GREATTHINKERDAIMA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 232
- 46
Mkuu tunashukuru kwa taarifa hiyo, kwa kuwa upo eneo la tukio tuwezeshe kupata habari kwa undaji na picha pia itasaidia.
Kwanini unataka ku play down issue hii? RPC alishasema wamekamata magaidi 9 Nyandeo Kilombero. Taarifa zikatolewa kwamba magaidi hayo yakiwa mikononi mwa dola yakasema tupo wengi tutatimiza azma yetu.
Mtu analipua bomu eneo la watu wengi na kujeruhi wewe una sema ni kibaka? Are you among them?
acha kuropokwa ndugu unawezaje kumtuhumu mtu kuwa ni gaidi bila ya kuwa na udhitisho....ndugu yangu chunga sana kauli yako usipende kuropokwa
Yatupasa kuangalia upya maudhui ya mafundisho ya dini yanayotolewa katika nyumba za ibada......
hakuna dini unayofindisha uovu.Yatupasa kuangalia upya maudhui ya mafundisho ya dini yanayotolewa katika nyumba za ibada......
acha kutisha watu, wamevamia kijiji au ni vibaka wamevamia ofisi ya ccm?
Ndugu wana jukwaa,
Muda sio mrefu kuna tukio la kutisha limetokea hapa kijijiji cha Msolwa ujamaa, wilaya ya Kilombero. Tukio hilo limefanywa na vijana wawili wadogo ambao wametoweka baada ya kufanya tukio hilo. Vijana hao walikodisha pikipiki wakitokea Ruaha na wakamwambia dereva wa pikipiki hiyo awapeleke kijiji cha Kisawasawa, wakiwa njiani, dereva wa pikipiki alipata mashaka juu ya vijana hao hivo akawaambia kua atawashusha kijiji cha Msolwa ujamaa ili watafute usafiri mwingine kwa vile muda umekwenda na hatakua tayari kwenda mpaka kisawasawa. Alipofika Msolwa ujamaa akawashusha vijana hao na kumpigia simu mwenyekiti wa kijiji. Mwenyekiti huyo alianza kuwahoji na kugundua kua ni vijana wageni wasiotambulika maeneo haya, hivo akaita watu wengine na kuanza kuwahoji zaidi.Vijana wale walipoona wanaanza kusachiwa, wakakurupuka na kuponyoka, wakafungua bomu la mkono na kulirusha.
Kumetokea majeruhi watano ambao wameumia vibaya.
Source: Mimi mwenyewe nipo eneo la tukio baada ya kupigiwa simu na jamaa yangu hivo nimefika hapa