Mafuta yanavyohangaisha utawala Z’bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta yanavyohangaisha utawala Z’bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 8, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 06 July 2011

  Kalamu ya Jabir
  KATIKA mazingira ya mfungamano wa kiutendaji uliopo ndani ya Jamhuri ya Muungano imekuwa vigumu Zanzibar kujizongoa na kile kinachoonekana kama mnyororo ili kujitegemea kiuchumi.

  Ukweli huu unajengwa na ushirikiano uliotokana na kuunganishwa dola mbili zilizokuwa huru kabla – Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika – kwa mkataba uliasainiwa 26 Aprili 1964.

  Sasa mfungamano huu, unajichimbia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, inayojumuisha nchi tano wanachama baada ya Burundi na Rwanda kujiunga pale Kenya, Uganda na Tanzania zilipoasisi ushirikiano huo.

  Kwa kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili, Zanzibar inaingia kwenye jumuiya kwa mgongo wa Tanzania.

  Jambo jipya limejitokeza. Baraza la Wawakilishi, chombo cha kutunga sheria mfano wa Bunge, limeambiwa itakuwa vema Zanzibar itambuliwe na kama mwanachama mshiriki – Associate member.

  Nini? Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ismail Jussa Ladhu wa Mji Mkongwe, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), anashauri serikali kuomba Sekretarieti ya Jumuiya irekebishe itifaki ya ushirikiano ili Zanzibar ijisemee yenyewe.

  Jussa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, anaipa nguvu hoja yake kwa kusema wakati itifaki ya jumuiya ya Afrika Mashariki inaunganisha nchi wanachama kwa mambo 17, kwa Jamhuri ya Muungano ni mambo manne tu ndiyo mambo yanayoshughulikiwa kimuungano.

  Nini maana yake? Kwamba Zanzibar inayotambuliwa na jumuiya kama mshirika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inanyimwa haki ya kimsingi ya kushughulikia mambo yale 13 yasiyokuwa katika muungano wake na Tanzania Bara.

  CUF kinashirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuongoza serikali chini ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

  Nini matokeo ya mfungamano huo wa mambo yasiyokuwa ya muungano katika jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Zanzibar imeingia chini ya mgongo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

  Kwamba Zanzibar haiwezi kusimamia masuala hayo 13 kwa uhuru na kama vile inavyoona inafaa kuyasimamia. Huku ni kunyimwa uhuru wake wa kimsingi kama nchi.

  Ndipo Jussa anapoishauri SUK iwasiliane na Sekretarieti ya Jumuiya kuitaka irekebishe itifaki na hivyo kuipa uhuru Zanzibar wa kuamua itakavyosimamia yenyewe mambo hayo kwa maslahi ya Wazanzibari.

  Baadhi ya mambo yanayobainishwa katika itifaki ya jumuiya ambayo hayamo katika Orodha ya Mambo ya Muungano kama inavyobainishwa katika Makubaliano ya Muungano – Aricles of Union – ni Kazi, Utalii, Mazingira na HIV/AIDS.

  Ikumbukwe kuwa Makubaliano ya Muungano ndiyo msingi wa mambo ambayo dola mbili huru, Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, zilikubaliana kushirikiana kimuungano.

  Mambo yaliyomo kwenye orodha hiyo yanasomwa katika Ibara ya 102 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Vile Zanzibar inavyochukuliwa katika jumuiya ilikuwa moja ya hoja zilizotawala mjadala wa bajeti ya kwanza ya SUK kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012.

  Hiyo ni moja ya changamoto nyingi kwa serikali ya Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye kwa miaka minane kuanzia Julai 2002, aliitumikia Serikali ya Muungano kama makamu wa rais, alipoteuliwa kuziba pengo la Dk. Omar Ali Juma (Mwenyezi Mungu amrehemu) aliyefariki 2 Julai 2002.

  Na changamoto hii inachimbuka mifupani mwa muungano wa Tanzania ambao kwa Zanzibar unaendelea kuonekana kikwazo cha maendeleo yake.

  Sitakosea nikisema wananchi na viongozi wakuu wa serikali Zanzibar wanaamini chini ya mfungamano wa kimuungano, Zanzibar itabaki nyuma kwani "imebanwa na haitoki bila ya ridhaa ya Dar es Salaam."

  Wazanzibari wanakumbuka walivyopigwa "changa la macho" na Tanzania. Mwaka 1993, Zanzibar ilipotangaza rasmi kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC), haraka ilitakiwa kutoka.

