serikali huku kwetu vinachukuliwa kama wapinzani wa serikali hasa pale vinapoandika ukweli wa mambo
 
Ha ha ha haaaa... Nimecheka sana, uko very royal Mkuu, kwakweli Pasco huyu wa sasa hawezi kuthubutu tu hata kufikiria akilini mwake kufanya kipindi kama kile.

So kwa kifupi tuseme HAKUNA UHURU WA MWANDISHI nchini.
Umemaanisha nini kwa neno "royal" hapo mstari wa kwanza?

Sijuwi nani mwenye afadhali Tanzania hii.
 
Back
Top Bottom