Magari yenye ZNZ Dar es salaam

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Hivi kwa nini lazima kulipia au kusajili namba upya kama gari lenye ZNZ likishaingia Dar baada ya Miezi 6?

Mbona suala hili halilalmikiwi?

Zanzibar ni Tanzania lakini kwa nini serikali yetu inatuibia mchana kweupe

labda mie nimezidi kulalama lakini huuu naona ni wizi wa mchana sijui wenzangu mnasemaje?
 
Si hilo tu, nakumbuka kisa kimoja cha mama mmoja daktari aliyekuwa mfanyakazi wa Wizara ya afya Zanzibar, ana gari lake alilokuwa akilitumia Zanzibar na lilikuwa na exemption ya ushuru kwa asilimia 99 (custom duties) na ililipiwa asilimi 1 ya ushuru na asilimia 20 ya VAT kama inavyoruhusiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, malipo yote yalifanyika Zanzibar lakini hayakulipwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, bali yalilipwa kwa Tanzania Revenue Authority (Zanzibar), chombo kinachokubalika ki-Muungano. Cha kushangaza, alipohamia Dar. ilibidi TRA hao hao wamwambie kuwa hawatambui exemptions za Zanzibar na inabidi akitaka kuitumia gari huku (Bara) ailipie ushuru uliokwisha samehewa Zanzibar. Na hakuwa na njia ila kulilipia hiyo 99% iliyokuwa exempted na walikataa hata kuifanyia depreciation wakati gari ilikuwa imeshatumika zaidi ya mwaka kabla ya kuhamishiwa bara.

Sasa maswali yanakuja, TRA moja inasheria za Zanzibar na Tanganyika?

Labda Kikwete na Amani Karume ndio wanaojuwa majibu?

Hata sijuwi nchi hii wanaiongozaje.
 
Hli linaeleweka na huko visiwani wakiwa na Vikao yao vya Baraza la Wilaya(BLW) husemewa, lakini nani atawasikiliza si unajua kiburi cha CCM.
Cha kujiuliza ni jee magari yaliyona na namba za TZ yanalipishwa tena ushuru yakienda Znz, anayejua atueleze kabla ya kulalamika tu.
 
Hayalipiwi, na sababu nilizosikia mitaani ni kwa sababu magari yenye namba za T ni registration ya Muungano kwa hiyo hayana haja yakuwa registered tena yakiwa Zanzibar. Yale yenye namba za ZNZ yanahesabika kuwa hizo si registration za Muungano na inabidi yakiwa bara yahisabike kama magari ya kutoka nje ya nchi na yafate sheria za gari za nje ya nchi zinazotumika Tanzania.
 
Si hilo tu, nakumbuka kisa kimoja cha mama mmoja daktari aliyekuwa mfanyakazi wa Wizara ya afya Zanzibar, ana gari lake alilokuwa akilitumia Zanzibar na lilikuwa na exemption ya ushuru kwa asilimia 99 (custom duties) na ililipiwa asilimi 1 ya ushuru na asilimia 20 ya VAT kama inavyoruhusiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, malipo yote yalifanyika Zanzibar lakini hayakulipwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, bali yalilipwa kwa Tanzania Revenue Authority (Zanzibar), chombo kinachokubalika ki-Muungano. Cha kushangaza, alipohamia Dar. ilibidi TRA hao hao wamwambie kuwa hawatambui exemptions za Zanzibar na inabidi akitaka kuitumia gari huku (Bara) ailipie ushuru uliokwisha samehewa Zanzibar. Na hakuwa na njia ila kulilipia hiyo 99% iliyokuwa exempted na walikataa hata kuifanyia depreciation wakati gari ilikuwa imeshatumika zaidi ya mwaka kabla ya kuhamishiwa bara.

Sasa maswali yanakuja, TRA moja inasheria za Zanzibar na Tanganyika?

Labda Kikwete na Amani Karume ndio wanaojuwa majibu?

Hata sijuwi nchi hii wanaiongozaje.

Wana JF kwa kweli hata mimi huu mchanganyiko wa kimuungano feki mimi siuelewi. Sio tu kwenye magari, bali hata kwenye airport ya Zanzibar. Niliwahi kulipia airport charges kwenye ticket nikiwa Dar, nilipofika airport ya Zanzibar nakumbuka nilichajiwa mara ya pili kwa kigezo kuwa bendera ni mbili. Yaani ukiwa Zanzibar hauko Tanzania na ndio maana kuna bendera ya Zanzibar. Sasa mimi sikuelewa kwa kweli, tangu lini Zanzibar sio Tanzania..??? Unless wangeniambia kuwa ukiwa Zanzibar hauko Tanganyika.