  Wakuu wake walitishwa kuadhibiwa wasipoitoa Zanzibar kwenye jumuiya hiyo.
  Serikali ya muungano iliahidi kwamba itafikiria kujiunga baada ya kutafiti muundo wa jumuiya hiyo kwa kuwa Zanzibar haipaswi kufanya hivyo kisheria.

  Tangu hapo kila ikiulizwa inatapatapa. Imezidisha kigugumizi kila swali kuhusu suala hilo linapoulizwa, iwe ndani au nje ya bunge.

  Lakini, zipo taarifa kuwa wakuu wameapa Tanzania haitajiunga OIC, mjumuiko unaofadhili miradi ya maendeleo kwa nchi wanachama, zikiwemo zile zenye watu wachache Waislam. Msumbiji na Uganda ni mfano wake.

  Hatua ya Serikali ya Muungano kuilazimisha Zanzibar, ilikuwa mzaha. Kilichokuja baadaye, kule Tanzania kukaa kimya na sasa kuthibitisha haiko tayari kujiunga OIC, ndiko kunawaumiza Wazanzibari.

  Kwamba kumbe muungano ni kiinimacho. Kwamba kwa yale ambayo Zanzibar inaamini yataisaidia kuendelea, inazuiwa na inatishwa isithubutu, lakini Tanzania Bara yenye raslimali nyingi inazozitumia bila ya kuifikiria Zanzibar, ina uhuru wa kujitanua.

  Ni mtizamo huu uliochochea wawakilishi kuibana serikali ndani ya mjadala wa bajeti, isimame imara na kuzingatia matakwa ya wananchi badala ya kuhofia kuandamwa na wakuu wa Dar.

  Ndivyo hoja ya kutaka SUK iharakishe uanzishaji wa shirika lake la maendeleo ya mafuta na gesi – Zanzibar Petroleum and Gas Development Corporation, ZP&GC – ili kushughulikia uchimbaji wa mafuta yaliyowahi kuthibitishwa kuwa yapo chini ya ardhi ya Zanzibar tangu miaka ya 1950.

  Kabla ya kumaliza muda wa uongozi wake, Amani Abeid Karume kutokana na azimio la baraza lilojadili suala hilo, alianzisha utaratibu kuwezesha mafuta na gesi kuondolewa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.
  Ingawa kauli za kisiasa zinabeza, ripoti ya kitaalamu inathibitisha Zanzibar kauwa na mafuta kutokana na utafiti uliofanywa mara mbili ikiwemo mpaka miaka ya 1980.
  Maeneo yaliyogundulika dalili za mafuta ni Tundaua, kwenye mwambao wa magharibi mwa kisiwa cha Pemba, na Kama, mwambao wa magharibi mwa kisiwa cha Unguja. Kama ni kilomita 12 tu hivi kutoka bandari ya Malindi, mjini Zanzibar.

  Karibu kila mwakilishi aliyejadili bajeti aliyowasilisha Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, alihimiza hatua zilizobaki za kuhakikisha mafuta yanakuwa suala la kushughulikiwa na Zanzibar yenyewe.

  Ndipo Jussa alipovunja mfupa kwa kuamini itachukua miaka mingi Dar kuridhia jambo hilo, aliposema SUK iandae rasimu ya marekebisho na kuipeleka bungeni.

  Utaratibu wa kikatiba na kanuni za bunge zinaelekeza kuwa jambo lolote linalogusa muungano linapohitaji uamuzi, lazima liridhiwe na theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar na pia kwa wabunge wa Bara.

  Jussa hana wasiwasi theluthi mbili itapatikana kwa wabunge wa Zanzibar, bali anahofia kwa wabunge wa Bara. Ikitokea ikakwama, anashauri Zanzibar iamue peke yake.

  Kwamba suala hilo litakuwa limekosa muafaka na kwa hivyo itakuwa haki kwa Zanzibar kushughulikia mafuta na gesi inavyoona inajenga maslahi ya watu wake.

  Kweli, huu ni mtihani kwa Dk. Shein. Pengine ndio maana Waziri Mzee na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi (CCM), waliposema kwa lugha nyepesi hatua zitachukuliwa bila ya "jazba."

