Mpitagwa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 2,338
- 1,126
WanaJF, kwa waliokuwepo ukumbi wa Nkrumah na kwa waliofuatilia mjadala wa jana kupitia ITV, watakubaliana nami kuwa kama kuna siku Nchimbi alionesha ukomavu wa kisiasa basi ni jana. Kwanza walimuwashia moto kama yeye, waliiwashia moto serikali kwa hali ya juu. Lakini alivyoinuka na kuanza kuongea, hakujibu matusi sana sana aliongea kama utani tu kwamba Dr. Slaa ni padri wake na yeye anamheshimu hivyo. Alijitahidi sana kujibu hoja zilizo kwenye uwezo wake na kuacha zile zilizo juu yake kama ya kumpandisha cheo Kamhanda. Hilo ni la JK mwenyewe. Na baadaye akakili ukweli kuwa kuna mazingira watu wanabambikiwa kesi na kutoa mfano. Cha ajabu magazeti ya leo yote hakuna hata moja lilimcover. Kunani kati ya Nchimbi na vyombo vya habari?
Mimi nilitegemea walau gazeti moja liandike waziri akiri serikali kusingizia watu kesi ili uibuke mjadala utakaopelekea kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya masikini wengi waliojaa magerezani kisa wamebambikiziwa kesi au hawana nguvu ya kisheria lakini wapi bwana. Waandishi hawako huko.
Ikumbukwe pia kuwa baada ya kumaliza kuongea alipigiwa makofi na watu wengi tu.
Binafsi ninampongeza Nchimbi kwanza kwa kuthubutu kwenda mlimani ambako boss wake anakuogopa kama nyoka, na pili kwa kutoa hotuba fupi ya kiutu uzima na kuonesha kuwa yeye ni mtawala.
Natamani ule mjadala wa jana wauone Nape na Nchemba ambao wanadhani kutukana ndiyo siasa. CCM tumeni watu kama Nchimbi kwenye mijadala sio watukanaji.
Ramadhan Kalim