Magari yaendayo kasi yawa sababu kuu ya vifo vya duma Serengeti

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Hii imejulikana katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI) wa kuchunguza mwenendo wa uzazi na ukuaji wa duma katika Mbuga ya Serengeti nchini Tanzania

Utafiti umerekodi ongezeko la vifo vya wanyama hao jamii ya paka katika miaka ya karibuni kutokana na kugongwa na magari ya watalii yaendayo kasi

Utafiti umebaini duma nane waliuawa kwa kugongwa na magari yaendayo kasi kati ya 2016 na 2018

Licha ya faini ya dola za kimarekani 5000 na kuzuiwa kuingia tena mbugani, bado tatizo la mwendokasi limezidi kuongezeka ndani ya mbuga hiyo

Duma ni wanyama wenye kasi ndogo ya kuzaliana na watoto wao hushambuliwa na wanyama wawindaji wengine kama fisi, simba na chui. Kati ya duma 100 wanaozaliwa, ni watatu tu huishi hadi ukubwani

My take:

Ikumbukwe duma anakimbia kilomita 100 hadi 120 kwa saa. Sasa hao wanyama wengine si ndo watamalizika kabisa?!!
 
Tatizo la Duma ni Dhaifu sana katika wanyama walao nyama hata mbwa mwitu wanamkimbiza.
 
Sasa si waanzishe mradi kama ule wa mbwa mwitu wawafungie mahali wazaliane then wawa release chakula nazani sio tatizo manyumbu yapo ya kutosha kuwalisha
 
Back
Top Bottom