  Mawaziri wakiwemo watokao CCM waliunga mkono hoja za Jussa kutaka mafuta yabaki katika himaya ya Zanzibar ili itumie mapato yake kujenga uchumi na watu wake. Kama mambo haya mawili yatashughulikiwa kwa maslahi ya Zanzibar ni kitu cha kusubiri; angalau kwa sasa serikali inajua ikilala, itaamshwa tu.

   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hongera sana Mwandishi umegonga mfupa Zanzibar iachwe kuamua mambo yake solution hapo ni serikali 3 au muungano uvunjike.
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Sawa; Zanzibar iachiwe mafuta yake, lakini wawakilishi hawa wajue kuwa Bara tayari wanachimba gesi na karibuni mafuta yataanza kuchimbwa na wawe tayari kusamehe mgawo wao wa mafuta hayo.

  Wakati wanatayarisha mswada huo, vilevile waje na pendekezo la kugawana mpaka wa baharini kwani ukipima maili 200 za 'International waters' ya Tanganyika, Zanzibar inmezwa ndani ya maji hayo; tusingepende mgogoro huu kukua zaidi ya haya majibizano ya wanasiasa.
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Mipaka ya Zanzibar ni mgogoro pia kwani ukanda wa pwani wote unasemekana umo ndani ya mipaka ya nchi ya zanzibar. Hiyo maili 200 ya international waters is irrelevant kama zanzibar wakijitenga (kwani Tanganyika yetu itakuwa haina bahari (a landlocked country), Kenya pia watapoteza Lamu, na Mombasa ) ukanda wote wa bahari. Nakubaliana nawe huu mjadala hekima na busara itumike badala ya ubabe na kebehi wakijitenga zanzibar pande zote mbili zitaumia.
   
 5. koo

  koo JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika swala la mipaka zanziba ndio watakao liwa sio pwani ya tanganyika lakini hatuna haja yakusema haya mambo yakaliwe kimya kwani kunasiku yatalipuka nivyema tukayazungumza sasa wakati bado tuko na mahusiano. Sioni cha kutushinda kusema hapa licha ya mgao mdogo wa madini tulionao bado wananufaika nao watanganyika hatujawa wachoyo huu ni ubaguzi wakipu-mba-vu unaosababisha naroho yauchoyo lakini naamini hatuna haja yakutunza kidonda shein anapaswa kuitisha mjadala wakizanziba wananchi waamue wanatakaje na wakiamua wanabaki na mafuta kama yazanziba pekee pia waseme wanajitoa katika madini,gesi na mafuta ya tanganyika na ili hili liwe sawa lazima tuwe na serikali tatu ili kila nchi iwe na resouce zake kwa manufaa ya watu wake
   
 6. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Kama Tanzania itapanguka basi mipaka itayotumika ni ile ya ukoloni..........na ndio inayotumika ingawa si rasmi , mfano wale askari wanamaji wa zanzibar hawawezi kuvuka mipaka hiyo mpaka kwa ruhusa maalum,kwani wao wanafanya kazi Zenji tu.

  kuhusu ukanda wa pwani wa Kenya , hii inanisumbua kidogo , kwani kuna wengine wanasema kuwa serikali ya Kenya inatakiwa iilipe Zanzibar kila mwaka kiasi fulani cha fedha , kwani mkataba ni kuwa aina wa fulani ya shirikisho , watu wa pwani wapewe mamlaka yao ya kujiendesha.

  kama hii ni kweli basi Zanzibar wanaweza kudai hizo fedha tangu 1963 mapaka leo na wakishindwa kulipa basi zenji iichukue ukanda wa pwani na hadithi kishwa

  hata kama zenji haitachukua huu ukanda wa pwani basi huu ushaanza na utaendelea kuwa mwiba kwa kenya.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,799
  Likes Received: 5,082
  Trophy Points: 280
  Kakalende,

  ..sheria za bahari na matumizi/mgawanyo wa rasilimali zilizoko baharini ziko wazi. kama kutakuwa na kutoafikiana kwa namna yoyote ile shauri linaweza kupelekwa mbele ya msuluhishi wa kimataifa. Nigeria na Cameroun waliwahi kuwa na mgogoro kuhusu mafuta yanayopatikana ktk eneo la Bakassi na shauri lao lilitatuliwa na mahakama ya kimataifa.