Kwa kweli huu Muungano tusipouweka wazi yaani tusipofafanuliwa wote (wa bara na visiwani), hatukawii kugeuka wakikuyu na wajaluo. Manake, kumeanza element ya kutengana na kukomaa na concept ya "wao na sisi", (yale yaleeee ya Mwl. Nyerere aliyokuwa anayaponda kila siku). Na muda si mrefu utasikia, Mkapa katoka bara, Kikwete katoka bara, n.k. katoka bara, sisi je..?? Hivyo tukemee hii tabia ya utengano, kama hawataki Muungano, basi serikali ikae chini na kufyatua Muungano tubaki kibara bara kieleweke. Kuna wakati niliwahi kusikia hadi mambo ya passport kwenda Zanzibar yanaweza anza. Sasa huu ni Muungano au ni urafiki wa kijirani...???
 
Ndio Mapungufu ya Muungano wetu,Je nyie mnatakaje?hayo magari yenyewe mnayanunua kwa bei ya chini..na hii ndio faida ya Muungano.
 
Hli linaeleweka na huko visiwani wakiwa na Vikao yao vya Baraza la Wilaya(BLW) husemewa, lakini nani atawasikiliza si unajua kiburi cha CCM.
Cha kujiuliza ni jee magari yaliyona na namba za TZ yanalipishwa tena ushuru yakienda Znz, anayejua atueleze kabla ya kulalamika tu.
Unaweza kuwa na hoja nzuri, lakini hii ya Baraza la Wilaya ni kipimo tosha jinsi gani hoja yako idhauriwe
 
TRA pamoja na marekebisho ya kuwa na TRA moja, bado kila kitakachoingia BARA lazima kilipiwe difference.

CCM imeua business Zanzibar. siwezi sema wabara hatutajenga. Najua ipo BUILT-IN chuki ambayo imejengwa for so long kati ya bara na znz. LKN ni Swala la Wazi CCM BARA are not Ready kuona ZNZ kuna maendeleo. zipo sababu zilizojificha hazisemwi, lkn imeonekana tuna CHUKI zile za ASILI za kuona Fulani atapata.

Zamani ilikuwa hata wafanya biashara wadogo...hata akina mama wanaofanya business kwa kukopesha walikuwa hasa wanakwenda znz kuchukua mali na wanaleta Bara kufanya business. Kumetokea WIND of CHANGE kubwa mno ktk miaka ya hivi karibuni, ambapo sasa ukiwa znz vitu vyake ni Ghali kuliko Bara. Sometimes bidhaa ukinunua Mwanza inaweza kuwa cheap kuliko Znz, wakati ZNZ wana ACCESS ya port n airport, ambapo Mali kutoka Nje yaweza leta mali anytime. Wind of Change hii imewafanya hata wafanya biashara wa ZNZ wahamie Bara.

Haya mambo inabidi yashughulikiwe effectively...CCM znz Wanatishwa na Bara, the only Man anayeweza kufanya mabadiliko haya ni Muungwana, lkn mafisadi wamekuwa wakimrudisha nyuma
 
suala hili nnakumbuka liko ktk meza ya mazungumzo ya kero za muungano.

ambayo hukaa waziri kiongozi wa SMZ na waziri MKUU wa SMT sasa sijui wamefikia wapi? na sasa ndio kaja bwana mpya sijui ile kasi ya mazungumzo yao itaendeleaje?
 
Binafsi tatizo ninaloliona katika huu muungano ni hili: WANANCHI AMBAO NDO WALENGWA WA HUU MUUNGANO HATUUELEWI. Yaani ni muungano wa viongozi na kwenye maandishi lakini ikija kwetu wahusika wakuu ambao ndo sisi we know nothing! Ndo maana mimi zaidi ya theories za darasani na nostalagia za akina Nkurumah na Nyerere waliotaka Africa iungane, siwezi kukwambia faida ya huu muungano! Its a bizarre, yaani wananchi we are almost not involved in the whole process. Kwa hiyo usishangae unapoona watu wana malalamiko kibao...Its not their fault....Its the government which keeps the whole issue as a governement secret!

