Mimi nimeingia Zanziba mara nyingi tu kwa kutummia pasipoti. Mbona sikuwasikia hao ndugu zangu wakilalamika kuwa huu ni upumbavu katika nchi inayojiita imeungana? Badala yake nikajifunza neno 'chogo' lililokuwa likitumiwa kutusimanga sisi tunaotoka bara.
Uzoefu unaonyesha kuwa TRA ilianza kutoza ushuru kwa namba za ZNZ, baada ya wingi wa magari hayo huko bara, na kuwepo na malalamiko ya mawakala wa uuzaji magari huko Bara. Katika awamu ya tano ya SMZ kulikuwa na viwango tofauti ya ushuru bandarini na SMT, kwani SMZ ilikuwa na idara yake ya forodha.
Awamu hii ndio iliyoshuhudia wingi wa wafanyabiashara ndogo ndogo toka kona zote za afika mashariki wakiingia Zanzibar kwa kutafuta bidhaa mbalimbali kama vile; TV, video, nguo, vitambaa, kanga, viatu n.k.
Kushamiri kwa biashara hizo kulifanya matajili wakubwa wa Zanzibar na Dar kuanza kutumia bandari ya zanzibar kwa manufaa yao binafsi zaidi. Hapa ina maana kuwa kutumia bandari hiyo kupitisha mizigo yao tu na kuipeleka Tz bara. Katika hali hii ndio ukawa mwanzo wa magari yanayonunuliwa Uarabuni na Japan kupitishwa na kusajiliwa Zanzibar kabla ya kupelekwa Dar na katika mikoa mingine. Wengi wanaweza kukumbuka wingi wa daladala za Dar zilizokuwa na namba za ZNZ.
Kilichofuata hapo kitu gani kifanyike ili kuondoa uingizaji wa magari hayo bara. Kwa maneno mengine SMT inanufaika vipi na biashara ya magari toka Zanzibar? Serikali ya muungano ikaamua kuibana SMZ na kufanikiwa kuanzishwa kwa TRA Zanzibar. Licha ya hatua hii kupingwa sana na SMZ, ilifanikiwa. Huu ndio ukawa mwanzo wa kuondoka kwa namba za ZNZ huko Bara. Kwa upande wa SMZ ukawa ndio mwanzo wa kuangalia sehemu nyingine ya kupata mapato yake zaidi ya biashara na karufuu.
..ZNZ ni nchi siyo wilaya au mkoa wa Tanzania Bara. Kwa msingi huo basi ni makosa kuendesha gari lenye number plate ya ZNZ ukiwa Tanzania Bara.
..wa-Zenj wanadai kwa ZNZ ni nchi, lakini wakifanya makosa yanayolingana na uhaini na wakashtakiwa wanageuka na kudai Zenj siyo dola/nchi.
..You can not eat your cake and have. Kama Wa-Zenj wanataka kufaidi matunda ya huku Tanzania Bara basi ni vizuri wakakubali ku-surrender utaifa wao.
..Muungano imekuwa kama kuchezeana akili tuu. we need some serious discussions on how we move forward.
Bado sijaridhika na majibu yenu
sijapata jibu la kitaalam pamoja na kusifiwa kwa JF kuwa ina wataalam kede kede
Hiii tunaweza tukaifanya iwe hoja nzito ambayo ZITTO na wenzie wanaweza kuiwasilisha BUNGENI (kwa sababu hakuna mbunge wa VUF ambaye anaona umuhimu wa kuinteract na si humu)
JE WATU KUTOZWA KODI MARA MBILI KWENYE NCHI MOJA NI HALALI?
JE TRA ZANZIBAR NI OFAUTI NA TRA BARA?
KAMA HAKUNA TOFAUTI KWA NINI KUWE NA KODI TOFAUTI WAKATI SISI WAMOJA?
KWA NINI TULIPIE MAGARI PESA ZINGINE TUKISHALETA BARA?
KAMA ISSUE NI WIZI KAMA ALIVYOSEMA KIBUNAGO HIYO SI KAZI YA TRA KUWAAMBIA WANANCHI WAASUZE MAGARI YAO KWANI WASHALIPIA KODI ZOTE SASA YA NINI KUWAAMBIA WATU WASIFANYE WATAKAVYO NA MALI ZAO?
JAMANI NAOMBA MNIPE MAJIBU YA MASWALI HAYA
TUJENGE HOJA KISHA TUIWASILISHE KWA WAHUSIKA NA IKIWEZEKANA TUFANYE ONLINE PETITION
...."Muungano umekuwa kama kuchezeana akili tuu. we need some serious discussion on how we move forward."
And I believe we're heading that way...to a serious discussion, sooner than later. Fortysome years tumekuwa na muungano ulioanzishwa na viongozi tu, lakini wananchi hatujapewa nafasi ya kuuzungumzia kiuwazi, why?
Fundi Mchundo,
Sii kweli- ni lini ulienda Visiwani ukapaswa kuwa na PassPort? Hii haipo we nenda tu hata leo huhitaji passport! Tena Visiwani kwa usalama wanazidi bara mara nyingi tu-- vibaka wapo wachache sana!
Wazenj ni watu wakarimu tu na wavumilivu, sema siasa chafu zinawarudisha nyuma!
Zenj could be a free port to serve hinterland ya Bara, E and C Afrika!
Halafu- kule kuna mabinti wazuri wenye heshima...Fundi kama hujaoa nenda Visiwani, au pia kama utataka bi mdogo ni poa tu!
Mie hata Pemba (Chanjaani, Utaani) pia nimefika na nimekupenda tu sana!
Brazamen: Haya ni maswali critical sana; ngoja niwa-forwad-ie wabunge wetu labda watauliza huko bungeni.
Hapa cha kulaumu ni huo mfumo wa muungano.
kabla hujaanza kuhoji kwanini unatozwa ushuru mara mbili ktk nchi moja mie naona ungeanza kuhoji hivi?
kwanini ktk nchi moja kuna marais wawili,serikali mbili,mabaraza ya mawaziri mawili??
Mbona wabunge wa zanz wanaingia ktk bunge la tz na wabunge kutoka tz bara hawaingii huko zaz??
Mdau mmoja hapo pia kachangia kuhusu ushuru nami namuunga mkono ushuru mkubwa hauisadii nchi bali unabomoa.
Watanzania tuna vichwa vigumu. Pesa haina mipaka ya nchi na serikali yetu inatakiwa kuelewa hivyo.
Suala ni kuwa Tanzania inalipisha kodi kubwa sana kuliko nchi zingine. Na wafanyabiashara siku zote wanatafuta upenyo wa kukwepa kulipa kodi zisizo na maana. Na hili sio suala la muungano ni upungufu wa akili.
Kwanini mwenye magari ya mizigo kutoka Tanzania watumie bandari ya Mombassa na sio DSM? Kuna watu wanapitishwa vitu Kenya, Burundi, Uganda na Rwanda kukwepa kulipa kodi. Na hao wanaofanya hivyo ni watanzania.
Sababu ya kulipa kodi kubwa ni kuwa ni asilimia ndogo ya watanzania wanaliolipa kodi. Na sehemu kubwa ya mapato inatokana na kodi ya ushuru wa kuingiza bidhaa. Na hiki kitu imefanya Tanzania ijitoe COMMESA.
Kodi kubwa haisaidi maendeleo ya nchi hata siku moja. Imefika wakati tuwe na flat rate kwa nchi zote za afrika mashariki.
JE TRA ZANZIBAR NI TOFAUTI NA TRA BARA?
Nimepitai hii thread mwanzo mpaka hapa ilipofika sijapata jibu la swali hilo hapo juu...