  ..zaidi mipaka baina ya Tanganyika na Zanzibar inajulikana. hiyo ni mipaka iliyokuwepo kabla ya muungano baina ya mataifa haya mawili. wakati OAU inaanzishwa ilikubalika kwamba mipaka yote iliyoachwa na wakoloni iheshimike. sidhani kama itakuwa busara kwa Zanzibar kujitumbukiza ktk mgogoro na Kenya,Msumbiji,Tanzania,na Somalia, kudai kurejeshwa kwa mipaka iliyokuwepo kabla ya utawala wa Sultan Khaliffa wa ZNZ. .

   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mipaka ya Zanzibar Sultan hakuwa ameridhia ule mkataba kwa kuwa ulifanyika kwa ubabe na vitisho. Isitoshe hayo maelezo yako ni hadithi za kusadikika wajerumani ndio wamezungumza na Waingereza wakakubaliana ni sawa na makubaliano ya mto Nile kukabidhi mto Nile Egypt from waingereza walikaa wakakubaliana Alexander huku wakiacha nchi wanachama wengine kama Tanzania, Uganda, Sudan, Ethiopia hawajui kinachoendelea. Kuachia sehemu kunaweza kuwa umelazimishwa au kutishiwa hakumaanishi umeuza eneo.  Sio OAU bali hata UN charter walikubaliana hivyo swali ni mipaka ya Zanzibar ni ipi?
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Mipaka ya Zanzibar ilikuwa inachukua pwani karibia yote ya bara Dar Es Salaam Mombasa na Pwani ya Mozambique Tanga Sijasikia Wazenji Noma Mipaka Ya Ukoloni mkileta mnakwisha Egypt na sudan zilitupiga Bao
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,111
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Hakuna raisi wa Tanzania atakaye kuwa mjinga na kukubaliana na Zanzibar kujitenga maana atauliwa! hata kama katoka zanzibar. Zanzibar imepata 4%-5% kwa miaka yote, umeme, chuo, kazi, balozi, n.k na sasa kwasababu ya mafuta wajitenge! basi walipe madeni yote kwanza! hii haitawezekana na hakuna raisi atakayekubali zanzibar kuwa na pesa zake wakati wamepokea mgao wa 4%-5% kwa miaka zaidi ya 40. Hizi ni ndoto tu mtaleta vita
   
 11. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wazenji wanajua kuwa wakitushirikisha kwenye mafuta yao basi wataumia kama tulivyoumizwa kwenye madini na mijitu yenye tamaa kama kina chenge na rostamu.Wanajua sisi kutoka bara tutawaingiza mkenge wasifaidike na mafuta yao.

  mi nakubaliana nao kabisa ktk hili suala kwani sisi tumeshindwa kutumia madini na gesi yetu na sasa tumeanza kuzengea mafuta yao.Wazenji msikubali hili kabisa.
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuna baadhi ya malalamiko nawaelewa wa Zanzibar na kuna mengine mengi zaidi huwa nawashangaa tu. Ila katika yote hayo nawashangaa ni kwa nini wana poteza pumzi kulalamika katika chaneli ambazo hazina mamlaka ya kufanya chochote. Kwa nini hatusikii Wazanzibar wakiandamana kushinikiza serikali yao kuwakilisha madai yao? Kwa nini kila leo tunasikia wananchi wa kawaida wa Zenji wakilalamika huko serikali yao ikiwa kimya? Kama Zanzibar inataka uhuru zaidi au uhuru kamili nawashauri wabadilishe strategy kwa maana hii ya sasa haita wafikisha popote.
   
 13. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hayo unayoyafikiria yatatokea...kwani kila kitu kinataka muda, na hivi sasa amini usiami siasa za zanzibar zimehamishiwa misikitini...wanafanya hivyo baada ya kuona viongozi wao hasa wa ccm wanashindwa kutetea maslahi ya wazanzibar, kwa manufaa ya ccm. Watu wanahamasishwa na sio muda mrefu sana tutaanza kuona matokeo kama ya kule Nigeria,Uganda na sehemu nyengine...Kitu kibaya sana dini ikiingia katika siasa...Lakini wazanzibari hawana budi, wemefanywa kuwa " desperate "sasa tusubiri matokeo
   
 14. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jambo moja ambalo hawa wenzetu wa bara ambalo linanishangaza siku zote, ni ile dhana ya kuwa wametutawala na kila kinchoambatana na jambo hllo ikiwa ni pamoja na dharau dhidi ya Zanzibar.