Na tunakosa viongozi/watendaji creative. Vitu kama kodi, TRA ingeweka awareness campaign, on who pays what and how on the either side of the Union, wafanyabiashara ndogo ndogo ambao ndo wahanga wakuu wakalijua hili......Tz matatizo yetu ni mengi mno! Uhhh...!
 
kondoa is too big to compare with! What about "SOWETO" Ooooh!!! sorry MANZESE"........!?

Mahesabu...Ghana inaingia mara 80 ya Tanganyika..lkn bado ni NCHI yenye MAMLAKA KAMILI...Ukilinganisha idadi utakuwa haufanyi Haki.Tanganyika still inataka kuifanya Znz kama "Buguruni" au "Manzese"

kwa Population ya DSM inahitaji kuwa na wabunge 26-30, lkn ina wabunge 7 tu...so sometimes hatwendi kwa hesabu kama zako. ndo maana hata unaposikia shule kuongoza wanaangalia vigezo vingie. Angalia st. Francis imeongoza ikiwa na wanafunzi 25, wakati AZANIA (AZABOY) ina wanafunzi 400~500, division 1, zaidi ya 80.
 
kondoa is too big to compare with! What about "SOWETO" Ooooh!!! sorry MANZESE"........!?

wengine wana visa vya kanisa, hivi kwa zanzibar watu wake kidogo ishakuwa wilaya jee tanzania nzima watu wake sawa na state ya new york isiitwe nchi? huu ni uzuzu zanzibar haiwezi kufananishwa na mkoa wowote seuze wilaya ni nchi iliokuwa na kila chake na kuamua kuingia kwenye muungano kwa ridhaa na tukaamua kubakisha nusu ya nguvu zetu.

tena na ukome mwana hizaya weee uso adabu
 
Mtu wa Pwani,

Calm down my dear....
 
Mkuu,
Pole pole. Mwelimishe jamaa kwa hoja, sio jazba.
Nadhani tuko pamoja.
 
Uzoefu unaonyesha kuwa TRA ilianza kutoza ushuru kwa namba za ZNZ, baada ya wingi wa magari hayo huko bara, na kuwepo na malalamiko ya mawakala wa uuzaji magari huko Bara. Katika awamu ya tano ya SMZ kulikuwa na viwango tofauti ya ushuru bandarini na SMT, kwani SMZ ilikuwa na idara yake ya forodha.

Awamu hii ndio iliyoshuhudia wingi wa wafanyabiashara ndogo ndogo toka kona zote za afika mashariki wakiingia Zanzibar kwa kutafuta bidhaa mbalimbali kama vile; TV, video, nguo, vitambaa, kanga, viatu n.k.

Kushamiri kwa biashara hizo kulifanya matajili wakubwa wa Zanzibar na Dar kuanza kutumia bandari ya zanzibar kwa manufaa yao binafsi zaidi. Hapa ina maana kuwa kutumia bandari hiyo kupitisha mizigo yao tu na kuipeleka Tz bara. Katika hali hii ndio ukawa mwanzo wa magari yanayonunuliwa Uarabuni na Japan kupitishwa na kusajiliwa Zanzibar kabla ya kupelekwa Dar na katika mikoa mingine. Wengi wanaweza kukumbuka wingi wa daladala za Dar zilizokuwa na namba za ZNZ.

Kilichofuata hapo kitu gani kifanyike ili kuondoa uingizaji wa magari hayo bara. Kwa maneno mengine SMT inanufaika vipi na biashara ya magari toka Zanzibar? Serikali ya muungano ikaamua kuibana SMZ na kufanikiwa kuanzishwa kwa TRA Zanzibar. Licha ya hatua hii kupingwa sana na SMZ, ilifanikiwa. Huu ndio ukawa mwanzo wa kuondoka kwa namba za ZNZ huko Bara. Kwa upande wa SMZ ukawa ndio mwanzo wa kuangalia sehemu nyingine ya kupata mapato yake zaidi ya biashara na karufuu.
 
Bado sijaridhika na majibu yenu

sijapata jibu la kitaalam pamoja na kusifiwa kwa JF kuwa ina wataalam kede kede

Hiii tunaweza tukaifanya iwe hoja nzito ambayo ZITTO na wenzie wanaweza kuiwasilisha BUNGENI (kwa sababu hakuna mbunge wa VUF ambaye anaona umuhimu wa kuinteract na si humu)

JE WATU KUTOZWA KODI MARA MBILI KWENYE NCHI MOJA NI HALALI?

