Mpitagwa naungana na mtazamo wako. Nkurumah ni pahala pagumu sana kusimama, ukahutubia, ukahitimisha salama na ukapewa makofi yasiyo ya kejeli. Tumewaona viongozi wengi, wajuvi wa kuhutubu kwa mbwembwe katika mimbari, altare na majukwaani wakishindwa kusimama pale walau kwa sekunde moja waseme neno moja tu-"Oyeee!"
Nchimbi alijitahidi sana tena sana. Binafsi nampa heko kwa kuimudu ile hadhira ya watu wa kaliba ile kisawasawa. Hata hotuba yake ilisahili vema katika hisia za hadhira isipokuwa pale tu aliposema suala la Mtwara. Ni orators wachache sana tulionao katika zama hizi Tanzania wanaweza kutumia mbinu ya Nchimbi ya kuvuta uungwaji mkono na kuweka mazingira chanya kwa hadhira kukusikiliza kwa kuanza kwa kutaanabaisha ukaribu na imani yake kubwa kwa
Dr.W.Slaa, mtu anayehisiwa kukubalika na wananchi wengi. Kwa tendo hili aliwabadili wengi kisaikojia na kuwafanya wafungue milango yao ya fahamu kumsikiliza vema huku wakianza kuhisi kuwa Nchimbi ni "mwenzao" Ndo maana hata mwishoni alipotoa msimamo wake na wa serikali juu ya suala la Mtwara hakukuwa na labsha yoyote maana tayari alikuwa amekonga nyoyo za hadhira vilivyo na kupata uungwaji mkono wa kutosha kukamilisha hotuba yake salama.
Ilikuwa mategemeo yangu kuwa kesho yake front pages za magazeti na hata radio na TVs usiku ule zingetoa tathmini hii na kumpa sifa yake Nchimbi. Kinyume na hayo, mpaka leo sijasoma, kusikia wala kuona hilo likifanyika. Nafahamu Nchimbi ni rafiki sana wa vyombo vya habari hasa Wahariri. Kwa MCL naweza kuhisi kuwa mabadiliko ya Wahahariri ya hivi karibu ndo hivyo yanaanza kumuathiri Nchimbi. lakini kwa vyovyote vile iwavyo ukimya huu unaleta hisia za kuwepo mpango maalumu kwa "kufunikana" kupitia news rooms/media houses