  Issue yoyote inayokuja kuhusu "muungano", huwa wanazungumza kama kwamba hali hii ndio iliokuwepo dum daima. Wanasahau kuwa Zanzibar ni partner katika huu "muungano" na wanataka tubadili dhana hio na kujiona kama mkoa miongoni mwa mikoa yao.

  Mzanzibari yoyote mwenye akili timamu hakubali hali hio na Zanzibar hamuwezi kuifuta katika ramani ya dunia.

  Suala la mafuta sio issue pekee kwa mustakabal wa Zanzibar kwani Wazanzibari wasichotaka ni huu "muungano" ambao kila siku Zanzibar inapoteza madaraka na mamlaka yake kwa Tanganyika. Resources si mafuta tu katika Tanzania na mbona Zanzibar hainufaiki na madini mengi yalioko bara ikiwamo hata hio gesi inayopatikana huko bara. Msifanye kuwa mafuta ndio issue, "muungano" wenyewe ndi issue na sisi hatuutaki.

  Sasa nyinyi chongeni lakini mjue kwamba Zanzibar itabakia kuwa Zanzibar na iko siku mtapanua wenyewe.
   
 15. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,773
  Likes Received: 6,105
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red. Naona umeshazuka tena mjadala mwingine zaidi ya Zanzibar kujitenga (Muungano kuvunjika); mipaka ya Zanzibar ni ipi? Kama wanadai mipaka yao inaishia/inakula hadi sehemu ya pwani za Kenya, Tanganyika, na Mozambique jibu ni rahisi mno, kama ilivyofanyika huko Sudan ya Kusini, ingekuwa pia vyema wakaazi wa pwani husika nao wakapiga kura ya maoni whether wanataka "kubaki" upande wa Zanzibar au katika nchi zao za sasa halafu mtaona habari yake!

  Wala tusichelewe, hebu tuwaulize wale wamakonde wa kule Msumbiji na Tz, wamatumbi, wakwere, wayao, wazigua, n.k halafu tutapata jibu ambalo hata mwendawazimu anaweza kuli-guess.
   
 16. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Ni nani aliyempa Sultani Zanzibar?
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,799
  Likes Received: 5,082
  Trophy Points: 280
  Mdondoaji,

  ..there r just too many documents zinazoonyesha kwamba Sultani Khallifa alichukua pesa in exchange ya eneo la pwani ya Tanganyika.

  ..i havent researched on what events took place mpaka kufikia kupoteza na maeneo mengine mfano pwani ya Msumbiji. pamoja na hayo, kwa upande wa eneo la pwani ya Tanganyika, the fact is Sultani aliliuza kwa Wajerumani na kupokea pounds 200,000.

  ..I really doubt it kama wa-Zanzibar wanaweza kuirudisha tena himaya iliyokuwepo kabla ya utawala wa Sultan Khallifa. naamini kwamba ili wafanikiwe wanapaswa kuungwa mkono na wakaazi wa maeneo hayo ya ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki. wakaazi hao hawajitambulishi tena kama wa-Zanzibar na hakuna dalili zozote zile zinazoonyesha kwamba watakuwa na mwamko wa kuwa wa-Zanzibar hivi karibuni.
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jokakuu,

  You have a point mkuu kwenye kipengele cha wakaazi wa maeneo hayo kuulizwa kama wanataka kujiunga na Zanzibar au la. Ila mie niliwahi kufanya utafiti kanda ya pwani sana sana maeneo ya Lamu, Mombasa, Tanga, Bagamoyo, Lindi, Mafia na nikakuta watu wengi wa huko wanaundugu wa karibu na watu wa Zanzibar na Pemba. Kiswahili chao sio kiswahili cha maeneo mengineyo na wengi wao bado wamehifadhi historia ya ukoo zao. Hivyo itakapoitishwa referendum kuhusu hilo jambo napata wasiwasi kama litakuwa vile unavyofikiria. Pengine Msumbiji ila ukanda wa pwani wa Tanzania na Kenya hali ni tofauti usichukulie Dar-es-Salaam ndio ukanda mzima wa Pwani.

