Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta(EWURA) imetangaza ongezeko la gharama za mafuta nchini kuanzia kesho Julai 05, 2016 kutokana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo duniani.
Petroli itauzwa shilingi 1888 badala ya shilingi 1865 ya sasa huku Diseli ikiuzwa shilingi 1720 badala ya shilingi 1633 na Mafuta ya taa nayo yakiuzwa shilingi 1687 badala ya shilingi 1607 ya sasa.
Saa chache baada ya wafanyabiashara kugundua kupanda huko kwa bei baadhi ya vituo vimefungwa kusubiri bei mpya ambapo onyo limetolewa juu yao.