Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
Ikiwa ni siku ya pili tangu serikali ya Zambia kufunga mpaka, shughuli zote za mpakani zimesimama, hali iliyosababisha magari yaliyobeba mizigo kama chakula na mafuta kukwama kuendelea na safari.
Brigedia Jeneral Nicodemas Mwangela, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, jana alifika katika mpaka huo uliopo mji wa Tunduma, wilaya ya Momba, ambapo alijionea bidhaa mbalimbali zikiwa zimekwama kuvuka.
Aliwataka wasafirishaji mizigo hiyo kuwa na subira ambapo alisema kuna mazungumzo yanaendelea, na kwamba huenda mpaka huo ukafunguliwa mapema kufuatia makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuzuia kufunga mipaka kabisa badala yake bidhaa muhimu kama mafuta na chakula viruhusiwe kuvuka.
Aidha, liwataka wasafilishaji kuondoa hofu kutokana na adhabu ambazo wanaweza kukumbana nazo kufuatia sheria ya kutokaa mpakani bila kuvuka kwa zaidi ya siku saba.
''Tunduma ni salama, Songwe ni salama hakuna haja ya wananchi kuwa na hofu, endeleeni kuchapa kazi,” alisema mkuu wa mkoa.
Juzi, serikali ya Zambia ilianza utekelezaji wa agizo hilo kwa kufunga mageti yote mawili ya kuingilia nchini humu pamoja na maduka, na shughuli zote zinazofanywa kwenye eneo la mpaka, hali iliyoibua vilio kwa wafanyabiashara wa mji wa Tunduma.
Wakizungumza baada ya utekelezaji wa agizo la kufunga mpaka, wafanyabiashara hao walisema kwa sasa wana mazingira magumu ya kumudu maisha yao kwani maisha ya mji wa Tunduma yanategemea sana biashara.
Neema Kalinga, mmoja wa wafanyabiashara waliofungiwa maduka, alisema hawana cha kufanya kwani walishindwa hata kuchukua chochote dukani kufuatia askari wa Zambia kufunga maduka yote majira ya alfajiri, na kwamba hakukutolewa taarifa yoyote kwa ajili ya kujiandaa na hatua hiyo.
Aliongeza serikali ya Zambia ilipaswa kutoa angalau siku moja kwa ajili ya wafanyabiashara kujiandaa kwani wangeweza hata kuhamisha bidhaa zo ili mpaka ukifungwa maisha mengine yaendelee.
George Kyando, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, alisema ulinzi mpakani umeimarishwa vya kutosha, na Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida.
NIPASHE