JE TRA ZANZIBAR NI OFAUTI NA TRA BARA?

KAMA HAKUNA TOFAUTI KWA NINI KUWE NA KODI TOFAUTI WAKATI SISI WAMOJA?

KWA NINI TULIPIE MAGARI PESA ZINGINE TUKISHALETA BARA?

KAMA ISSUE NI WIZI KAMA ALIVYOSEMA KIBUNAGO HIYO SI KAZI YA TRA KUWAAMBIA WANANCHI WAASUZE MAGARI YAO KWANI WASHALIPIA KODI ZOTE SASA YA NINI KUWAAMBIA WATU WASIFANYE WATAKAVYO NA MALI ZAO?

JAMANI NAOMBA MNIPE MAJIBU YA MASWALI HAYA

TUJENGE HOJA KISHA TUIWASILISHE KWA WAHUSIKA NA IKIWEZEKANA TUFANYE ONLINE PETITION
 
wengine wana visa vya kanisa, hivi kwa zanzibar watu wake kidogo ishakuwa wilaya jee tanzania nzima watu wake sawa na state ya new york isiitwe nchi? huu ni uzuzu zanzibar haiwezi kufananishwa na mkoa wowote seuze wilaya ni nchi iliokuwa na kila chake na kuamua kuingia kwenye muungano kwa ridhaa na tukaamua kubakisha nusu ya nguvu zetu.

tena na ukome mwana hizaya weee uso adabu

Kanisa limeingiaje humu tena?
 
Hivi kwa nini lazima kulipia au kusajili namba upya kama gari lenye ZNZ likishaingia Dar baada ya Miezi 6?

Mbona suala hili halilalmikiwi?

Zanzibar ni Tanzania lakini kwa nini serikali yetu inatuibia mchana kweupe

labda mie nimezidi kulalama lakini huuu naona ni wizi wa mchana sijui wenzangu mnasemaje?

Serikali ya mapinduzi Zanziba ina viwango vyake vya kodi tofauti na vilivyo katika serikali ya Muungano. Viwango hivi vinatumika Zanziba tu na si bara. Kwa hali hiyo mtu akitaka kuvifaidi inabidi atumie gari lake Zanziba na si bara. Akienda nalo bara, viwango vya muungano inabidi vitumiwe. Akitaka kuepuka adha hiyo, anapoingiza gari lake alipie viwango vya muungano na hatasumbuliwa akienda nalo bara. Hataki, alibakize Zanziba na akiwa bara atumie daladala. Uchaguzi ni wake.

Hiyo biashara inayolalamikiwa ilikuwa ikiinyima serikali ya Muungano kodi yake ya halali. Watu walikuwa wanaingiza bidhaa zao zanziba si kwa lengo la matumizi zanziba bali ku'reexport' kupeleka bara na hivyo kuepuka viwango vya kodi ya Muungano. Wengi walikuwa wanatumia bandari ya bagamoyo kufanya hivi. Serikali ya muungano kama ambavyo serikali nyingine yeyote inayotegemea kodi kwa shughuli zake imebana loophole hizi.

Kwa nini hatulalamikii viwango vya bei ya umeme ambao serikali ya Muungano inafidia? Itafika wakati wazanziba watadai hata watakapohamia bara waendelee kulipa umeme kwa viwango walivyozoea!!!!! Kwa nini wazanziba hawatumii tofauti hii kuanzisha viwanda ambavyo vingeweza kuuza si bara tuu bali nchi nyingine? Hivi kweli uchumi wenu ulikuwa unategemea hao wakina mama wanaokuja kununua sidiria ili wakawauzie wenzao maofisini kwa mikopo? Basi iko kazi!!!

Mimi nimeingia Zanziba mara nyingi tu kwa kutummia pasipoti. Mbona sikuwasikia hao ndugu zangu wakilalamika kuwa huu ni upumbavu katika nchi inayojiita imeungana? Badala yake nikajifunza neno 'chogo' lililokuwa likitumiwa kutusimanga sisi tunaotoka bara. Ukija kwetu, ishi kama mtanzania. Ukitaka kuishi kama mzanziba, baki Zanziba. hatutakufuata huko.

Hii tabia ya kujiona victims kila wakati haitawasaidia kitu.
 
Back
Top Bottom