Magari ya wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya wizi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Preta, Aug 21, 2010.

 1. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  wakuu nimeshuhudia mkasa mmoja ambao umenisukuma kuja kuuleta hapa jamvini ili tuweze kuelimishana. Nina mshkaji wangu mmoja alinunua gari kwa jamaa sasa ameichoka akaamua kuiuza. katika kutafuta mteja akampata afisa mmoja wa usalama,wameelewana bei kila kitu mwisho ikafikia wakati wa kukabidhiana documents. Afisa kachukua documents akasema azihakikishe, kilichotokea kwanza kadi ya gari yenyewe ilikuwa kanyaboya (fake) pili engine # na ile iliyoandikwa kwenye kadi tofauti, tatu chasis # imemiss tarakimu, jamaa kaponea chupuchupu kulala sero...sasa ninachotaka kujua kabla hujaenda TRA kuhakikisha je utajuaje documents ni fake?.......nimesikia hata shipping documents watu wanafyetua...help pls
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tuanze taratibu, huyo jamaa yako ametumia hiyo gari muda gani? Inamaana hakuwahi kurenew road licence? Na amenunua hapahapa Bongo? Maana upo uwezekano kuwa alinunua gari ya uwizi.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hapo ndio nilichoka..kurenew licence alirenew mara kama mbili na gari aliinunua hapa hapa bongo
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kwa ufupi usinunue magari ya mitaaani....
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  apart from kuagiza nje....mbona nasikia hata yard mtu unalizwa vile vile
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Yard ya wapi..........

  Sio kila yard ni wa kuaminika..........
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yard nyingi kwa Bongo ni km umeenda kununua kiatu kariakoo. Kuna uwezekano ukaondoka na boksi lenye viatu unavyohitaji au boksi lenye viatu visivyo. Maana hawa jamaa wanaouza magari utawasikia mara nyingi wanasema na kadi tunaishughulikia kabisa (hapa ndio kwenye tatizo). Maana inakuwa card fake. Ukiweza check kila kitu kabla ya makabidhiano. Sasa km aliweza kurenew inawezekana pia wachapaji walikosea. Angeweza kuanzia TRA au hata polisi maana vinginevyo itakula kwake.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Pole wanalizwa yard ije kuwa huyo
  mpe pole sana mwambie tu atafute lingine la ukweli
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni PM ukitaka mambo hayo bila kupata usumbufu
   
 10. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  huyo rafiki yako anajua A to Z ya hilo gari ila ajakueleza ukweli. Huyo rafiki yako ni muhusika mkuuu

  yard haziuzii watu magari ya wizi bila kuwataarifu wenyewe
  watu wengi wanaoendesha magari ya wizi wanajua ni magari ya wizi, wanafanya hivyo kwa ajili bei ni rahisi mkuuu
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  lakini mkuu kumbuka mteja alikuwa ni afisa wa usalama....inawezekana kweli alikuwa anajua halafu aende kuliuza poshti?
   
 12. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Siku hizi documents nyingi (card au renewal zake) zinafanyiwa barabarani au mitaani. Kwa mfano kijiwe sugu sana kwa hii biashara ya documents fake za magari na zinginezo ni mbele ya Billicanas na Break Point. Pale unaweza ukamili gari miaka yote na usijue biashara za TRA. Hata ukihitaji documents zingine kama vile fm 4 and fm 6 certificates, jamaa wapo pale, unawapa hela, next day unakuja kuchukua cheti kikiwa na jina lako na number ambayo iko registered Baraza la Mitihani la Taifa.

  Ukitaka kununua gari ambalo una wasi wasi nalo, mwambie mwenye gari akupe card then panda makao makuu ya Police ghorofa ya sita. Unawakatia jamaa kidogo dogo wanakupa details zote za wamiliki wa hiyo gari baada ya kutengenezwa mpaka siku hiyo.

  Msilaumu system, hata dola fake siku hizi zinapita kwenye machine....
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Tumekwisha ...
   
 14. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  duh,mpaka hapo nimenawa mikono.hii nchi sijui inelekea wapi.sipati picha baada ya miaka kumi itakuwaje.
   
 15. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Haleluyah:confused2:
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hiyo niliyoweka kwenye red, inawezekana kuna wakubwa kwenye system wanahusika maana hicho kijiwe kinajulikana na watu wengi sana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Nasikia hata ukitaka funguo na mihuli ya ikulu hapo unapata. Mhhh!
   
 17. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wakubwa wenyewe wanategemea pale pa Bilcanas kufanikisha mambo yao. Pale ndo penyewe. kuna kibosile mmoja alikuwa anakaribia kustaafu akagundua kuwa amespend life na hakusave akaona solution ni kuongeza muda wa kukaa kazini maana alikuwa astaafu mwakani. Amekwenda pale wamempa vyeti vya kuzaliwa, kumaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo ambavyo ni genuine kabisa. Yule mzee as we are speaking atastaafu baada ya miaka 5 from now.

  Ni mtu anayenihusu kwa hiyo naongea from real example.
   
Loading...