Mafuta ya Binadamu Yawa Dili

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Polisi nchini Peru wamewakamata watu watatu miongoni mwa kundi la wauaji ambao wamekuwa wakiwaua watu kwaajili ya mafuta ya miili yao ambayo wamekuwa wakiyauza kwenye makampuni ya ulaya kwaajili ya kutengeneza madawa ya urembo

Polisi nchini Peru wamewatia mbaroni watu watatu ambao ni wanachama wa kundi la wauaji wanaojificha kwenye misitu ya Peru ambao huwaua watu kwaajili ya mafuta ya miili yao na kisha kuyauza mafuta hayo ya binadamu kwa mashirika ya madawa ya urembo ya ulaya.

Wauaji hao watatu waliokamatwa walikutwa wamebeba chupa za mafuta ya binadamu ambazo walidai yana thamani ya dola 60,000. Kila lita moja ya mafuta ya binadamu inadaiwa kuuzwa dola 15,000.

Watuhumiwa hao watatu waliokamatwa walikiri kuwaua watu watano lakini idadi ya watu waliouliwa na kundi la wauaji linalojificha maporini inakisiwa kuwa kubwa sana.

Wauaji wa kundi hilo huwateka watu na kuwapeleka porini ambako huwaua na kisha kuyatoa mafuta ya miili yao.

Hadi sasa jumla ya watu 60 hawajulikani walipo katika mji wa Huanuco ambako wafanyabiashara hao wa mafuta ya binadamu wanafanya mauaji yao.

Wauaji waliokamatwa waliowaonyesha polisi sehemu waliyowaua watu watano na kisha kuikata kata vipande vipande miili yao na kisha kuvibanika vipande hivyo kwenye moto ili mafuta ya miili yao yatoke na kuangukia kwenye chupa walizoweka chini yake.

Polisi wanaamini kuwa mafuta hayo ya binadamu huuzwa kwa wafanyabiashara katika mji mkuu wa Peru, Lima na kisha huuzwa kwa njia za panya kwa makampuni ya madawa ya urembo ya ulaya.

Source: www.nifahamishe.com
 
Back
Top Bottom