  Kuhusu document ya kucease the sovereignty of Zanzibar, historia inayoofahamika sana ni ile iliyoandikwa na wajerumani na waingereza ambayo imejaa controversial issues. mfano hapa:-
  "
  In 1873 the British Navy compelled Sultan BARGASH to abolish slave trade).
  The British have long played a role as advisers to the Sultan of Zanzibar. In 1877, Sultan Bargash, in communication with the Germans, refused a British protectorate; in 1880, Germany's chancellor Bismarck rejected a request by the Sultan of Zanzibar for a German protectorate. In 1886, Britain and Germany, both interested in the acquisition of colonies, agreed on partitioning the mainland territories of the Sultanate, ostensibly to suppress the slave trade the Sultan had nominally abolished and was unable to suppress, technically while respecting the Sultan's sovereignty. Britain would receive British East Africa (Kenya), while Germany would receive German East Africa (Tanzania).
  Zanzibar, i.e. the islands of Zanzibar and Pemba, remained independent until 1890. "

  Picha hii inaonyesha kwamba tamaa ya wakuu hawa ilipelekea kuhamasisha makubaliano ya kugawa ukanda wa pwani for their intentions. The Sultan of Zanzibar alipokubalia kuachia eneo hilo kwa £200,000 sijakutana na mkataba wa mauziano baina ya hawa wawili. Isitoshe waingereza nao walitoa bei gani kuachiwa eneo la Lamu na Mombasa? Mozambique pia wareno walilipa kiasi kwa Sultan of Zanzibar?
   
 19. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Naona Swali langu la " ni nani aliyempa sultani Zanzibar limeshindwa kujibiwa".

  Je Dar-es-salaam kwenye Ikulu ya Tanzania nayo ni Zanzibar?.
  mimi binafsi namuona Sultani naye kama mkoloni tu, kwa hiyo Wakoloni kwa Wakoloni kuraruana katika vita/kudhulumiana wao kwa wao sisi haituhusu. nchi tulizozikomboa kutoka kwa hawa wakoloni zina mipaka yake inayoeleweka, Tukizungumzia Tanganyika tunajua ni mainland na visiwa vya mafia na vinginevyo vidogovidogo, Tanganyika ilikujaje? sisi haituhusu!, kama sultani alidhulumiwa hiyo ni shauri yake, kwa nini yeye hakudhulumu?, kama alishinikizwa hiyo ni shauri yake kwa nini yeye hakushinikiza?, kama alilipwa pesa hewala, sisi hiyo haituhusu.

  Je ni Zanzibar ipi iliungana na Tanganyika?, na Tanganyika ipi iliungana na Zanzibar?, je ni himaya ya Zanzibar iliyoungana na Tanganyika au ni "Zanzibar" iliyoungana na Tanganyika?.

  Kama Wazanzibar wanaitaka himaya ya mkoloni sultani, basi waidai hata Oman maana kiasili sultani wa Zanzibar na Oman alikuwa mmoja kabla ya baadae kutengana
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,799
  Likes Received: 5,082
  Trophy Points: 280
  Mdondoaji,

  ..off course kuna muingiliano[damu,Dini,uvuvi,biashara,...] mkubwa baina ya wakaazi wa pwani ya Afrika Mashariki na wale wa visiwa vya Unguja na Pemba.

  ..ninachokiangalia mimi zaidi ni IDENTITY ya Uzanzibari.

  ..je, hawa wakaazi wa Pwani ya Afrika Mashariki wana haki ya kutambuliwa na kujitambulisha kama wa-Zanzibari?

  ..Je, hawa wananchi wananchi ya pwani ya Afrika Mashariki[Dsm,Kilwa,Bagamoyo,Tanga,Lindi,Mtwara,Lamu,Mombasa..] wamewahi hata wakati mmoja kutamani, au kudai, kujitambulisha/kutambuliwa kama wa-Zanzibari? Yaani kuunganishwa pamoja na wenyeji wa visiwa vya Unguja na Pemba?

  ..Je, Waunguja na Wapemba wanawatambua wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki kama wa-Zanzibari wenzao, tena wenye haki sawa na wao?

  ..nimewahi kuwasikia baadhi ya wa-Zanzibari wakidai viongozi kama Karume,Jumbe,Ali Mwinyi, kuwa si wa-Zanzibari. Hoja yao ni kwamba viongozi hao wana asili toka ukanda wa pwani ya Tanganyika.


  NB:

  ..katika kufuatilia kwangu historia, sijaona mahali popote pale ambapo Sultani aliwaunganisha kijamii na kiutawala wenyeji wa ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na wale Waunguja, na zaidi wa Oman. The Sultani treated these areas as simply trading posts. Nothing more than that.​

   
Loading...